Tanzania haitambui ushindi wa Mugabe - Membe

Sasa ishu za Mugabe na Zimbabwe, nani amuhonge yupi kwa manufaa ya nani na siasa zipi?Ni incompetence tu. Hawajui fani yao wale watu.Harare imemwita balozi nyumbani hawaandiki? Hao watu wameenda shule ya Uandishi kweli? Au wanashindwa kuumuliza Mbunge hizo habari umezisikia wapi, mpaka anakuja kuulizwa hapa JF? Kuna press hapo kweli? Please Mushi, be objective for a second.

Kuhani soma NewAfrican la mwezi June linaloenda kwa kicha cha habari "Exposed Western Media Bias Against Africa:Whatever you thought about Africa, think again!" unaweza kuelewa na nani anamuonga nani katika mazingira kama haya, mfano mzuri na Cameron Duodu alipoandika makala kali kwa mhariri wa gazeti Ghana na jinsi ilivyozimwa na maofisa wa ubalozi wa US Accra!
 
Kama waandishi wa Tanzania wanahongwa na Foreign officials wa Tanzania eti wasimswalishe Kikwete kuhusu foreign policy ya Tanzania au wasiandike kwamba Harare wamemwita Balozi nyumbani basi hiyo inadhihirisha claim yangu: hakuna press. Mwisho wa hadithi.
 
Kina TSIVANGIRAI sasa wameenda kukamata watoto na kina mama wenye njaa na wamewapeleka huko kwenye UBALOZI WA US ZIMBABWE!
ETI WANADAI WANAHOFIA MAISHA YAO!
NA SASA WANAWAONYESHA HAPA KWENYE CNN KILA MARA!
ILI KUPATA HURUMA YA WAMAREKANI!
SASA NGOJA HISTORIA YOTE WAWEKEWE WAMAREKANI UONE KAMA HAKITAWAGEUKA..TENA UKIZINGATIA MUGABE NI SADDAM WA BLAIR!
AMA KWELI MAMLUKI MUNGU NA AWALAANI!
 
Nadhani hapa kwa ujumla tumechemka kiasi ambacho hatujawahi. Kimsingi Membe amesaliti jitihada zote za waafrika katika kuhakikisha misimamo yetu ni kwa ajili ya maslahi ya bara letu. Hivi msimamo huo wa Membe unamsaidia nani hasa?

Jibu hapo ni msimamo huo unamsaidia mkoloni!
 
Hii vita tuliishinda kwenye jukwaa la kimataifa na kumsababishia Kikwete kubadili kauli ama mawazo...Sasa niliwaambia inakuja kitaifa...HIYO SASA!
 
Mafuchila,
Kwanza kulinganisha msimamo wa tanzania na swala la Zanzibar utakuwa huitendei haki CCM bara. Tangia uchaguzi alioshinda Komandoo, the Mwalimu alimwambia Komandoo aunde serikali ya mseto akakataa, hata juzi tu tumeshuhudia juhudi za JK za kutaka mseto zikikataliwa na wazanzibar, sasa unataka Tanzania bara ilazimishe wazanzibari kukaa pamoja?
Ndo maana hata JK alipohudia kikao cha bunge kwa mara ya kwanza kama raisi alisema atajitahidi kumaliza mpasuko lakini ili yote yafanikiwa ni mpaka wazanzibar wenyewe watake, sasa tumeona wazanzibar hawako tayari kukaa pamoja kambi zote mbili zinatumia muungano kwa manufaa yao binafsi.
 
Yebo Yebo kweli unanichekesha!
Haya mambo ya mpasuko wa JK yametoka wapi?
Taifa kupasuka ama kuuzwa?Si bora lipasuke kuliko kuuzwa?
Mambo ya ccm ni baadaye...Now ni maslahi ya TAIFA!
 
Ni Bora ila wasifanye kwa mashinikizo ya nje mbona walimkubali Kibaki?

This is double stadards, japo naunga mkono kutokumtambua Mugabe.

forget about Kibaki! Mbona hawamtambui Mugabe!? Safi sana AU!!! Keep it up, kumbe mnaweza.
 
KAMA KWELI AMETOA TAMKO BASI LITAKUWA LINAKINZANA NA SERA YA MAMBO YA NJE YA TANZANIA.......! 'to promote african unity/good naighbouliness/non-alignment(NAM) AMBAZO ZIMEKUWA RE-DEFINED ILI KENDANA NA HALI YA SASA.......!
( LABDA TUNATAKA WALE WAKULIMA WALIOFUKUZWA WAJE KWENYE MAPORI YETU YASIYO NA MTU) shamba la bibi.....!
 
pale sinza kuna shule inaitwa MUGABE..... ! AS LONG AS HATUMTAMBUI NINI KITAFANYIKA?
 
Date::7/3/2008
Tanzania yatangaza kutotambua urais wa Robert Mugabe Zimbabwe
*Yasema uchaguzi ulikiuka vigezo vyote vya demokrasia

Na Muhibu Said

...Alisema msimamo wa kutotambua uchaguzi wa Zimbabwe, unaungwa mkono pia na AU na Sadc, baada ya kuridhika na ripoti ya waangalizi wa uchaguzi huo.

