Tanzania haitokaa iendelee milele hata mfanyeje

Wewe mkuu utakuwa ulikuwa unakwenda shule kwa kutumia ule usafiri wa Mabasi ya njano.Ungekuwa umekung'uta umande wakati wa kwenda shule usingeandika kuwa hatutaendelea.Kwa ukweli kabisa nchi inaendelea sema tu kasi ndiyo ndogo.
 
Wa kusifu na kuabudu vp tena!??

Mpaka Mama anaondoka litakuwa 120 Tr.
We pambana kivyako.
 
Kwani wee maendeleo unayapimaje?

Wenzio tunapima kwa Barabara, maji, umeme. Majumba, magari.

Hivi ma mwendokasi, barabara za juu bado unasema hatujaendelea?
Mbona kabla ya hayo mabarabara majumba watanzania maisha yao yalikuwa nafuu na bora? Hakuna maendeleo yoyote kila siku heri ya jana. Maendeleo yako kwa wachache tuu hao viongoz wa CCM kwa kufisidi nchi bila huruma
 
Siwakatishi tamaa ila huo ndo ukweli

Nchi yetu haina dalili ya kuendelea kabisa

Deni la taifa ni trilioni 80

Na asilimia kubwa ya bajeti yetu huishia kulipa madeni, watumishi nk...Fedha za maendeleo ni kidogo mno sasa hapo mtaendelea vipi?

Mfano halisi ni wizara ya fedha, waliwekewa bajeti ya trilioni 12....Ambapo trilioni 10 zinaenda kulipa madeni...Sasa hapo mtaendeleaje?

Pesa zimekua zikiishia kwa wachache majority wanabaki na hawaguswi na miradi ya umma

Tutaendelea vipi wakati hata dalili ya kuacha kutegemea misaada haipo?

Tutaendelea vipi deni linazidi kukua na fedha zote asilimia 90 huishia kulipa madeni na watumishi wa umma?

Tutaendelea vipi huku tunazidi kukopa imf na wb na tunawapa migodi,mafuta na gesi vinaenda ulaya?

Tutaendelea vipi na sera za hovyo hovyo tu nchi haijulikani inapoenda?

Tutaendelea vipi kila rais akija anakuja na yake?na mambo yake akiingia mwingine naye anabomoa yale ya mwenzie anaanza na yake na mwingine akija ni hivyo hivyo?Ni sawa na nyumba unaanza na msingi,kisha fundi anamaliza mkataba,anakuja mwingine anabomoa msingi anaanza wake wa style na nyingine anamaliza anakuja mwingine anavunja anasema sio hivyo anajenga kivyake... Haya yanafanyika kila baada ya miaka 5 nchi hii

Tutaendelea vipi wakati kuna chain ya pesa kuliwa from top area(mawaziri,marais) hadi bottom area (serikali za mitaa na wananchi) Yaani hela inaanza kudonolewa kuanzia juu huko hadi ije kumgusa mwananchi wa chini ishaliwa

Pesa yenyewe ya miradi na maendeleo inayotengwa ni kidogo na bado inadonolewa na kupunguzwa kwa kuliwa hadi ije mfikia mtu wa chini ishapungua au kwisha kbs

Kwa haya tutaendeleaje?SIDHANI KAMA HII NCHI ITOKAA IENDELEE KAMWE!!!!!!!
Kuacha ufisadi na kujituma ndiyo silaha ya maendeleo.
 
Kabla ya ukoloni Tanzanian ilikuwa hivi ilivyo sasa? Baada ya ukoloni Tanzanian ilikuwa hivi? Baada ya kuingia vyama vingi Tanzania unaionaje? Wacha kuwa na mawazo ya ujima wewe.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Tulipotoka na tulipo sasa kuna hatua kubwa kama nchi tumepiga, shida ni moja tu tuna wapigaji wengi mnooooo
Watu wapo kwa ajili ya fursa za upigaji! Nchi nzima viongozi wote azma yao ikiwa upigaji nafikiri maendeleo yatakuwa swala la kusadikika kabisa😆
 
Siwakatishi tamaa ila huo ndo ukweli

Nchi yetu haina dalili ya kuendelea kabisa

Deni la taifa ni trilioni 80

Na asilimia kubwa ya bajeti yetu huishia kulipa madeni, watumishi nk...Fedha za maendeleo ni kidogo mno sasa hapo mtaendelea vipi?

