Tanzania haiwezi kukua kiuchumi bila MAFIA wa kiuchumi, WEZI, MAFISADI, na WELEDI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania haiwezi kukua kiuchumi bila MAFIA wa kiuchumi, WEZI, MAFISADI, na WELEDI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yericko Nyerere, Sep 21, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,850
  Trophy Points: 280
  Kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa kulileta mageuzi makubwa katika uchumi wa Tanzania. Tanzania inajivunia kuwa ni moja kati ya nchi za mfano wa maendeleo barani Afrika tangu ikumbatie sera za soko na uchumi huria kutokana na kupigwa mwereka kwa Azimio la Arusha la 1967 na Azimio la Zanzibar la 1992.

  Takwimu zinaonyesha kuwa uchumi wa Tanzania umeendelea kukua kwa kasi nzuri kwa kipindi kifupi. Kwa mfano mwaka 1996 uchumi ulikuwa kwa asilimia 4.2, mwaka 1999 asilimia 4.7, mwaka 2001 asilimia 5.7, mwaka 2002 asilimia 6.2 nakufuatia hali mbaya yahewa mwaka 2003 kasi ya ukuaji wa uchumi ilipungua na kukua kwa asilimia 5.6, mwaka 2004 ulipanda tena asilimia 6.3. Kwaupande mwingine mfumuko wa bei umeshuka kwa kasi sana. Ulishuka kutoka zaidi yaasilimia 16 desemba 1997 na kufika asilimia 6.0 Novemba 2000 na kushuka zaidi hadi kwenye asilimia 4.5 kwa wastani hadi 2005. Hii tena ni dalili njema kabisa kwakuwa hakuna atakayependa kuwekeza katika uchumi ambao mfumuko wa bei unakimbilia asilimia 100.

  Lakini dalili hii nzuri yakukua kwa uchumi inakwenda sambamba na kukua kwa tabaka la matajiri na masikini. Ongezeko hilo limekuwa kwa kupindukia, Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 20% ya matajiri mwaka2001 ilitumia kiasi cha 44% ya matumizi yote ya kaya, ikilinganishwa na 43% ya mwaka 1991.

  Kukua kwa uchumi kunakoambatana na ongezeko la pengo la walionacho na wasio nacho kunaonyeshwa na kipimo kiitwacho GINI ambacho kwa Tanzania kilionyesha kuongezeka toka 0.34 mwaka 2001 hadi 0.345 mwaka 2005. Kadiri tarakimu hii inavyokua ndivyo pengo linavyozidi kukua. Mfano: jamii ambayo mgawanyo wa pato unauwiano mzuri sana tarakimu hii hupungua nakuwa ndogo, na kwa jamii au nchi yenye mgawanyo mbovu tarakimu huwa kubwa sana. Matharani, tarakimu hii ikiwa 0 nikwamba wote mnagawana pato sawa, naikiwa 1 inawezekana mtu mmoja anakuwa na pato kubwa. Ninadra! Haijapata kutokea na haitotoke tarakimu hii iwe 0 au 1 kutokana na mageuzi ya kiuchumi huku ufisadi ukishika kasi katika dola nyingi duniani hususani Tz. Mfano, nchi za China na Norway ambapo kuna uwiano mzuri wa mgawanyo wa pato bado hawawezi kuwa na 0 au 1.

  Takwimu zinazotumika kujua pato la nchi kwa Tanzania, zinakinzana na ukweli wa pato la kaya. Mfumo unaotumika kujua wastani wa pato la kila mmoja hupatikana baada ya kujumlisha pato la nchi na kuligawa kwa idadi ya watu wa nchi hiyo.Inamaana kwamba kila mwananchi anahesabika kuwa ni mmiliki wa.kilichozalishwa katika uchumi kwa mwaka huo. Dalili hii ya kukua kwa uchumi na pengo la masikini na matajiri kuongezeka, linaendelea kuumiza vichwa vya wanauchumi wengi duniani kwani tatizo hili si kwa Tanzania tu bali nchi zote zinazo endelea kukua.

