Tanzania hakuna Chama cha Upinzani bali wachumia tumbo

mtoto wa mchungaji

Senior Member
Oct 24, 2020
187
500
Wananchi wengi wa kawaida na hata viongozi wa kada ya chini ya vyama wanaamini kuwa wanaviongozi wa upinzani mbele yao kumbe wanawasindikiza wachumia tumbo sikuzote hapa Tanzania. Kwanini basi:

Tangia kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini mwaka 1992 makanjanja kibao walitokea CCM na kuja kuanzisha vyama najua wote tuna wafahamu, na watu waliwaamini kuwa wale viongozi watawapeleka katika mageuzi ya kweli kumbe lile lilikuwa kosa.

Chakwanza cha kufaamu chama cha siasa lazima kiwe taasisi yaani kusiwe na hisia za umiliki wa mtu au kakikundi cha watu. Yaani kama kweli upo katika chama cha siasa na inaingiza imani yako humo lazima kwanza chama kiwe na UTAASISIIZIM. Kinachotokea leo watu wanawaamini viongozi hasa wenyeviti wa vyama utazani mayesu yaani utadhani nao walizaliwa na bikira. Au watu wanaamini wenyeviti kama huku kwetu kanisani Askofu au mchungaji anaendelea kukusanya sadaka mpaka Mungu amchukuwe.

Leo hii kunachama kinaitwa A SI T utaona mambo ya ajabu sana mlendani tena katika katiba yao wenyewe wana kiongozi mkuu yaani huyu haguswi mwanangu. Katiba inasema yeye ndiyo kilakitu na kama kunauchaguzi mkuu yeye ndiyo mgombea pekee wa urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania labda akatae au ateue mtu mwingine kwa kukishauri chama. Sasa utaweza shangaa yaani hata watu hawajachukua nchi tayari wanajipa uongozi mkuu je wakichukuwa nchi si watakuwa zaidi mayesu.

Chama kingine ni KAFUU, tumewai kushuhudia mambo ya ajabu sana mle yaani mwenyekiti anajiuzulu kwa mujibu wa katiba mara tunasikia kajirudisha kwa mujibu wa katiba, uliwai kuona wapi, yaani inakuwa ngumu sana kuelewa inakuwa kama huku kwetu kanisani tunasema Yesu ni Mungu lakini alikufa na baadae akajifufua haya ni mambo magumu sana kuyaelewa.

Kunachama kingine kinaitwa SI D au M kipo hapa Tanzania hiki ndiyo chama cha ajubu kuwai kutokea duniani, licha ya kuwa hakina utaasisi hata kidogo lakini chenyewe kinaweza kubadirisha giabox angani hata kama wapo mita 7000 kutoka usawa wa bahari, hawaangalii hatari yoyote itakayo wakuta kama wakibadili giabox huko juu wenyewe wanamsikiliza mtu mmoja tu na si vikao naye anaitwa mtu asiye tawaliwa na mtu yoyote ajawai tawaliwa na hata tawaliwa ndiyo wanamsikiza.

Na huyu mtu Mungu amempa neema ya ajabu sana akisema wote tia plasta mdomoni wote plasta. Akisema wote tunasusa kama watoto au mwanamke wote wanasusa mpaka mtaani pia wanasusa. Cha ajabu lakini kila akitangaza maandamano nchi nzima tarehe ikikaribia anayafuta. Na kibaya zaidi kama hiki chama kikija kuchukua nchi wanaume watakuwa wanaolewa na harusi kubwa kuzidi hizi za kawaida --laana tulhalau. Na hiki chama kina mwenyekiti wa maisha kama aliyekuwa Kamuzu Banda wa Malawi yeye anamiaka takribani 30 sasa ofisini, yaani hata dhana ya kuja kwa mfumo wa vyama vingi hili kubadilishana vijiti haupo tena.

Chama kingine ni N MASIALA - MAGEUZI hiki kina mwenyekiti wa ajabu ajawai kutokea duniani na hata kabla ya misingi ya uumbaji, yeye anauwezo wa kujipendekeza kokote hata kama ataona chama kinakufa lazima akamilishe hilo zoezi. Anaasili ya kupenda kitonga zaidi ... huyu sichangii sana.

Chama kingine cha kushangaza ni TIA LO - P hiki nikisema sana mtasema nakufuru, yaani uliona wapi mnataka mchumba ambaye mnamgombania alafu wewe unasema mimi naungana na yule tunakuja kukuoa mchumba, yaani mke mmoja waume wawili. Pia unaharibu dhana zima ya wazungu kutugawa. Ndiyo maana hawakuruhuusu urafiki huo badarayake rafiki atoke nje ya nchi hili divaid and rulu iendelee.

Kunachama kinaitwa TAKIDEDEA hiki kinamwenyekiti yeye kama yeye anaomba ruzuku na misaada kutoka kwa mwenyekiti wa CCM eti chama chake kichanga hivyo asaidiwe kiwe na nguvu baadaye kije kukiondoa CCM.

