BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,117
Sitta aagiza kupitiwa upya kwa sheria ya maadili
Maulid Ahmed
Daily News; Friday,May 09, 2008 @19:02
Spika wa Bunge, Samuel Sitta ameiagiza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, kuipitia upya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ili kubaini mapungufu yanayolalamikiwa na wananchi.
Akizungumza kwa niaba ya Spika, Katibu wa Spika Daniel Eliufoo alisema tayari ameshamuandikia barua Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje (CCM), ili Kamati yake iipitie sheria hiyo namba 13 ya mwaka 1995.
Katika maelekezo yake, Spika anataka sheria hiyo ishughulikiwe katika vikao vya Kamati za Bunge vinavyoanza Mei 26, mwaka huu. Baada ya Kamati hiyo kupitia sheria hiyo itawasilisha mapendekezo yake bungeni na hatimaye serikalini kwa hatua zaidi, alisema Eliufoo, akimkariri Spika ambaye kwa sasa yuko jimboni kwake Urambo.
Mbali na kuagiza kupitiwa upya Sheria ya Maadili, kuanzia sasa Spika atakuwa akizipelekea Kamati za Bunge masuala mbalimbali yanayolalamikiwa na wananchi. Msingi wa hatua hii ni kuziwezesha Kamati za Bunge kuwa proactive kwa kulisaidia Bunge kutafuta majawabu ya matatizo, migogoro na kero mbalimbali zinazowakabili wananchi na jamii kwa jumla.
Hatua hii italiwezesha na kuliweka Bunge katika nafasi nzuri zaidi ya kutekeleza kwa ufanisi majukumu yake ya kikatiba yaliyoainishwa kwenye ibara ya 63(2), alisema Eliufoo. Spika amefikia uamuzi huo kwa kutumia kanuni ya 116 ya Kanuni za Bunge inayosema Spika aweza kukabidhi jambo lolote kwa kamati yoyote kadri atakavyoona inafaa kwa ajili ya kushughulikiwa na Kamati hiyo.
Agizo la Spika limekuja baada ya viongozi wa vyama vinne vya siasa kuwasilisha barua kwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakitaka kuangalia mali za viongozi 11. Miongoni mwa viongozi hao ni aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Andrew Chenge ambaye amejiuzulu kupisha uchunguzi dhidi yake wa kujipatia rushwa kutokana na ununuzi wa rada.
Mbunge huyo wa Bariadi Magharibi (CCM), anadaiwa alijipatia zaidi ya Sh bilioni moja. Wengine ni Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, Mbunge wa Rombo Basil Mramba, aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Mbunge wa Bukoba Mjini, Nazir Karamagi ambaye alijiuzulu nafasi ya Waziri wa Nishati na Madini baada ya kuhusishwa na kashfa ya kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond, Katibu Mkuu Wizara ya Maji Patrick Rutabanzibwa.
Vyama hivyo pia vinataka kufahamu mali za Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), ambaye ni mwanasheria maarufu Nimrod Mkono, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Daud Ballali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995, inakataza mtu anayepewa ruhusa ya kukagua mali za viongozi zilizoorodheshwa kwenda kuchapisha au kutangaza kwenye vyombo vya habari au kuitoa taarifa hiyo bayana kwa umma, kutumiwa kwa madhumuni yasiyohusiana na malalamiko yaliyowasilishwa kwa kamishna au matumizi ya kashfa. Anayekutwa na kosa hilo adhabu yake ni kulipa faini ya Sh 10,000 au kwenda jela miaka isiyozidi miwili au adhabu zote kwa pamoja.