Mfano halisi ni wizara ya fedha, waliwekewa bajeti ya trilioni 12....Ambapo trilioni 10 zinaenda kulipa madeni...Sasa hapo mtaendeleaje?

Pesa zimekua zikiishia kwa wachache majority wanabaki na hawaguswi na miradi ya umma

Tutaendelea vipi wakati hata dalili ya kuacha kutegemea misaada haipo?

Tutaendelea vipi deni linazidi kukua na fedha zote asilimia 90 huishia kulipa madeni na watumishi wa umma?

Tutaendelea vipi huku tunazidi kukopa imf na wb na tunawapa migodi,mafuta na gesi vinaenda ulaya?

Tutaendelea vipi na sera za hovyo hovyo tu nchi haijulikani inapoenda?

Tutaendelea vipi kila rais akija anakuja na yake?na mambo yake akiingia mwingine naye anabomoa yale ya mwenzie anaanza na yake na mwingine akija ni hivyo hivyo?Ni sawa na nyumba unaanza na msingi,kisha fundi anamaliza mkataba,anakuja mwingine anabomoa msingi anaanza wake wa style na nyingine anamaliza anakuja mwingine anavunja anasema sio hivyo anajenga kivyake... Haya yanafanyika kila baada ya miaka 5 nchi hii

Tutaendelea vipi wakati kuna chain ya pesa kuliwa from top area(mawaziri,marais) hadi bottom area (serikali za mitaa na wananchi) Yaani hela inaanza kudonolewa kuanzia juu huko hadi ije kumgusa mwananchi wa chini ishaliwa

Pesa yenyewe ya miradi na maendeleo inayotengwa ni kidogo na bado inadonolewa na kupunguzwa kwa kuliwa hadi ije mfikia mtu wa chini ishapungua au kwisha kbs

Kwa haya tutaendeleaje?SIDHANI KAMA HII NCHI ITOKAA IENDELEE KAMWE!!!!!!!
Tukipata anayetaka tuendelee tutaendelea
 
Ahsante kwa mada na hoja nzuri.

Kwa tafsiri yangu ambayo inaweza isiwe rasmi ni kwamba,Maendeleo ni hali ya upigaji wa hatua ya mwanadamu ambayo uhusisha vitu hai na visivyo hai(Living & non-living).

Nadhani maswali ya kujiuliza ni haya

1.Je,toka tumepata uhuru masuala ya huduma ya afya(Hospitali,vifaa tiba) yalikuwaje na mpaka mwaka huu wa 2021 yapoje?,je tulistahili kama Taifa kuwa hapa kutokana na rasilimali tulizonazo?,Je tumepiga hatua kubwa sana au tunajongea kwa mwendo wa kobe?ni nini shida na inapaswa viongozi wafanye nini?

2.Je,toka tumepata uhuru masuala ya elimu yapoje ukilinganisha na huu mwaka wa 2021?,je tumepiga hatua au ndo tunajongea kwa mwendo wa kobe?,Je shule zinatoa elimu bora au bora liende?,je elimu yetu inawaanda vijana kutatua tatizo la ajira au ndo inawaanda kuwa tegemezi katika ajira?,Je elimu ya sasa ni bora kuliko ya mwaka 1961?,na kama ni bora je ubora upo kwenye nini?

3.Je,toka tumepata uhuru maisha ya mtanzania yamebadilika kwa kiasi gani ukilinganisha mwaka huo 1961 na mwaka huu wa 2021?,Je mwaka 1961 tuliishi kwa kiwango cha dola ngapi kwa siku ukilinganisha na mwaka huu wa 2021?,Je mtanzania aliyeishi mwaka 1961 na mwaka huu 2021 ni yupi alikuwa au mwenye nafuu ya maisha ?unadhani ni kwanini?,Je mtanzania unadhani ananufaika na rasilimali zinazomzunguka ?,kama sivyo ni kwanini?,Je maisha anayoishi mtanzania yanaridhisha?,na kama hayaridhishi ni wapi mtanzania anakwama au anakwamishwa?.

