Tanzania haiwezi kuendelea hata baada ya miaka 50 kwa sababu..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania haiwezi kuendelea hata baada ya miaka 50 kwa sababu.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Huduma, Oct 8, 2008.

 1. H

  Huduma Member

  #1
  Oct 8, 2008
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TANZANIA ni nchi iliyojaliwa ardhi ambayo si mbaya kwa kilimo; ina madini tele yanayouzwa kwa bei sawa na bure kwa wageni; kuna mali asili tele; ina fukwe za bahari, maziwa na mito; ina milima kama Kilimanjaro na Meru; ina wanyama wasiopo kwingineko duniani; inaweza ikiwa kivutio kikubwa cha watalii miji, mitaa na mahoteli yakiwa na mandhari nzuri na usafi wa hali ya juu; inaweza ikawa na Dubai kadhaa za Afrika; inaweza ikawa na meli za kisasa za uvuvi; inaweza ikawa na mijidege ya kubeba mizigo toka China na Uarabuni kuja kuuzwa kwa Wakongomani, Burundi, Wazambia, Wazimbabwe, Wamalawi na Warundi na Wa nyaranda na kuwaondoa mamilioni ya Watanzania toka kwenye umasikini wa kutisha. Lakini umekwishajiuliza kwanini hakuna linaloendelea na badala yake wananchi wanaibiwa mchana kweupe na viongozi wao. Zipo sababu. Na baadhi yake ni hizi hapa:

  i. Dhuluma serikali za awamu mbalimbali iilizowafanyia wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
  ii. Dhuluma waliyofanyiwa wajane wa maaskari waliokufa katika vita vya Kagera,
  iii. Dhuluma wanayofanyiwa wapinzani na wale wasiokuwa wanachama wa chama tawala na viongozi na wanachama wa chama tawala,
  iv. Dhuluma waliyofanyiwa na wanayoendelea kufanyiwa Waislamu ikiwemo kunyimwa Ofisi ya Kadhi, na upendeleo kwa wakiristo na hasa Wakatoliki,
  v. Dhuluma ya ubia kati ya viongozi wa seirikali na wachimba madini kama vile almasi, dhahabu, tanzanite, vito na sasa uranium na platinum na mafuta ya peteroli wanayowafanyia Watanzania,
  vi. Dhuluma inayofanywa na NSSF, PPF, LAPF na mifuko mbalimbali ikiwemo ile ya afya kwa Watanzania wafanyakazi,
  vii. Dhuluma waliyofanyiwa na inayoendelea kufanyiwa wakulima na bodi au mamlaka za hiki au kile,
  viii. Dhuluma wanayofanyiwa Watanzania na viongozi wao kutokana na mishahara na masurufu ya kufuru ikiwemo yale ya safari ambazo tayari zimekwishalipiwa na wahisani au nchi za nje,
  ix. Dhuluma waliyofanyiwa Watanzania kwa kuuzwa mashirika ya umma na hata mmoja wao asillipwe hata senti tano,
  x. Dhuluma inayofanywa na viongozi wa serikali kutumia matrilioni kwa magari, mafuta na meintenansi ya magari ya kifahari,
  xi. Dhuluma wanayofanyiwa watoto kwa fedha yao inayotolewa na nchi za nje na Umoja wa Mataifa na hususan UNESCO kuliwa na wake na watoto wa wakubwa,
  xii. Dhuluma wanayofanyiwa Watanzania na viongozi wao kwa kuuza miti na mali asili nyingine nje kwa bei sawa na bure,
  xiiii. Dhuluma inayofanywa na benki na vyombo vingine vya fedha dhidi ya wanyonge na wajasiriamali wa Tanzania,
  xiv. Dhuluma inayofanywa na Mamlaka za kodi dhidi ya watu wanaohangaika usiku na mchana kukidhi mahitaji yao ya msingi,
  xv. Dhuluma inayofanywa na jumuiya au vyama vya hiki au kile dhidi ya wanachama wao ikiwemo wazee, wanawake, walimu, vijana na kadhalika,
  xvi. Dhuluma wanayofanyiwa madaktari, manesi, walimu na wafanyakazi wengine,
  xvii. Dhuluma wanayofanyiwa wanafunzi, machinga na vijana kwa ujumla,
  xviii. Dhuluma wanayofanyiwa wapigania demokrasia na haki za binadamu,
  xix. Dhuluma wanazofanyiwa wazee, walemavu, maalbino, masikini na wagonjwa,
  xx. Dhuluma wanayofanyiwa wapiga kura wa nchi hii na chama tawala na mawakala wake,
  xx. Dhuluma wanayofanyiwa Watanzania na baadhi ya mawaziri na wabunge ambao wanalipwa unono lakini wanachokifanya hakionekani,
  xxi. Dhuluma, uonevu na unyanyaswaji wanayofanyiwa watembea kwa miguu na wale wenye magari wakiwemo wanasiasa na watumishi wa umma,
  xxii. Dhuluma wanyofanyiwa baadhi ya watu na askari polisi vituoni na mabarabarani,
  xxiii. Dhuluma wanayofanyiwa wananchi na wageni wanaowekeza au kuishi hapa nchini,
  xiv. Dhuluma wanayofanyiwa wananchi na mahakama, bunge na vyombo vingine vinavyotegemewa kutetea haki zao,
  xxv. Dhuluma inayofanyiwa vizazi vijavyo na chama tawala na viongozi walioko madarakani.

