Tanzania hakuna wacheza filamubali wacheza maigizo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania hakuna wacheza filamubali wacheza maigizo

Discussion in 'Entertainment' started by CHUAKACHARA, Apr 10, 2012.

 1. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Hopeless Tanzanians (SOME, NOT ALL), mijitu inalia (HASA WANAWAKE) eti Kanumba (RIP) alikuwa mcheza sinema kafa, hapa Tanzania hakuna mcheza sinema bali mcheza maigizo. Ni michezo ya kuigiza tu hakuna filamu hapa!!!
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu hamna filamu hapa yote tunayona ni maigizo Kama ya kanisani tuu
   
 3. jimjamtz

  jimjamtz Senior Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 147
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kweli mtupu nakubali kabisa.Mtu uwezi kuigiza sinema 40 kwa mwaka! sinema moja yaweza kuchukua mwaka kuendelea.Eg 10 commandment took 15yrs!!!!
   
 4. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,640
  Likes Received: 2,002
  Trophy Points: 280
  kweli mkuu! Haya yetu ni maigizo daraja la nne ngazi ya wilaya....hakuna sinema hapa.
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Una uhakika kwamba hii thread yako ulipaswa kuipost hapa jukwaa la siasa? au hii habari ni siasa?
   
 6. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Mkuu kila mtu ana haki ya kuamini na kukililia kile anachokiona kinampa furaha.. Kuwatukana na kuwaita majina haitasaidia bali itakufanya uonekane una hulka ya kidikteta.. Unaamini la kwako ndilo liko sawa.. Hiyo haiko fair hata kidogo.. Kuwa na yako unayoyaamini bila ya kuponda waaminio wenzio..
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  subiri tunakuja kufanya filamu sasa
   
 8. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ndio nashangaa mcheza "filamu" za mahusiano anakufa kwa wivu wa mapenzi,kanumba wasnt a "badass"
   
 9. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  kanumba was a video clips star
   
 10. Chali wa Moshi

  Chali wa Moshi JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  wewe kama sio mwehu, Noah Ramsey kacheza picha ngapi 2009?

  yeye nimcheza filamu au maigizo??
   
 11. k

  kwitega Senior Member

  #11
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acheni umbumbumbu jamani. Hao Nollywood na Hollywood walianzaje? Chako ni chako hata kama kikiwa ni kidogo, kibovu. Kinachotakiwa ni kukikuza au kukiboresha. Kucheza filamu nyingi au chache inategemea na aina ya filamu, mazingira na malengo ya filamu yenyewe. Tusijifunge mawazo yetu kama kifaranga kwenye boksi, lazima twende mbali zaidi ya hapo. Wewe unayeropoka, ukifa leo tutakukumbuka kwa lipi? si ajabu hata barozi wako wa nyumba kumi asifike kukuzika. Bora wasanii wetu wakiwemo wacheza filamu, maigizo na wanamziki wanaonyesha walau mchango wao kwa taifa. wewe mchango wako ni upi? au kupiga soga kwa domo lisiloonja mswaki? shut up!
   
 12. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hatuwezi kuwasapoti wazinifu kama kanumba.
   
 13. J

  Jonas justin Member

  #13
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijakuelewa napia mbona unawakatisha tamaa ndugu zetu halafu inavyoonekana watu walivyo uchukulia msiba wa kanumba wengine vimekuumeni sana..
   
 14. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kwani Ramsey Noah ni nani??
  Kwani soko la Nollywood lina rates zipi kwenye standards za filamu duniani??
   
 15. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mkuu punguza jazba, twende taratibu!
  Kwani Nollywood na Hollywood wapo sawa?

  Dhana ya chako ni chako imekaaje hapo Mkuu?

  Unawajua wamiliki wa tasnia ya filamu nchini ni nani hasa?

  Wasanii wetu au waigizaji wetu ni makarai tu yanayotumiwe kwenye ujenzi.....!

  Hivi kumbukumbu za TRA zinasema filamu za Kanumba zimeliingizia taifa shilingi ngapi vile?