4.Je,toka tumepata uhuru mpaka leo ni vipi suala la miundo mbinu?,je inaridhisha au tunaendelea kunikongoja kama bibi kizee kwenye fimbo?,Je ukioanisha rasilimali tulizonazo nchi hii na hatua tunayopiga kwenye miundo mbinu vinaoana?,Je,tumepiga hatua kubwa sana kiasi kwamba mpaka tumetekewa au tuko nyuma sana kiasi kwamba mpaka tunajishangaa?,unadhani kwa uchache au uwingi wa rasilimali tulizonazo tulipaswa kuwa hapa tulipo?,kama sivyo ,je tufanye nini kama taifa?

5.Je,toka tumepata uhuru mpaka leo,suala la maji safi ya kunywa na kutumia kwa watanzania inaridhisha?,je mwaka 1961 hali ilikuwaje na sasa mwaka 2021 hali ikoje?,Je tumastahili kupongezana au tumepuyanga?,Je kulingana rasilimali nyingi na vyanzo vya maji vingi tulivyonavyo leo mwaka 2021 ni haki watanzania kukosa maji safi na salama ya kunywa na kutumia?,Je kama kuna tatizo ni nini kifanyike ili kila mtanzania "ai-enjoy" rasilimali za taifa lake?,shida ni nini,Je ni bajeti ndogo au tuna sera za huduma za maji mbovu?,kukiwa na upungufu je,nani achunwe ngozi(alaumiwe)?

6.Je,toka tumepata uhuru mwaka 1961 mpaka leo mwaka 2021 masuala ya ulinzi na mali za watanzania zipo salama?,Je mtanzania yupo huru kufanya atakalo ilimradi asivunje sheria zilizowekwa au kuna manyanyaso?,Je,vyombo vya ulinzi na usalama vinatimiza wajibu wao kwa kila mtanzania pasipo shuruti za kisiasa?,Je,toka mwaka 1961 mpaka mwaka huu 2021 wafanyakazi wa vyombo hivyo vya usalama wanatendewa haki ikiwemo posho na mishahara?,Je,miundo mbinu ya mwaka huu wa 2021 ni bora ukilinganisha naya mwaka 1961?,Je ,vifaa na nyenzo za vyombo vya usalama ikiwemo magari,mavazi n.k vina akisi uwingi wa rasilimali tulizonazo au ndo bado tunajikongoja kwa mwendo wa kobe?.

Ndugu zangu nadhani yangu ni hayo,na wewe pia waweza ongezea ili tuone namna tulipo toka,tulipo na tunapoelekea,Je kuna maendeleo yoyote ukilinganisha na rasilimali tulizonazo nchi hii au tunajongea kwa mwendo wa kinyonga?
 
Mtu anayesema hii nchi haiendelei sijui anatumia criteria zipi ... na data ziko wazi kabisa
Iko wazi mbona, sisi tunaendelea kinyumenyume

Kwa rasilimali zetu wenzetu tuliokua nao Sawa miaka ya 70's Ni;

Malaysia,
China,
Vietnam,
peru.k

Kwa wakati huo hata GDP zetu ziliachana tarakimu chache sana,

Nchi wenzetu Kama Vietnam walikuja kujifunza tunavyowekeza kwenye zao la korosho

So mwamba yupo sahihi kabisa sisi tunarudi beki mpaka dunia ikiisha nadhani tutakua tumefanikiwa kufika ZERO
 
Masystem ya kudhibiti hela yaliyokuwa launched kipindi cha mwendazake yangesaidia sana kuongeza pato la taifa..Lakini ndo inakuwa easymoney kwa baadhi mipanya iliyopo sasa madarakani
 
Huo unaoitwa ufisadi na ubinafsi una mizizi mirefu hapa nchini, tayari tulishafundishwa staili ya chukua chako mapema toka shule ya msingi...
 
Back
Top Bottom