Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,480
- 35,371
Habari za asubuhi waungwana!
Nimeamka salama nimekutana na habari moja ya ugunduzi wa madini katika Kijiji fulani huko Mtwara a.k.a Ntwala.
Nikajisemea moyoni kuwa bado hayataleta impact kwa taifa ingawa wananchi wachache watanufaika kwa kupata vibarua huko.
Nimebahatika kufanya kazi kwenye mgodi mkubwa zaidi wa dhahabu Tanzania, nimebahatika kufanya kazi kwenye hifadhi kubwa zaidi Tanzania, na nimebahatika kupita kwenye rasilimali kadhaa Tanzania. Hakika ni utajiri juu ya utajiri.
Hatuhitaji kugundua aina mpya ya madini, hatuhitaji kugundua rasilimali zingine kwa sasa.
Tuna hifadhi za wanyama lukuki
Tuna mito lukuki
Tuna maziwa lukuki
Tuna gesi nyingi
Tuna madini lukuki
Tuna fukwe za mahari kutoka kaskazini mpaka kusini mwa nchi.
Tuna ardhi inayosapoti karibu aina zote za mazao( Tanzania ina mikoa yenye uoto tofauti).
Tuna anga salama na kubwa
Je, kama hivi vyote vimeshindwa kuuondoa umaskini miongoni mwa Watanzania unadhani kuna haja ya ugunduzi wa rasilimali zingine?
Jibu ni hapana.
Tanzania hata tukiwa na dhahabu au almasi kila mtaa bado umaskini utaendelea.