Tanzania hakuna pesa ndiyo maana tunazunguka kukopa mpaka Barclays? Aibu nyingine hii kwa CCM na watu wake

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,259
2,000
Muda huu Serikali imewaomba Barclays Bank mkopo wa fedha ili imalizie Reli ya Standard Gaurge kuifikia nchi ya viwanda.

Leo Waziri wa Mipango Dr.Mpango ametembelea Makao Makuu ya Benki ya Barclays na kuiomba kuisaidia Serikali mkopo wa riba nafuu ili Serikali iweze kutekeleza miradi yake ya miundombinu ya Reli ya kati ya "Standard Gauge" na mradi wa umeme wa Stiglers Gorge.

Waziri Mpango ameiomba Benki hiyo kutenga kiasi cha fedha ili kuikopesha Serikali ili iweze kuijenga hiyo miradi yake ambayo inahitaji pesa nyingi ili Serikali iweze kufikia adhima yake ya nchi ya viwanda.

Swali: Inakuwaje tena Serikali inaanza kwenda kukopa kwenye mabenki binafsi na wakati tuliambiwa pesa inayojenga Reli ya Standard Gauge na ule mradi wa Stiglers Gorge ni pesa za ndani ambazo ni kodi zetu?

Je, kiuchumi kuna athari gani kukopa Benki binafsi kama Barclays? Zile taarifa kuwa miradi inajengwa kwa pesa za ndani huwa ni siasa tu?

Kwamba hakuna pesa ndiyo maana tunazunguka kukopa mpaka Barclays? Aibu nyingine hii kwa CCM na watu wake.

mkopo.jpg
 
BIGURUBE

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
6,726
2,000
Hizo pesa hawatalipa kamwe, kitakachotokea Hapo watafanya figisu ili bank ionekane mtaji umeshuka na kuiweka chini ya BOT control na kuitangaza kufilisika!

Serikali ya awamu hii ni kuwa nayo makini sana!
 
Sophist

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
4,423
2,000
Mleta uzi ni bora ungekaa kimya kwa kuwa umedhihirisha kuwa wewe ni mbumbumbu wa uchumi. Kutoa mikopo ndio shughuli kuu na mikopo ndio bidhaa kuu za mabenki na taasisi za fedha duniani kote. Aidha unatakiwa kufahamu kuwa ukisha kukopa hicho kiasi ulichokopa kinakuwa pesa yako, siyo pesa ya benki. Kwa hiyo serikali kusema tunajenga miundombinu kwa pesa zeu wenyewe ni kauli sahihi kabisa.
 
Naton Jr

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
7,498
2,000
Usikute unalinganisha Barclay's na efatha.?

Largest banks in the world
Rank Bank name & Total assets (US$ billion)

1 Industrial and
Commercial Bank of China 3,473.09

2 China Construction
Bank Corporation 3,016.45

3 Agricultural Bank of
China 2,815.92

4 Mitsubishi UFJ
Financial Group 2,626.29

5 Bank of China 2,611.43

6 JPMorgan Chase &
Co. 2,500.00

7 HSBC Holdings PLC 2,374.15

8 BNP Paribas 2,189.27

9 Bank of America 2,187.70

10 Wells Fargo & Co. 1,930.12

11 Crédit Agricole 1,816.97

12 Citigroup Inc. 1,790.68

13 Mizuho Financial
Group 1,752.19

14 Deutsche Bank 1,675.69

15 Sumitomo Mitsui
Financial Group 1,648.66

16 Barclays PLC 1,495.84
 
Hawa ndio wanataka tuwape nchi wakati hata sayansi ya uchumi ni zero alafu Eti anaiita Barclay's "serikali inakopa mpaka Barclay's" anafikiri Barclay's ni kama wallet yake ya mfukoni au kopa ng'ombe lipa ndama
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,679
2,000
Mleta uzi ni bora ungekaa kimya kwa kuwa umedhihirisha kuwa wewe ni mbumbumbu wa uchumi. Kutoa mikopo ndio shughuli kuu na mikopo ndio bidhaa kuu za mabenki na taasisi za fedha duniani kote. Aidha unatakiwa kufahamu kuwa ukisha kukopa hicho kiasi ulichokopa kinakuwa pesa yako, siyo pesa ya benki. Kwa hiyo serikali kusema tunajenga miundombinu kwa pesa zeu wenyewe ni kauli sahihi kabisa.

Angalia taifa lilipopitia hawa ndio ThinkTank wa NACCM.
 
