Tanzania hata jiwe linaweza kuwa kiongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania hata jiwe linaweza kuwa kiongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Mar 10, 2011.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama mtu ambaye hajui umaskini wa watu wake zaidi ya 75% unatokana na nini ameweza kuongoza tena kwa vipindi viwili basi nchi hii inaweza kuongozwa na mtu yeyote hata Sophia Simba na mambo yakaendelea kama kawaida. Kwa hali hii kama kunauchawi basi sisi tumelogwa na aliyetuloga ametupa funguo baharini kwenye kina kirefu.

  Nijambo la kusikitisha kuona kuwa pamoja na nchi yetu kuwa rasilmali nyingi hatuna hata dalili ya kutoka kwenye umasikini uliokithiri tatizo ni kukusa mkakati wa kuwawezesha wananchi wazawa kumiliki uchumi wetu kwa kukosa viongozi wenye maono na uchungu kwa nchi.

  Viongozi tulionao leo hii wengi walikuwa wanataka ukubwa tuu hawakuwa na uwezo hata na uchungu kwa watanzania dhamira yao ilikuwa wapate ukubwa na heshma basi lakini watambue kuwa heshma wamepata lakini iko siku watajibu wamewafanyia nini waTanzania.
   
 2. Freddy81

  Freddy81 Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hiii ndo changamoto kwetu sisi vijana, tusipobadilka sisi hatutafika kwenye nchi ya ahadi, wazee wetu wamegoma kubadilika sas it is our turn
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa mfumo uliopo unayoyasema ni ya kweli, lakini kwa bahati nzuri mambo yanabadirika haraka; kwani katika mfumo wa sasa, ilikwisha zoeleka ya kuwa rais ni lazima atoke CCM, na huko CCM kwenyewe utaratibu wa kumpata mgombea urais mpaka sasa hauko wazi, umejaa mizengwe mitupu. Lakini kwakuwa watanzania hivi sasa wamezinduka, CCM ikipitisha mgombea hasiye na sifa, atapigwa tu kwenye kura hata waibe namna gani.
   
 4. IFM

  IFM Member

  #4
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera sana kwa mawazo yako ni mazuri na mimi kila siku ndo nilikuwa nawadha hivyo kuwa kwa dalili hizi hata Kichaa wa Mirembe anaweza kuwa RAIS WA TANZANIA YA SASA. Ni ukweli usiopingika kuwa CCM ya sasa na udhalimu wao hawawezi kubadilika......ni aibu kubwa Rais wa nchi anaposema nchi yake ni masikini lakini hajui umasikini wao unatokana na nini wakati nchi yake ina utajiri wa kila aina.

  mi ninahasira sana na nchi yangu.. nikikumbuka kipindi cha nyuma kama kweli watanzania tuliweza kupiga kura kuchagua either picha ya mwl/ Mwinyi ama kivuli bila kuhoji basi TULIKUWA TUMELOGWA!! yaani hakuna hata aliyeuliza?
   
Loading...