Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,192
- 3,351
Katika pita pita zangu mtandaoni nimeona jinsi nchi nyingi zilivyodai haki za kisiasa kwa kubishana na maamuzi ya kinyanyasaji yanayofanywa na serrikali zao kitu kinacholeta vurugu na umwagaji damu ndani ya nchi, ila mwishowe muungano wa wananchi katika kufanya sauti yao isikike huleta tunda katika taifa na huifanya nchi iwe imara maradufu.
Sasa nikija hapa kwetu Tanzania naona wazi kabisa jinsi wananchi wa hii nchi walivyo tofauti na nchi za wenzetu katika kudai haki, kila lifanywalo na serikali ndilo litakalokuwa, wananchi wanabaki kulalamika chini kwa chini kwa siku mbili tatu na ndio mwisho wa mjadala, Chukua mfano wa hili sakata la escrow kiukweli kila mwananchi mwenye uchungu wa maendeleo ya nchi hii aliumizwa, ishu ikawa juu kila kona ni escrow but the end result mawaziri wengi hawakujiuzulu, kiufupi hakuna uwajibikaji, ila wananchi wengi hawakufuraishwa na hiki kitendo kwani wananchi walitaka adhabu kali zitolewe kwa hawa watu, kiukweli niliona wananchi wengi walioumia lakini hakuna kitu kilichofanyika.
Wananchi wa hii serikali ni yetu, inatengenezwa na sisi na kwa manufaa ya kila mtanzania, Pale tunapoona serikali haiendi kunako stahili haina budi kuikalia serikali hadi kieleweke katika kutimiza wajibu wake, msione watu kwenye nchi nyingine wanagoma hadi kumwaga damu mkafikiri wanapenda, ni kwa ajili tu ya kuifanya serikali itanbue serikali haipo kwa manufaa ya wanasisa bali ni kwa ajili ya wananchi wote,