  Nukuu za wanauchumi maarufu dunia zinazoonyesha kutimilika: John Maynard Keynes wa Uingereza ananena yakuwa, “Yamukini pengo la masikini na matajiri likawa dhahiri kadiri nchi zinavyo endelea kukua”. Brentano Lujo aliyezaliwa Aschaffenburg, Bavaria (Ujerumani ya sasa) “Inafurahisha na kusikitisha kwani kuna uwezekano wa kuongezeka maradufukwa umasikini kwa nchi zinazo endelea:. Simon Kuzinets mwanauchumi wa Marekani aliyezaliwa Kharkiv nchini Ukraine: “Mgawanyo wa pato hautakuwa sawia na huenda usawa ukaongezeka kupungua baadae kadiri pato lanchi linavyo zidi kukua”. Joseph A. Schumpeter mchumi wa Kimarekani aliyezaliwa Triesch, Moravia (Jamuhuri ya Czech kwa sasa) “Katikati ya mwanga mwanana wa machipuko ya kiuchumi panaibuka zuio la tathimini, tatizo hili litastawi katika mataifa yanayoendelea”.

  Kwa Tanzania kinacholeta kanganyiko huu wa kutopungua umasikini wakati ambapo uchumi unakua ni kwamba ukuaji wa uchumi haujagusa sekta kiongozi ya kilimo. Sekta hii inayoimbwa kila siku kuwa ndio uti wa mgongo wa taifa letu. Licha ya sekta ya kilimo kuchangia kiasi cha asilimia 45 ya pato la taifa, asilimia 85 ya mauzo ya nje na kuajili asilimia 80 ya watanzania wote, ukuaji wa sekta hii umezorota kwa kipindi cha miaka ya karibuni. Mfano sekta hii ilikua kwa asilimia 5.5 mwaka 2001, mwaka 2002 asilimia 5.0, mwaka 2003 asilimia 4.0, mwaka 2004 asilimia 3.8, mwaka 2005 asilimia 3.7 na mwaka 2006 asilimia 3.5.

  Hii inaonyesha kwamba vipato vya asilimia 80 ya waajiliwa wa sekta hii vimekuwa duni kwa miaka hiyo, hivyo kutia shaka kama umasikini unaweza kupungua miongoni mwa watu hao. Sekta iliyokua kwa kasi ni ya madini ambayo inaonyesha kwamba imekua toka asilimia 13.5 mwaka 2001 hadi asilimia 15.0 mwaka 2002 na asilimia 17.0 mwaka 2003. Sekta hii ni mpya na imekuwa ikipata wawekezaji wengi kwa haraka sana. Tatizo kubwa la sekta kama ya madini hasa katika nchi za Afrika ambazo husafirisha madini ghafi ni kwamba haizalishi ajira zinazoweza kupunguza umasikini kwa kasi sambamba na ukuaji wa uchumi.

  Hii inatokana na ukweli kwamba madini ghafi husafirishwa nje ya nchi na kukatwa katika maumbo mbalimbali tayari kwa uuzaji. Hivyo sekta hii haina uhusiano wa karibu na sekta ya viwanda katika nchi zinazo zalisha na kusafirisha madini ghafi. Pili ajira inayozalishwa ni ndogo kutokana na matumizi ya mashine katika uzalishaji wa madini hayo. Hali ya ardhi yetu si mbaya na njia pekee itakayo harakisha kupungua kwa umasikini wetu pamoja na kuongeza thamani ya madini ni kuwekeza katika kilimo. Fedha zinazopatika katika madini ziwekezwe katika kilimo ilikuwasaidia asilimia 80 ya watanzani walioajiliwa katika sekta hii. Hii ni changamoto kubwa kwa Tanzania kufikia malengo ya milenia ya kupunguza idadi ya watu wanaoishi katika umuasikini wa kupindukia ifikapo mwaka 2015.