Yaani atanikiorodhesha vyama vyote utaona mambo ya jabu sana kama tulivyoletewa dini kutoka Ukaya na Arabia kanakwamba sisi Mungu alikuwa atutambui.

Hapa wajanja ni viongozi wa vyama na wajinga ni wafuasi na wapambe wa vyama.

Kunamtu nimemkwaza. Mtoto wa Mchugaji.
 
El ohinu

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
254
500
Kama ambavyo hakuna CCM ila kuna kundi la majizi jizi tu na kuwatia umaskini Watanzania.
  • ndege alizoacha mwl zIko wapi?
  • viwanda alivyoacha mwl viko wapi?
  • mashirika aliyoacha mwl yako wapi?
Au ndo hao wapinzani walivigawana
 
WALOLA VUNZYA

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
663
1,000
Wachumia tumbo wako ccm tu hawana mbele wala nyuma,enzi za mwendazake walisema korona haipo,leo wanasema korona ipo,wao wanaishi na matakwa binafsi ya kiongozi aliyepo madarakani mradi tu wapate hela,leo kuna tozo kwenye mitandao na simu walishangilia sana eti kodi ya kizalendo,

kwa vile mama ameona na amechekwa,kuna watu au baadhi ya viongozi watakaa na kujadili ili kumridhisha mukulu wao napo watashangilia sana wakati aliyepitisha mswada kwa mbwembwe ni yeye,ukiwa huna akili huwezi kuliona hili,lakini kama una hata chembe ndogo ya akili kaa chini utafakari.
 
El ohinu

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
254
500
Wachumia tumbo wako ccm tu hawana mbele wala nyuma,enzi za mwendazake walisema korona haipo,leo wanasema korona ipo,wao wanaishi na matakwa binafsi ya kiongozi aliyepo madarakani mradi tu wapate hela,leo kuna tozo kwenye mitandao na simu walishangilia sana eti kodi ya kizalendo,kwa vile mama ameona na amechekwa,kuna watu au baadhi ya viongozi watakaa na kujadili ili kumridhisha mukulu wao napo watashangilia sana wakati aliyepitisha mswada kwa mbwembwe ni yeye,ukiwa huna akili huwezi kuliona hili,lakini kama una hata chembe ndogo ya akili kaa chini utafakari.
Usisahau enzi za jk aliposema fedha za escrow ni za bnafs yote yakaunga mkono huku yakiwakejeli wapinzani ambao ndo walikuwa wanasema ni za umma.

Alipokuja mwendazake akasema ni za umma maccm yote tena yakaunga tela huku yakiwaita wapnzani wasaliti
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,332
2,000
Wezi kwa kura bana....yaani unakurupuka kufanya jambo la ajabu na hovyo sasa ni aibu tupu.

Tatizo la kufikiri kila jambo ni jepesi kama kukimbia na mabox ya kura mchana mchana ndiko huku sasa.

Tozo hata wiki hazijamaliza kifo cha mende teh teh teh

CCM hamna kitu humo.
 
Deeboyfrexh

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
1,845
2,000
Kwa hali kuna haja kwa wananchi kuanzisha chama chao! Kianzie tu uraiani kama asasi ya kiraia ili kutetea maslahi ya raia. Hata graduates wakianzisha chama amabacho ki stem kwenye uzalendo tu na katiba inayoeleweka na sera zinazoeleweka pengine kutakuwa na mageuzi sahihi sio ya kutegemea vinyonga wa CHADEMA! Nahisi kizungumkuti kikubwa baina ya hivi vyama na CCM kutotaka kuachia dola ni kwamba kuna wasiwasi wa hali ya visasi na kukomeshana ambako kunaweza tekelezwa na CDM against CCM endapo wakishika dola!

Kuondosha root ya CCM kabisa kwa namna ambapo chama kitakuwa na wagombea vijana tu damu mbichi wapige siasa safi na katiba ikipatikana basi tuanzie kwenye level ya udiwani, ubunge mpaka uraisi! Mtu ambaye ana dhamira isiyoeleweka basi tuwe na katiba ya kumu expel on the spot. Tunataka hayo majukumu ya uongozi yafanyike kizalendo.

Hivi vyama vyote vilivyopo sasa havina tija kisiasa na kimaendeleo ya nchi! Vimebase kwenye Ilani ya kiinimacho ambayo wanadai ina guide mtawala ila kuna chembe chembe za kulindana kupitia Ilani hio hio na ndio inaturudisha nyuma kwa kupelekea kutotii sheria mama zilizoainishwa na katiba ya nchi yetu.

Ni wazo ghafi tu natoa room for improvements ili kuliweka in great shapes!
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,430
2,000
Nimekusoma vizuri nikategemea utaorodhesha vyama vyote vilivyopo kunbe wapi, kile unachokipenda chenye majanga yakutosha umekificha, hivyo huu uchambuzi wako umekosa maana, nautupia kapuni.
 
Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,372
2,000
Wananchi wengi wa kawaida na hata viongozi wa kada ya chini ya vyama wanaamini kuwa wanaviongozi wa upinzani mbele yao kumbe wanawasindikiza wachumia tumbo sikuzote hapa Tanzania. Kwanini basi:

Tangia kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini mwaka 1992 makanjanja kibao walitokea CCM na kuja kuanzisha vyama najua wote tuna wafahamu, na watu waliwaamini kuwa wale viongozi watawapeleka katika mageuzi ya kweli kumbe lile lilikuwa kosa.

Chakwanza cha kufaamu chama cha siasa lazima kiwe taasisi yaani kusiwe na hisia za umiliki wa mtu au kakikundi cha watu. Yaani kama kweli upo katika chama cha siasa na inaingiza imani yako humo lazima kwanza chama kiwe na UTAASISIIZIM. Kinachotokea leo watu wanawaamini viongozi hasa wenyeviti wa vyama utazani mayesu yaani utadhani nao walizaliwa na bikira. Au watu wanaamini wenyeviti kama huku kwetu kanisani Askofu au mchungaji anaendelea kukusanya sadaka mpaka Mungu amchukuwe.

Leo hii kunachama kinaitwa A SI T utaona mambo ya ajabu sana mlendani tena katika katiba yao wenyewe wana kiongozi mkuu yaani huyu haguswi mwanangu. Katiba inasema yeye ndiyo kilakitu na kama kunauchaguzi mkuu yeye ndiyo mgombea pekee wa urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania labda akatae au ateue mtu mwingine kwa kukishauri chama. Sasa utaweza shangaa yaani hata watu hawajachukua nchi tayari wanajipa uongozi mkuu je wakichukuwa nchi si watakuwa zaidi mayesu.

Chama kingine ni KAFUU, tumewai kushuhudia mambo ya ajabu sana mle yaani mwenyekiti anajiuzulu kwa mujibu wa katiba mara tunasikia kajirudisha kwa mujibu wa katiba, uliwai kuona wapi, yaani inakuwa ngumu sana kuelewa inakuwa kama huku kwetu kanisani tunasema Yesu ni Mungu lakini alikufa na baadae akajifufua haya ni mambo magumu sana kuyaelewa.

Kunachama kingine kinaitwa SI D au M kipo hapa Tanzania hiki ndiyo chama cha ajubu kuwai kutokea duniani, licha ya kuwa hakina utaasisi hata kidogo lakini chenyewe kinaweza kubadirisha giabox angani hata kama wapo mita 7000 kutoka usawa wa bahari, hawaangalii hatari yoyote itakayo wakuta kama wakibadili giabox huko juu wenyewe wanamsikiliza mtu mmoja tu na si vikao naye anaitwa mtu asiye tawaliwa na mtu yoyote ajawai tawaliwa na hata tawaliwa ndiyo wanamsikiza.

Na huyu mtu Mungu amempa neema ya ajabu sana akisema wote tia plasta mdomoni wote plasta. Akisema wote tunasusa kama watoto au mwanamke wote wanasusa mpaka mtaani pia wanasusa. Cha ajabu lakini kila akitangaza maandamano nchi nzima tarehe ikikaribia anayafuta. Na kibaya zaidi kama hiki chama kikija kuchukua nchi wanaume watakuwa wanaolewa na harusi kubwa kuzidi hizi za kawaida --laana tulhalau. Na hiki chama kina mwenyekiti wa maisha kama aliyekuwa Kamuzu Banda wa Malawi yeye anamiaka takribani 30 sasa ofisini, yaani hata dhana ya kuja kwa mfumo wa vyama vingi hili kubadilishana vijiti haupo tena.

Chama kingine ni N MASIALA - MAGEUZI hiki kina mwenyekiti wa ajabu ajawai kutokea duniani na hata kabla ya misingi ya uumbaji, yeye anauwezo wa kujipendekeza kokote hata kama ataona chama kinakufa lazima akamilishe hilo zoezi. Anaasili ya kupenda kitonga zaidi ... huyu sichangii sana.

Chama kingine cha kushangaza ni TIA LO - P hiki nikisema sana mtasema nakufuru, yaani uliona wapi mnataka mchumba ambaye mnamgombania alafu wewe unasema mimi naungana na yule tunakuja kukuoa mchumba, yaani mke mmoja waume wawili. Pia unaharibu dhana zima ya wazungu kutugawa. Ndiyo maana hawakuruhuusu urafiki huo badarayake rafiki atoke nje ya nchi hili divaid and rulu iendelee.

Kunachama kinaitwa TAKIDEDEA hiki kinamwenyekiti yeye kama yeye anaomba ruzuku na misaada kutoka kwa mwenyekiti wa CCM eti chama chake kichanga hivyo asaidiwe kiwe na nguvu baadaye kije kukiondoa CCM.

Yaani atanikiorodhesha vyama vyote utaona mambo ya jabu sana kama tulivyoletewa dini kutoka Ukaya na Arabia kanakwamba sisi Mungu alikuwa atutambui.

Hapa wajanja ni viongozi wa vyama na wajinga ni wafuasi na wapambe wa vyama.

Kunamtu nimemkwaza. Mtoto wa Mchugaji.
Pole sana Kutolewa Ubongo
20210716_160047.jpg
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom