Tanzania Hatarini Kuwekewa Vikwazo Na Umoja Wa Ulaya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Hatarini Kuwekewa Vikwazo Na Umoja Wa Ulaya.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Oct 6, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimeanza harakati za kuzishawishi nchi za Jumuiya za Ulaya kuweka vikwazo kwa Tanzania kutokana na matatizo yanayojitokeza katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapigakura linaloendelea visiwani Zanzibar.

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho, Mhene Said Rashid ambaye yupo mji wa Stockholm nchini Sweden akijaribu kuzishawishi nchi za ulaya ya kaskazini kuweka mbinyo kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya zanzibar kwa kutoheshimu demokrasia.

  Mjumbe huyo ambaye anatarajiwa kutembelea katika nchi za Finland, Sweden na Denmark na kuonana na wajumbe mbali mbali kwa lengo la kuzishawishi nchi hizo ambazo zinaifadhili tanznaia katika suala zima la kusimamia demokrasia nchini.

  Akizungumza katika Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW) jana asubuhi Rashid alisema lengo la safari hiyo ni kuzishawishi nchi zinazoifadhili Tanzania ziwache kuisaidia kutokana na kutoheshimu misingi ya demokrasia kutokana na wananchi wa zanzibar kunyimwa haki yao ya kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapigakura linaloendelea hivi sasa ambapo kikwazo kikubwa na kukosekana kwa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi.

  "Hakuna suala la kuingilia mambo ya ndani jambo la msingi ni kuwa unposema unasaidia fedha kwa kusaidia aktika shughuli za uchaguzi ni pamoja na demokrasia na misingi yake, halafu ushindwe kusimamia demokrasia yenyewe hilo ni tatizo kubwa" alisema Rashid alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa Dw.

  Nchi ya Sweden hivi sasa ni raia wa jumuiya za ulaya na ina nafasi kubwa katika kuzishawishi nchi nyengine za jumuiya hiyo katika kufuatilia suala la demokrasia ambapo nchi hizo zinatoa fedha nyingi kuisiadia tanzania katika uchaguzi mkuu ujao wa 2010.

  "Tuna matatizo ya uandikishaji na hivi sasa umeanza kw avurugu na watu wnegi hwana vitambulisho na daftari hili ndilo litakalotumika katika upigaji kura tunajua nchi nyingi zinatumia vutambulisho lakini kwa misingi ya haki sisi kwetu hakuna haki inayotendeka" alisema Mkurugenzi huyo.

  Alisema lengo kuu ni kuzielewesha nchi za ulaya zifahamu kwamba Tanzania na hasa Zanzibar hakuna demokrasia ya kweli katika chaguzi zinazofanyika hivyo kama nchi hizo zina uwezo wa kusaidia ziweze kuisaidia Zanzibar iweze kufuata misingi ya sheria na haki.....


  SOURCE:ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Labda Mh. Kikwete unaweza kuzinduka kutoka usingizini kuwa Chama chako ni tatizo na kikwazo kikubwa cha nia njema na maendeleo ya demokrasia Zanzibar. Sasa tutapigana kwa kucha na meno kushinikiza lolote zuri kwa maendeleo ya demokrasia ya kweli visiwani, ikibidi hata kwa Tanzania yote ku-suffer.Potelea mbali we are tired na manyanyaso yasiyo kwisha.
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Cha Msingi sio kutoa shinikizo la kukata msaada ila ni kuhakikisha kuwa wao wanakuwa washindi katika uchaguzi mwakani, Na pengine ni kujua na kuwamashisha watu katika kulinda kura zao na pengine katika kufanya mambo mengine ya msingi katika siasa zetu
   
 4. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu hilo halitokei kutokana Ulaya na Marekani pamoja na Ulimwengu mzima inatambuwa kuwa Tanzania ni nchi ya Majuha ,kufanya hivyo kutawakosesha wao kuchukuwa kilichomo ndani ya Tanzania, hususan ukiangalia kila nchi hivi sasa inahakikisha inaweka mrijayake Tz .
   
 5. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Vikwazo wawekewe eti kwa sababu ya kelele za CUF who care CUF after all it is "alleged muslim party" hapo CUF wamedoda!
  Strategy ni moja tu "mapambano yenye kuleta maumivu ya moja kwa moja kwa wana CCM"
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  waweke vikwazo tu tutakwenda mbele mbona Commrade mgabe anadunda?
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Lakini CUF nao wana udini sana ndo maana hata EU hawa hangaiki nao sana
   
 8. O

  Omumura JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sio udini tu, hata hivyo pamoja na hayo bado hawaaminiki vile katika macho yenye matongotongo ya watanzania wengi.Anyway, bora zimwi likujualo.......!
   
 9. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  mbona wananchi wake wanakufa njaa?
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Namsubiri huyo mjumbe hapa Finland
   
 11. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ndoto za Alinacha!

  Amandla...
   
 12. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Halafu hao CUF watafaidika vipi Tanzania ikinyimwa misaada!?

  Ukichaa mtupu!
   
Loading...