  Ili malengo ya timie inatakiwa uchumi ukue kwa wastani wa asilimia 3.8 hadi 4.5 kwa mwaka, mpaka ifikapo 2015 Nimuhimu kutilia mkazo elimu itakayo wawezesha watu kujiajiri wenyewe,kwani hii ni njia rahisi ambayo inaweza kumkwamua mtu katika umasikini. Bilashaka nchi nyingi za Asia ya Mashariki ambazo tunapenda kuiga namna zilivyoweza kukua kiuchumi kwa kasi ya ajabu ni kwamba ziliweza kuua ndege wengi kwa jiwe moja, ukuaji wa pato la kila mwananchi kwa wastani ulikua kwa kasi ya kutisha, wastani wa umri wa kuishi uliongezeka, kuongeza kasi ya elimu na upunguzaji wa umasikini kwa kasi.

  Waliweza kufanya hayo bila kufuata TORATI walizopewa na mabwana wa IMF na Benki ya Dunia. Walitilia mkazo elimu ya ufundi, utafiti na uwekezaji katika teknolojia sahihi. Ukuaji wa uchumi ambao hauwezi kubadili maisha ya watu masikini hautakuwa na mafaa yoyote. Utakuwa ni ukuaji wa uchumi kitakwimu zaidi kuliko kuleta maisha bora ya watu. Hayo ndiyo tumekuwa tukishuhudia zaidi katika nchi nyingi za kiafrika na Latini Amerika ambapo takwimu huonyesha kuwa uchumi unapanda kwa kasi nzuri, lakini ukweli ni kwamba ukiingia kwenye nyumba ya mtu wa kawaida kunawaka moto. Ukuaji wanamna hiyo wa uchumi hunufaisha kundi dogo la jamii na kujikita katika ukuaji wa vitu vichache ambavyo huwa nafaida ndogo kwa jamii kubwa.

  Mf: sekta ya madini ikikua kwa faida kubwa ya mwekezaji, haitakuwa na maana kama watanzania hawafaidi matunda yake. Badala yake tunapewa viini macho vya wawekezaji kwa kujengewa shule na zahanati ambazo maranyingi huwa na lengo la kuwaduwaza wanavijiji na wanaotembelea migodi hiyo. Kinachotakiwa ni maendelo ya kweli yatakayoletwa na ukuaji wa sekta hii kwa maana ya kodi za kutosha na gawio linaloonekana. Tusizugwe na wanayoipa jina la misaada ya milioni 200 kwa kupoteza mabilioni ya fedha zetu za madini na ajira ambazo kwakukata madini hapa nchini tungezipata. Kwaujumla ukuaji wa uchumi haujapunguza makali ya maisha ya watanzania walio wengi

  Katika moja ya masimulizi ya kale yenye kuelezea mageuzi ya china toka kwenye lindi la ujamaa mufu mpaka ujamaa wa kimapinduzi ya kiuchumi, Masimulizi yaliyo kwenye makumbusho ya Szechuan yanasomeka kuwa ni matajiri 8 tu ndio walioibadili China mpaka kuja ilipo sasa.

  Najiuliza swali lakini linakosa majibu, je ni taifa gani lililoendelea bila mabilionea? bila mafisadi? bila mamafia wa ukwasi? bila WEZI?

  Mimi naamini tatizo ni mfumo wa hawa wakwasi ndio unaoliyumbisha taifa, ni vigumu kuwaondoa lakini tunaweza kupunguza spidi yao na kuwaambia wabadili mfumo wao wa ukwasi.

  Mfano nchi ya Marekani mabebari hawa wanapiga sana hela nje ya nchi na wanalipa kodi kwa wingi ndani ya nchi yao. vivyo hivyo ufaransa, Urusi, Uchina, Uingereza na Japan

  Lakini Tanzania ni matajiri wangapi biashara zao ni halali na wanalipa kodi stahiki??????

