Tanzania hakuna Ukabila wala Udini lakini kuna Makabila na Dini

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Tanzania Hakuna ukabila wala udini lakini kuna makabila na Dini.

kipindi cha awamu ya Tano Wananchi wengi na wadau wengi wa mtandao wetu pendwa wa JamiiForums walikuwa wakieneza propaganda kuhusu uteuzi na ajira kipindi cha miaka iliyo pita ulikuwa ukihusisha ukabila na kutaja kabila moja wapo kutoka kanda fulani kuwa ndio wenye nafasi serikali na ndio wenye uwezekano mkubwa wa kupata ajira kitu ambacho siyo. Wadau walisahau kufanya ulinganifu wa idadi ya kabila husika kuwa ni idadi kubwa sana maana Tanzania yenye makabila Zaidi ya 120 kabila hilo limechulukua asilimia 16 Kati ya 200 ya makabila yote.
Je, kipindi hicho Wadau hawakuona kama serikali iliweka hata watu wa Kabila fulani?

Lakini wadau hao hao katika kipindi hiki cha awamu ya sita wamejikita pia kueneza propaganda kuhusu uteuzi na ajira kipindi hiki umejikita katika Dini fulani kisa tu aliye shika Muhimili mkubwa anatokea Dini hiyo. Wadau wanalinganisha teuzi za hivi karibuni kujikita katika Dini hiyo kitu ambacho Kasomi nakemea kwa ulinganifu wa kuwa pengine Mimi si mmoja wa Dini hiyo hivyo mbona kuna watu wa Dini na Imani fulani wapo serikali na hakuna kwani anae fahamu hayo?

Kitabu cha Profesa Mearsheimer kinaeleza sababu mojawapo ya serikali kutotoa taarifa halisi na kamili wakati fulani. Kama kutoa taarifa rasmi kunaweza kuleta mjadala mkubwa zaidi kuliko kutoa taarifa kidogo, hilo limefanyika mara nyingi ikiwamo wakati wa mgogoro wa baina ya Marekani na Urusi kuhusu makombora ya Cuba (Cuban Missiles Crisis).

Yapo malalamiko kwamba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kumekuwa na tatizo la watu kupewa vyeo na ajira serikalini bila kuzingatia uwiano walau wa maeneo na dini. Mwanahistoria maarufu wa Tanzania, Mohamed Said, hivi karibuni alitoa chapisho mitandaoni lililoonyesha kwamba katika miaka sita iliyopita; uteuzi katika nafasi za mawaziri, wakurugenzi, viongozi wa halmashauri na wengine ulikuwa na uwiano wa asilimia 80 kwa Wakristo na 20 Waislamu. Yapo pia malalamiko kwamba kuna makabila yalinufaika zaidi na uteuzi kuliko mengine.

Kuna uwezekano kwamba serikali inataka kujiridhisha na kufahamu ukubwa wa jambo husika. Hoja hii inatiwa nguvu na ukweli kwamba walau kwa sasa, wanaotakiwa kutoa taarifa hizi ni wale ambao tayari wako serikalini na si wanaoomba. Huenda zoezi hili litaipa serikali nafasi ya kufahamu kama kuna tatizo na namna ya kubadilisha mwelekeo. Hii ni kama sababu za kutaka watu wataje makabila na dini ndiyo zile za Munyendo.

Na kama hii ndiyo sababu halisi, kama ambavyo Mearsheimer aliandika miaka michache iliyopita, sioni namna ya serikali kutoka hadharani na kusema sababu halisi ndiyo hiyo. Ikifanya hivyo, itakuwa imefungua mlango wa mjadala ambao pengine moto wake ni mkali kuliko huu wa kusema "hii ni hatua ya kawaida".

Kiuhalisia Tanzania Kama Tanzania Hakuna ukabila, udini wala ukanda kama wengi huzani bali Tanzania kuna Makabila, Dini na Kanda kama ilivyo na inavyo fahamika


---+++---
Kasomi, wa Kasomi TV
 
Nikikaa hapa siti ya mbele ndo ntakuwa dereva eti ,Tanzania tutakuja gombana kwa kitu kingine kabisa ila sio dini wala ukabila
 
Kosa la kiufundi mleta mada umelifanya na inabidi usahihishe mapema ni kumuita Mohamed Said kuwa ni mwanahistoria maarufu..naomba niseme neno maarufu limetumika vibaya..huyo mzee ni mwendawazimu..mdini..mnafiki..mwenye chuki na mfumo kanisa..hana umaarufu wowote zaidi ya kupewa airtime humu JF.

Anafaa kukemewa na kupingwa na kila mtanzania mana lengo lake ni kuleta utengano na kupotosha.

Mwisho Tanzania haina dini ila wananchi wake wana dini na makabila..na teuzi ama ajira zinaangalia uwezo wala sio dini..rangi ama kabila la mtu.
Hii ndio misingi ya umoja na amani katika nchi yetu kama ilivyoasisiwa na baba wa. Taifa hayati mwalimu J.K Nyerere.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikikaa hapa siti ya mbele ndo ntakuwa dereva eti ,Tanzania tutakuja gombana kwa kitu kingine kabisa ila sio dini wala ukabila
Hakika Mimi binafsi nimekuachia usukani ngoja nikusanye abiria nje ili uwaendeshe vyema.

The rider
 
Kosa la kiufundi mleta mada umelifanya na inabidi usahihishe mapema ni kumuita Mohamed Said kuwa ni mwanahistoria maarufu..naomba niseme neno maarufu limetumika vibaya..huyo mzee ni mwendawazimu..mdini..mnafiki..mwenye chuki na mfumo kanisa..hana umaarufu wowote zaidi ya kupewa airtime humu JF...
Nimekuelewa vyema.
Lakini hoja Yangu ya kusema Mohamed Said kuwa ni mwana historia maarufu namaanisha kabisa.

Mkuu mzee Mohamed nimemjua nje ya JF kwa mfano mzee huyu ameandikwa na media nyingi kubwa za ndani na nje ya nchi na magazeti pia yamemuandika pamoja na mitandao.

Labda utete hoja yako ya kuwa mzee ni mdini swala ambalo Mimi pengine sikurifahamu awali au sikulifichua kwenye Mada hapo juu.

Ukiachana na udini wa mzee ila ni maarufu sana Baadhi ya interview nilizo wahi ona za mzee ni media kubwa za ndani mfano Azam na ITV na media za nje mfano BBC, DW na media nyingine.
 
Back
Top Bottom