  KWA MTAJI huu itakuwa ni vigumu sana kwa Watanzania kupata cha kutegemea achilia mbali neema au baraka inayoonekana na kuhesabika.
  Na Watanzania wasimtegemee Muumba kuwa ndiye atakayebadili hali zao. Maana Muumba keshasema 'hatowasaidia watu hali zao kubadilika, hadi pale watakapomtambua na kujitambua wenyewe na kisha kuanza harakati za kubadilika wao wenyewe. '  TANZANIA KWA DHULUMA NDIYO YENYWE, NA MWENYEZI MUNGU KATU HAWAPENDI MADHALIMU. NI MSIBA MKUBWA ULIYOJE MAFISADI NA MADHALIMU KUIFANYA NCHI YETU ICHUKIWE NA MUUMBA NA MALAIKA WAKE!
  huduma,
  zanzibar
   
 2. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #2
  Oct 9, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kitaeleweka tu,dawa yao ni Mapinduzi makubwa yanayosubiri muda
   
 3. I

  Iga Senior Member

  #3
  Oct 9, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KATIKA kuparaphrase kauli ya mtoa mada hii ninadhani anachokisema ni kuwa chama tawala na serikali yake inahitaji kupitia msururu huu wote wa dhuluma kama msahafu na kuona mapungufu na udhaifu wake na kwamba kisipojirekebisha na wapinzani wakaacha wehu wao na ulafi wao basi wajue 2010 mambo hayatakuwa mtelemko kama vile 2006!


  Katika kuongezea naona kama vile Umesahau:
  . Dhuluma za TANESCO kwa watumiaji umeme Tanzania na choyo yao kwa kuwa wanakula kila wanachozalisha na wasichozalisha. Ninasikia bei ya kufunga LUKU sasa kuwa milioni 1.5 hivi karibuni,
  . Dhuluma ya mijikampuni ya ugawaji maji ambayo sijui hata namna walivyopewa tenda na uwezo hawana,
  . Dhuluma za wazoaji taka ambao wako hoi na magari na vifaa wanavyotumia navyo vikiwa pia ni UCHAFU, eti uchafu unaweza kuondoa uchafu jamani,

  Yapo madhambi mengi tu. Na hakika baraka na neema za Muumba zimegura toka nchi hii na mtu asitudanganye vinginevyo. Wanaosema vingine ndio hao wanaopewa chochote na walioko madarakani. Hawa ndio wale ambao wako tayari hata kupigwa mawe na umma kutokana na uzushi na uongo wao ili kuendelea kumwambia Mfalme aliye uchi wa mnyama kwamba kavaa JOHO la ajabu .....
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Oct 9, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Maneno meeeeeeeengi.......
   
 5. w

  wajinga Senior Member

  #5
  Oct 9, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  from the way it looks like God left this place long time ago. So please fight for your rights with whatever means necessary.
   
 6. w

  wajinga Senior Member

  #6
  Oct 9, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  from the way it looks like god left this place long time ago.Please fight for your rights with whatever means necessary
   
 7. w

  wajinga Senior Member

  #7
  Oct 9, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  from the way it looks like God left this place a long time ago. PS fight for your rights with whatever means necessary. Godless Tanzania.
   
 8. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2008
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mapinduzi ya kifikra labda ila our leaders' schadenfreude is far from ending.
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Una maana vitendo vichache?BTW welcome back.
   
 10. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Watanzania wataendelea.
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha..Tembelea ile thread ya makampuni yanayolipa kodi zaidi Tanzania.Mimi sioni tutaendelea vipi huku serikali haiwezi kufanya majukumu yake ya awali kabisa,kukusanya kodi tu.
   
 12. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tunaowategemea watuonyeshe njia ya ukombozi wana-demand 7.2 M kwa mwezi!
   
 13. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  In short ni kwamba serikali iliyopo na chama chake wameshindwa kumanage nchi ndio maana inaporomoka na haiwezi kubadilika kwa mwendo uliopo. Massive change is needed.
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Aug 27, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  What's happenin' Meku? Vipi wewe uko mbali na path ya Irene?
   
 15. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
  nimeiona. Nashangaa sioni kampuni za simu wakati %80 ya watz wanatumia simu ukilinganisha na wanaotumia huduma za kibenki
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Naona sababu yako kubwa ni dhuluma.

  Marekani na Ulaya wamefanya dhuluma sana, kuanzia utumwa, ukoloni mpaka leo wanaendeleza ukolni mamboleo.

  Mbona wao wameendelea?

  Kama Watanzania hawataendelea, kuna sababu nyingi sana na kusema "dhuluma hii na ile" tu hakulifanyii haki hili swala.
   
 17. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #17
  Aug 27, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hapo ndipo tatizo lilipo. Wanaobwabwaja juu ya ukombozi hawako serious about ukombozi bali ni waliojawa na tamaa ya kufyonza kama wale waliopo.
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha!I am bracing for it.Or should i say her?She is really a biyach.Down to category 1,thanks God.
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Nadhani mleta hoja alimaanisha kwamba pamoja na dhuluma zote walizofanyiwa watanzania,bado wameshindwa kufanya mabadiliko ya uongozi.Na ndiyo maana akasema hata itake 50 years bado hawataweza.
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Aug 28, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  1. Miafrika Ndivyo Tuilivyo -
  a). Wazimaa wa Afya lakini tunatembea na Bakuli kama maskini wa Jamatini..
  b). Ombaomba sii rahisi kuwa na vision zaidi ya tumbo lake hivyo maneno mengi kuliko utendaji.
  c). Malimbukeni, hivyo husababisha kujenga nchi kutoka juu kuja chini.
  d). Last but not beast - Wanafiki!
   
Loading...