  Tangu nchi yetu ifuzu kujiunga na kikundi cha nchi tegemezi zinazotembeza bakuli kila kukicha mwaka 1997 baada ya kuifurahisha Benki ya Dunia (WB) na Shirika la fedha la Kimataifa (IMF) juu yauzingatiaji wa TORATI ya mashirika hayo mumiani, zaidi ya watanzania 50% ni masikini wa kutupwa wanaoishi chini ya mstari wa umasikini (Poverty line) kwa matumizi chini ya Tsh 260 kwa siku, asilimia36% ni masikini sana, Wakati watanzania asilimia 14% ni matajiri wa kupindukia wanaoishi maisha ya anasa, wakimiliki mahekalu, magari ya kifahari na ya gharama kubwa na watoto wao kusoma shule za sifa ya kimataifa. Hawa ndio wanaodhibiti uchumi na siasa ya nchi hii kwa gharama ya watanzania asilimia 86 walio nje ya kundi hili.
   
 2. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yericko Nyerere

  Asante na Hongera kwa uchambuzi mzuri, ila nasita kukuunga mkono kuwa bila wezi hatuwezi kuendelea, inamaana unapigia debe mafisadi tusiwapeleke mahakamani?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hujasema hizo njia unazoshauri watumie ni zipi?
   
 4. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,850
  Trophy Points: 280
  Ukiisoma makala yote kwa umakini utaona mapendekezo yangu mkuu
   
 5. F

  Fursa Pesa JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 2,324
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Sacrifice should be made starting from familiy to nation so as to restore what called lost identification of the nation without any harm.
   
 6. m

  mharakati JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  taifa kuendelea kiujumla tunahitaji investors na more industrialists kama akina SSB na siyo mission town kama akina RA
   
 7. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Nikiangalia data za hiyo article, zote zimeishia 2005! For that case, ni irrelevant kwa sasa ambapo miaka 7 zaidi imeshapita. Mwandishi kwa wakati huo alikuwa sahihi. But kwa sasa sidhani!!!
   
 8. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,850
  Trophy Points: 280
  Wianisha na uchumi wa sasa, ukisoma utaona nimeeleza malengo ya milenia ifikapo 2015 angalau uchumi uwe unakua kwa wastani gani
   
 9. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #9
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,850
  Trophy Points: 280
  Hehee ni sawa unataka unataka kufaulu bila kusoma kwa bidii, hao mission town ndio wanaoleta investors. Bila hao ni bila mwekezaji
   
 10. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #10
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,850
  Trophy Points: 280
  Kuna kipande hiki sijui umekielewa mkuu?

  "Ili malengo ya timie inatakiwa uchumi ukue kwa wastani wa asilimia 3.8 hadi 4.5 kwa mwaka, mpaka ifikapo 2015 Nimuhimu kutilia mkazo elimu itakayo wawezesha watu kujiajiri wenyewe,kwani hii ni njia rahisi ambayo inaweza kumkwamua mtu katika umasikini. Bilashaka nchi nyingi za Asia ya Mashariki ambazo tunapenda kuiga namna zilivyoweza kukua kiuchumi kwa kasi ya ajabu ni kwamba ziliweza kuua ndege wengi kwa jiwe moja, ukuaji wa pato la kila mwananchi kwa wastani ulikua kwa kasi ya kutisha, wastani wa umri wa kuishi uliongezeka, kuongeza kasi ya elimu na upunguzaji wa umasikini kwa kasi."
   
 11. m

  mharakati JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  investors gani wamenufaisha taifa kiuchumi kama siyo sectoral growth ambayo haina impact kwenye overall growth ya uchumi wetu.
   
 12. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #12
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,850
  Trophy Points: 280
  Ni kweli, ila unaamini Taifa lolote linaweza kuwaondoa watu wa aina hiyo ktk nyanja ya kiumi na likakua vema?
   
Loading...