  Wabongo tusiwe watu wa kusombwa na mkumbo jamani.....
  Nilisikitishwa na msiba wa kijana mwenzangu ila utiaji chumvi uliopitiliza na kufanya watu mazuzu umenichefua kabisa!
   
 16. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Chuakachara sinema au filamu au movie zialianzia na michezo ya kuigiza na taratibu zikanakshiwa na kuwa sinema/filamu/movie.. hapo zamani mashuleni tulikuwa na drama au michezo ya kuigiza ( sanaa za maonyesho) ambayo ni daraja la chini katika kuweka kwenye matendo themes mbalimbali. kali yako ni sawa na kuponda hatuza za mwna kutambaa .kusimama dede na hatimaye kutembea. Hollywood,Bollywood Nollywood walianzia mbali kama tunavyoona Tollywood ya kina Kanumba, Kagozi, Dr, Cheni, JB , Woulpers na wengineo kaka!!! Fani ilipokomaa ndo vikorobwezo vikaanza...
   
 17. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #17
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hamna kiliyemuuma, ila tupunguze unafiki.....
  Hii tasnia ni bado sana kuliko masifa ya kijinga yanayomwagwa,
  tuache blah blah tujadili sanaa kwa upana wake Kanumba alikuwa ni muigizaji mwingine tu kama kiungo kimoja kwenye soko liliooza!
   
 18. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #18
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli itabidi waache ile tabia ya kuongea sauti za kuvuta ambazo sio watanzania asilimia kubwa tuongeavyo.

  Mie niliboreka sana na movie za kibongo kwa sababu ya kuweka sauti feki yaani ukilala ukisikia uwezi jua yupi ni yupi kabisa anayeongea hata wanaume nao duh hadi inaudhi.

  Ona sinema za ki nigeria hata ukiwa umelala mtu unasikia sauti unajua ni actor yupi anaongea bila kuangalia tv hata kwenye redio. Na hiyo imewafikisha mbali sana kimaendeleo.

  Nyie ma producer acheni kuaribu sauti za watanzania mie siongei hivyo kuvutaaaaaaaa kuvutaaaaaa hadi inaudhi na wanaume nao wanavutaaaaaaaa
   
 19. b

  blackwizard Senior Member

  #19
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huo ujinga kusifia ujinga
   
 20. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #20
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mkuu napingana na hoja ya kuipandisha Nollywood kwenye ngazi za Bollywood na Hollywood!
  Kiukweli kwa kuweka kumbukumbu sawa Nollywood ipo chini sana ukilinganisha na hao wakongwe, soko la Nollywood ni la afrika humu humu na sana sana ndani ya Nigeria ukizingatia nguvu ya soko lao kutokana na wingi wao.....
  Hizo idara zingine za sanaa ulizoainisha kama ngoma, maigizo ya majukwaani ni kweli ndio msingi wa filamu lakini cha kusikitisha sana hapa kwetu hvyo vitu hamna tena hvyo ni kama tumeua misingi sasa jee tasnia itasimama vpi? Wasanii wanapikwa wapi?

  Tollywood ni zao la wajanja wachache ambao wala hawana utashi na sanaa na wanataka kuaminisha umma kuwa kabla ya uwepo wao eti hapa kuwa na filamu nchini,

  Huu ni uongo, filamu nchini zilikuwepo toka enzi za wakina Prof Amandina Lihamba kuna filamu nimeisahau jina huwa inaonyeshwa na tbc ni filamu ya kitanzania imeigizwa miaka ya tisini.....!
  Filamu ziliigizwa na chuo cha sanaa cha bagamoyo wakina Vitalis Maembe, Irene Sanga na wengine kibao!
  Mwanzoni mwa tamasha la ZIFF filamu nyingi za kitanzania zilizoshiriki ni zile zilizoshiriki kwenye matamasha ya ulaya na kufanya vizuri.
  Tulikuwa na fursa nzuri sana ya kufanya vizuri zaidi katika tasnia kama tungezuia makanjanja kwa idara husika kusimamia na kufanya!

  Tuache mbwembwe za kutaka kumtukuza Kanumba tuangalie hali ya Tasnia kwa ujumla wake tumeacha njia.
   
Loading...