Tanzania haitasalimika! Kenya yatumika na Magharibi kuishambulia Alshabaab! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania haitasalimika! Kenya yatumika na Magharibi kuishambulia Alshabaab!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Profesa, Oct 20, 2011.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Haiingii akilini kwamba Kenya wanaweza kuingia kwenye vita leo hii? Sidhani kuna any push factor to this extent mpaka wanaamua hivi! Na sidhani kama wana uchumi mzuri kiasi hicho wa kuafanya waende vitani leo hii! Nadhani huu ni mkakati mpya ambapo hata Tanzania inaweza kutumika siku moja. Imeonekana kuwa ni gharama sana kutumia vifaa vya kivita kutoka Ufaransa au Markani au kuleta wanajeshi Obvious, ni gharama kisiasa kwa mataifa haya na ni gharama hata kimahusiano maana tayari wanashutumiwa kwa mambo wanayoyafanya huko Libya na kwingineko. Sasa njia pekee ni kuwatumia majirani, kwa mkataba maalum.

  Nikiangalia Historia ya Kenya na Somalia, bado hainiingii akilini kabisa. Na usisahau hao Al-Shabaab wakati mwingine wamekuwa wakiishi ndani ya Kenya na wakipanga mipango yao kutokea Kenya na hata baadhi ya Suply (bidhaa za matumizi) hupitia huko muhimu zaidi Mirungi (miraa) kutoka Kenya!

  You may be interested on this link: http://allafrica.com/stories/201107300012.html
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sasa unataka tufanye nini? Tuhamishe ujirani na Kenya? Hivi wewe sababu za Kenya kuingia vitani na Alshabaab wewe huzijui au huzikubali?
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi hakuna mtu anayeweza kuwapinga Al Shaabab bila kuonekana anatumiwa na wamagharibi? leo hii Tanzania inajikuta inashughulikiahilo tatizo la Wasomali wageni na kuwa mzigo kwa taasisi zetu mbalimbali. Sasa leo likitokea tukio dhidi ya Tanzania (fikiria meli ya Kitanzania ivamiwe na watu wauawe) tukiamua kwenda na kushirikiana na Kenya kwenda kupacify Somalia tutakuwa tunatumiwa na Wamagharibi? Yaani, maslahi ya nchi za Kiafrika yaamuliwe London au DC?

  Matokeo yake ndio tunaweza kujikuta tunafumbia macho mambo mengine kwa kuogopa kuonekana tunatumiwa na "Wamagharibi"!
   
 4. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Wewe unafiria wangefanyaje? Magaidi wanawateka wageni wao na hvyo kupunguza fedha za kitalii,wewe unaona wangekaa kimya? Wanachofanya kenya ndo inatakiwa serikali shupavu ifanye,adui kama huyo afuatwe mpaka uvunguni kwake atiwe adabu.
   
 5. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Alshabaab kwa mambo wanayoyafanya hawafai kabisa...
   
 6. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji well said.

  Haya ni mawazo mgando ya kusema kuwa kila nchi ya kiafrika inapokwenda vitani kupambana na Magaidi kama AL-SHABABI wanatumiwa na nchi za Magharibi. Ni ujinga na upuuzi kuwazia hivo.

  Mwaka 1978 Tanzania tulitangaza vita na nduli Idd Amin Dada baada ya kuivamia Tanzania. Je,tulitumiwa na Mataifa ya Magharibi??? La hasha. Ilikuwa ni maamuzi ya Kiongozi wetu shupavu Mwl. JK Nyerere. Kwamba joka lilikuwa limeingia nyumbani ilikuwa lazima li[pigwe na lisakwe popote litakapokuwa. Tulifanya hivo na tukamung'oa nduli Amin na tukaweza kuikomboa Uganda.

  Kenyans are doing the same today in Somalia. They're waging a war against Al-Shaabab baada ya uchokozi wa kuingia kwenye mipaka ya Kenya na kuteka Watalii kutoka Ulaya. Kenya wanategemea sana Watalii kuinua Uchumi wao. Wasingeweza kukaa kimya wakti uchumi wao unaanza kutishiwa na Al-Shababi.Hata Tanzania tusingekubali upuuzi kama huo.

  Mimi nawapongeza Kenya kwa moyo wa dhati kabisa kwa uamzi wa kuingia Somalia kuwasaka Magaidi wa Al-Shaabab. Watu hawa ni hatari kwa ustawi wa Kenya,Somalia,Africa na dunia nzima kwa ujumla. Lazima vikundi hivi vya wahuni vinavyojidai viko chini ya mwavuli wa dini ya Kiislamu vidhibitiwe na kusambaratishwa kwa haraka sana.

  Big up Kenyans. Malizeni na kusafisha Al-Shababi tuko nyuma yenu.
   
 7. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,074
  Likes Received: 7,563
  Trophy Points: 280
  Tofauti na Kenya inavotambulika lakini kwa hili la Alshabaab wamekuwa wavumilivu sana, nadhani walikuwa wanatengeneza military strategy namna ya kuendesha operation hii, kama inavyoeleweka kuwa ni operation dhidi ya taifa ambalo tayari lina namba of refugees wake nchini Kenya, na kwa operation hiyo huenda wakimbizi wakaongezeka na yeyewe kujikuta ikijiongezea 'mzigo ' wa kuwa accommodate wakimbizi hao, ambao huenda na wapiganaji wake wakatumia mwanya huo kuingia Kenya kwa mashambulizi ya kujitoa mhanga na mengineyo ya kigaidi.
  Hivyo Kenya wapo sahihi kwasababu kila mmoja anaelewa namna hali ambavyo imekuwa tete nchini Kenya na usalama kudunika kutokana na hali ya mambo nchini Somalia.
  Ni suala ambalo hata sisi tuliwahi lifanya, sema sasa hivi hatuna tena uthubutu huo mbele ya watu wasio hata na jeshi yaani mafisadi.
   
 8. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2011
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Ulitaka waje Wamagharibi wenyewe kutusaidia kuwaadabisha Al Shabib? Sijaelewa... Nilishangilia kusikia, angalau kwamba tunaweza wenyewe kumtia bakora mdogo wetu mkorofi badala ya kukimbilia kushtaki kwa mpita njia. Vita mbaya, lakini uchokozi gani huo kuingia hadi nchi ya watu kufanya uhuni? Wangeachiwa unadhani matokeo yake ni nini? Kwenda hadi ikulu kuchukua watakacho, kisa? Wao Al Shabib. Mi naona poa tu.
   
 9. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kitendo cha Kenya kuamua kuingia vitani na Alshabaab ni ishara nyingine ya uthubutu walio nao wakenya, uwepo wa hili kundi unakwamisha kwa kiasi kikubwa jitihada za kimaendeleo kwa nchi zetu kwa maana hata baadhi ya nchi zinasita kuleta meli zao kwenye ukanda huu kwa kuhofia kutekwa nyara. Nilitegemea kusikia nchi nyingine za Afrika Mashariki kuunga mkono jitihada za Kenya lakini mpaka dakika hii tumekaa kimya......
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kitu ambacho sijapenda ni kuwa Kenya wamefanya out ouf a knee jerk reaction; sidhani kama wamefanya based on strategic military action. I hope I'm wrong. Maana tatizo la Al Shaabab halina tofauti na tatizo la Kony na katika wazimu wetu nchi zetu za Afrika zimeshindwa kushugulikia yote mawili.
   
 11. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Kenya wameonyesha uhalisia wao kwenye mambo yanayohusu masuala ya nchi na wanahutaji pongezi juu ya hilo.Alshababu ni kundi baya lenye malengo mabaya likiachwa hivi hivi litaota mizizi(au limeshaota mizizi)hata hapa kwetu Tz.Watafutwe na wamalizwe Alshababu hawafai.
   
 12. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,074
  Likes Received: 7,563
  Trophy Points: 280
  Samahani Mzee Mwanakijiji ukiondoa ufanano wa makundi hayo mawili yaani Kony na Al Shabaab katika malengo yao ya Kidini, unaweza ukatupatia kufanana kwao kwingine ni kupi?

  Kony (LRA) ------------------------------------------------------- Al Shabaab (Mujaheddin )
  1.
  2.
  3.
  4.