Mafwi Munda

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
1,752
2,000
Hahaha tuliambiwa nchi hii tajiri sanaaa, na alituambia kwa utajiri tulio nao hatupaswi kukopa popote eti tulihitaji a good watchman asiyepepesa kope kulinda rasilimali zetu tu. Tuliambiwa sisi ndio tutatoa mikopo kwa mataifa ya nje, sasa sisi leo tunakopa tena?! Nini kimetokea kwenye utajiri wa Tanzania?! Nchi hii hata ukisikia kuna sherehe za miaka 100 ya chama jua tumesha kopeshwa maana sifa yetu sikuhizi eti bado TUNAKOPESHEKA.
 
Milanzi2018

JF-Expert Member
Dec 28, 2017
389
500
Muda huu Serikali imewaomba Barclays Bank mkopo wa fedha ili imalizie Reli ya Standard Gaurge kuifikia nchi ya viwanda.

Leo Waziri wa Mipango Dr.Mpango ametembelea Makao Makuu ya Benki ya Barclays na kuiomba kuisaidia Serikali mkopo wa riba nafuu ili Serikali iweze kutekeleza miradi yake ya miundombinu ya Reli ya kati ya "Standard Gauge" na mradi wa umeme wa Stiglers Gorge.

Waziri Mpango ameiomba Benki hiyo kutenga kiasi cha fedha ili kuikopesha Serikali ili iweze kuijenga hiyo miradi yake ambayo inahitaji pesa nyingi ili Serikali iweze kufikia adhima yake ya nchi ya viwanda.

Swali: Inakuwaje tena Serikali inaanza kwenda kukopa kwenye mabenki binafsi na wakati tuliambiwa pesa inayojenga Reli ya Standard Gauge na ule mradi wa Stiglers Gorge ni pesa za ndani ambazo ni kodi zetu?

Je, kiuchumi kuna athari gani kukopa Benki binafsi kama Barclays? Zile taarifa kuwa miradi inajengwa kwa pesa za ndani huwa ni siasa tu?

Kwamba hakuna pesa ndiyo maana tunazunguka kukopa mpaka Barclays? Aibu nyingine hii kwa CCM na watu wake.

View attachment 688636
Mkuu sema kwa sauti ya chini jirani atasikia
 
Kapustakasha

JF-Expert Member
Sep 9, 2016
248
500
Njia ya mwongo ni fupi!

Anayemlipa mpiga zumari ndiye mwenye haki ya kuchagua wimbo! Who pays the piper chooses the Music! Yaani hawa washamba wanateua kampuni ni Turkey kuwa Mkandarasi (main Contractor ) halafu unakwenda kuomba fedha ( financing loan) kutoka Barclays Bank. What we used to do you prepare a Bankable project document and call DFI ( Direct Financing Institutions) meeting sell the project project na hata kama kuna shortfall you iron out the basics tuliambiwa the Stiglers Gorge 2100MW project is in the world heritage and it requires dialogue for civility washamba wakakata! Do you remember lilie saga la Uranium tulipunguza ukubwa wa Selous National park but je Uranium imechimbwa and where is the CCM pomp ! Wakati mwingine don’t risk your neck to support hawa watu wa kijani ni matatizo matupu? Tuliambiwa Stiglers and SGR it’s after 3 years and I am betting my neck if it happens kichwa changu ni halali ya Serikali niko tayari kunyongwa pale National Studium saa tatu asubuhi if the projects are completed in those three years! Wacha Dr. Mpango nae akatembee kubadilisha matembele!
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
12,585
2,000
Usikute unalinganisha Barclay's na efatha.?

Largest banks in the world
Rank Bank name & Total assets (US$ billion)

1 Industrial and
Commercial Bank of China 3,473.09

2 China Construction
Bank Corporation 3,016.45

3 Agricultural Bank of
China 2,815.92

4 Mitsubishi UFJ
Financial Group 2,626.29

5 Bank of China 2,611.43

6 JPMorgan Chase &
Co. 2,500.00

7 HSBC Holdings PLC 2,374.15

8 BNP Paribas 2,189.27

9 Bank of America 2,187.70

10 Wells Fargo & Co. 1,930.12

11 Crédit Agricole 1,816.97

12 Citigroup Inc. 1,790.68

13 Mizuho Financial
Group 1,752.19

14 Deutsche Bank 1,675.69

15 Sumitomo Mitsui
Financial Group 1,648.66

16 Barclays PLC 1,495.84
Mkuu sidhani kama umeelewa mada, ni vzr uwe unasoma kabla ya kukurupuka!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom