Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 259
- 353
Ukweli sio kama ni mbaya au mchungu kama wasemavyo wahenga, ila uchungu na ubaya wake huja kulingana na maandalizi ya kuupokea. Ukitayarisha akili yako kupokea ukweli wakati wowote wala haitokuwia ugumu kuukubali na kuendelea na maisha yako. Tatizo ni pale tu ukweli unapokuja kisha hukuandaa akili yako kuupokea, utaumia tu.
Kichwa cha habari cha makala yangu hii mafupi ni ukweli ambao utakuwa shubiri kwa wengi hapa JF na kwingineko. Kwanini nasema Tanzania hakuna vyama vya upinzani vyote ni CCM tu? Nitatoa ufafanuzi.
Upinzani wa kweli Tanzania ulikuwa ule wa kabla ya 1965, ila baada ya Katiba ya 1965 iliyotambua TANU pekee kuwa chama cha siasa, vyama vya vyote vya upinzania vimekuwa vyama vya mchongo tu kama mifereji ya kujipatia fedha.
Vyama vyote vilivyoazishwa baada ya sheria ya vyama vya vingi ya 1992 vyote ni vyama vya mchongo na hadi leo vinajiendesha kimchongo tu. Wasomi wa Political Science wanajua vyama vya upinzani huchipua vipi na katika mazingira gani, kwa mazingira ya vyama vya Tanzania ni wazi kabisa vilianzishwa kimchongo. Unajua ilikuwaje?
Wakati Tanzania inapita ukata wa hali ya juu kuanzia mwaka 1980 baada ya vita na Uganda hadi mwaka 1985, Tanzania ilikuwa kwenye shinikizo kubwa kutoka nchi za magharibi kukubali baadhi ya masharti kama kupunguza thamani ya fedha, kukubali demokrasia ikiwemo vyama vingi, kubinafsisha mashirika ya serikali na kadhalika ili tu ipokee misaada ya fedha kutoka IMF na WB kunusuru uchumi wetu. Hapo ndio michongo ya vyama vingi ilianzia.
Hapo chama kilikuwa kimoja tu, CCM kilichabadili jina kutoka TANU 1977. Wazee kwa busara zao wakachaguana ndani ya CCM humohumo na kwenda kuazisha vyama vya siasa kuwacheza shere wazungu ili tupate fedha. Wakati huo Urusi mtu wetu wa nguvu dhooful-hali, China naye hayuko sawa sana, ikawa hatuna namna tukubali tu masharti ya Magharibi.
Kuanzia hapo akina Mtei wakaazisha CHADEMA, akina Mrema wakaja na NCCR - Mageuzi, CUF, TLP na vyama kibao vikafuata hadi leo tuna vyama zaidi ya 25 na ukitazama kwa karibu zaidi ya 90% ya waasisi wa vyama hivi wakati fulani walikuwa wafuasi warekeketwa wa CCM.
Bado kuna mtu kila siku anawaza kwamba kuna siku CHADEMA au chama kingine kitakuja kushika dola Tanzania, huwa nacheka na kumuombea dua kwa Mungu amtue mzigo huo wa ujinga, maana ni adhabu kwake. Hakuna nadharia hata moja kwenye sayansi ya siasa ambayo inafiti kuelezea namna vyama vya siasa Tanzania vilivyoibuka. Ni wazi kwamba ulikuwa mpango uliopangwa kwa lengo fulani, na sio madhumuni mahususi na ya dhati ya ukombozi wa watu na mali zao.
Ndio maana unaona ni rahisi sana mtu leo kuwa CHADEMA, kesho yuko CCM. Tena sio mtu mdogo, bali mtu wa nafasi kama ya Waziri MKuu mstaafu au nafasi yeyote kubwa. Vyama hivi vya upinzani vinafanya kazi miaka yote kutoa tu uhalali kwamba Tanzania tuna vyama vingi, na mwisho wa siku kila chama kinakula hela yake kwa kazi nzuri ya kuidanganya dunia kwamba Tanzaia tuna vyama vingi.
Tanzania inaweza hata kudanganya dunia kumfunga kiongozi mkubwa wa upinzani gerezani kwa muda mrefu kuonesha namna siasa za vyama vingi zilivyochangamka Tanzania. Viongozi wale kule ndani nani anajua wanaishije? Nani anajua wanakula kitu gani au wanalala wapi? Wakitoka hao wanakwenda zao Ikulu kukutana na marafiki zao ambao sisi tunaamini ni maadui. Huwa nacheka sana.
Kubwa mtambue tu kwamba siasa za upinzani Tanzania ni kiina macho tu. Nyie hamuoni vyama vya upinzania hapa tu nchi za maziwa makuu vinavyokuwa? Acheni utani Tanzania hakuna vyama vya siasa ni miradi ya watu hii.
CCM is here to stay, na hata vyama vya upinzani vinavyoanzishwa vinajua wazi kwamba ni ndoto kushika dola. CCM imefikia hatua ambayo haiitaji tena watu au kura ishinde uchaguzi. CCM ina mbinu zaidi ya 10 za kushinda Uchaguzi bila hata kupata kura. Sasa ni chama utashindana nacho hicho?
Wakati tunakaua makoo maskani kubishana CHADEMA na CCM, na hata kupigana na kujeruhiana kisa vyama vya siasa, tutambue kuwa maumivu yetu ni mtaji mkubwa sana kwa watu fulani mahali fulani. Narudia tena, Tanzania hakuna upinzani, vyama vyote ni CCM.