  Na je naweza nikafahamu hisia au clues ulizonazo kuwa ni kwanini unadhani Kenya hawakuwa based on Military Action Strategies?
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Si Al-Shaabab tu bali pia Al-Shaabablets walioingiza hela za kumwaga Kariakoo pamoja na wafadhili wao na wale wote woliokua wanatumika kumdhuru kiongozi wetu Dr Mwakyembe ...

  Mwache tu aendelee kukingia kifua Al-Shaabab pengine ni mpangaji wao au mwenyeji kwa 'wageni' hawa waharibifu ambao hivi sasa wanatumika nchini kwa malengo ya kisiasa.

  Ni kweli Tanzania kama nchi, tunahitaji sana wawekezaji na hasa katika real estate; kujenga majengo marefu kiloko yote duniani hapa nyumbani, mihoteli, makazi ya watu na hata sehemu za biashara LAKINI huyo mwekezaji akiwa ni Al-Shaabab bunduki kiunoni muda wote - hapana hatumtaki!!!!!

   
 14. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,782
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkuu ulitaka Kenya wafanye nini? Kama hawa jamaa wanaanza kuhatarisha moja ya vyanzo vikuu vya mapato ya Kenya,waangalie tu? Hata sisi miaka michache iliyopita tulitumia JWTZ kuangamiza kundi la maharamia wa Kisomali waliokua wanateka na kuua watalii huko Ngorongoro.
   
 15. D

  DONALD MGANGA Member

  #15
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi siwatetei sana kenya sababu wamechelewa kuchukua hatua madhubuti mapema. Hawa wanyama ndo watekaji wakubwa wa meli na hela zao hupitia Djibouti ama kenya. sasa mianya ya uhalamia imeaaza kuzibwa wanataka kuteka watalii. Ukitaka kujua hela yote haramu iko wapi kenya nenda Eastlands au Esilii wao wanavyotamka utafikiri uko Mogadishu jinsi kulivyo na wasomali wengi na sasa kuna maghorofa ya nguvu sana huko. Kwa maana hiyo basi wenzetu wa kenya wakitaka msaada tuwape haraka iwezekanavyo kuepusha maafa zaidi
   
 16. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Profesa mzima umeandika CRAP, hlafu ni kama vile unalalamika
   
 17. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Inaitwa "Operation LINDA NCHI"

  Kama unadhani uchumi mzuri ndio kigezo cha kupigania uhuru/sovereignty yako basi siku moja watamchukua mkeo (kama unae) nawe utasubiri uchumi wako ukae sawa ndio upambane na adui!!!

  Alshabab wamepandisha gharama za maisha ukanda huu bila hatua mahsusi kuchukuliwa....let KIBAKI and Kenyans take the lead.
   
 18. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 738
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Tubadilike jamani, kila jambo zuri wakifanya nchi za kiafrica utasikia kuna mkono wa marekani. haya ni mawazo ya kikoloni, tuwaunge mkono kenya, hawa watu wamekuwa kikwazo sana africa mashariki, watalii wanakimbia, wanatishia amani ukanda wa africa mashariki. mashambulizi ya ubalozi wa marekan nchin wahanga wengi ni watanzania ambao hawakuwa na hatia yoyote. ugaidi, al shabab ni kundi hatari sana.
   
 19. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wewe sijui unaota. wakitaka msaada upi? wa vita? Hatutaki. Ukome, ushindwe na ulegee.
   
 20. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #20
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  hakuna vita ngumu kama vita ya kupigana na wanamgambo au watu wa kikundi fulani wasio na sare zinazofahamika.
  Chunguza hili, vita vingi vya wanamgambo Duniani huwa haviishi.
  Na hata hii vita walioianzisha Kenya ni wazi kuwa itakuwa ngumu na itawagharimu sana coz hawa wala Mirungi waliokubuhu toka Somalia hawana cha kupoteza zaidi ya Roho.
  ila kama wakifanikiwa kulipua majengo kadhaa ya Kenya au kushambulia makazi ya watu nahisi itakuwa ni ushindi mkubwa mno kwao...
   
Loading...