''Katika mkutano wa wakuu wa nchi za AU nchini Misri, hakuna kiongozi aliyeunga mkono wala kupongeza uchaguzi wa Zimbabwe,'' alisema Membe...

Source: Mwananchi 03/07/2008 in http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=6448

binafsi nadhani serikali imeharakisha sana kutoa tamko hili.
kwa maneno mengine kwa kauli hiyo tanzania imekwishajiondolea rasmi
uwezekano wa kuwa msuluhishi wa mgogoro wa zimbabwe kwani imekwisha chagua upande. kwa siasa zetu mwenyekiti wa au ndio amekwishajitoa kusaidia juhudi za upatanishi.

hivi au ilitoa communique ya kuupinga uchaguzi wa zimbabwe? kwa maana kama au wanamsimamo mmoja katika hili naamini kungekuwa na communique ili kuongeza shinikizo na kuitambulisha dunia kuhusu msimamo wa afrika ambao ulikuwa unangojewa kwa hamu. kwa mtazamo wangu ni kwamba afrika haina msimamo wa pamoja katika hili suala.

mbona kenya tanzania haikutoa msimamo na tuliambiwa zinafanyika juhudi za kimya kimya kurekebisha mambo? kulikoni zimbabwe serikali yetu kuwa mstari wa mbele?

kweli jongwe anaharibu mambo huko zimbabwe lakini mkakati wa serikali ndio unaharibu zaidi.
 
Kafara,
Usiharakishe kuhukumu. Nahisi kuna strategy baada ya mkutano wa AU kumtenga kando Mugabe. Sidhani Tanzania imekurupuka tu.
 
Huu sasa ujinga huu, mbona Mwenyekiti wa AU aliwapongeza Wazimbabwe kwa uchaguzi huko Egypt halafu anarudi nyumbani na kudai hautambui uchaguzi huo, sasa alikuwa anapongeza nini basi... duh! Huyu mheshimiwa has the uncanny ability of making a fool of himself routinely, well, at least he is good at something!
 
aliingia akiamini kuwa yeye ni Rais wa Zimbabwe. Hadi mkutano unafanyika kule Misri AU hawakuwa na msimamo juu ya Mugabe, sasa wanao. Ina maana ukifanyika mkutano mwingine kesho, Mugabe akiruhusiwa kuingia kama Rais ndipo tungekuwa na mzozo.

Na pia sioni ugumu wa ili kueleweka. Kama msimamo hatimaye wa kutomtambua umekamilika nje ya muda wa kikao tatizo ni nini? Labda hadi jana ndio walikuwa wana negotiate na hatimaye kutoa msimamo wapamoja.

Sasa AU imesema haimtambui, itashangaza kama wanachama wake watakuwa wanamtambua!

hapana mzee, mambo ya nje ya kikao ni nje ya kikao. mambo kama haya lazima yafanyike kwenye kikao rasmi vinginevyo msimamo (kama upo) unabakia "informal" na unakuwa hauna mshiko.
 
Angalia makala yangu ya leo kwenye Tanzania Daima. Bernard Membe amesema kuwa Umoja wa Afrika hautambui Mugabe kama Rais wa Zimbabwe. Zaidi ya yote kwa niaba ya Mawaziri wa SADC amesema kuwa Au haiutambui uchaguzi uliofanyika huko Zimbabwe.

Mkuu MJJ,
Nafikiri uelewa wako wa suala la Zimbabwe ni mdogo sana na article yako inaonyesha wazi hilo.
  1. Sababu zipi za kisheria TZ itatoa za kutoutambua utawala wa Mugabe?
  2. Una maana gani ya kuwa TZ itakua imehalalisha kiongozi mbovu, hao wengine Africa wanatofauti gani na Mugabe? Kipimo chako ni kipi?
  3. Unasema kuwa Mugabe kashindwa kuona alama za ukutani, hivi 42% vs 47% votes ndio unasema kashindwa kuona alama? This was a very close contested election.
  4. Umesema matatizo ya Zim yamechangiwa na mambo mengi, ni yapi hayo na kwa kiwango gani? Any solution?
Kwa wewe kulinganisha upinzani Zimbabwe kuwa sawa na TZ nafikiri inaonyesha jinsi usivyoelewa yanayoendelea huko Zim. Jielimishe zaidi na hili suala kabla hujaliingilia maana inaelekea unayoongelea ndio msimamo wa CHADEMA (compare it with Zitto statements). Kwa misimamo yenu butu, mnaweza mkawa mnasaidia kikundi fulani ndani ya CCM ambacho nina uhakika misimamo yao juu ya Zimbabwe ni kwa maslahi yao binafsi na wala sio kwa ajili ya watu wa Zimbabwe, SADC au hat TZ. Zidumu fikra za Mwalimu.

NB: Bernard Membe was neither speaking on behalf of AU nor TZ. He was speaking on behalf of those who sent him to condemn Zim election, even before a vote was cast.
 
Nikiwa nje ya nchi nimesoma na kuona taarifa za luninga kwamba raisi Kikwete alitoa kauli ya kumpongeza Robert Mugabe kwa kuchaguliwa kuwa raisi wa Zimbawe na dunia yote inaelewa hivyo.

Halafu akaja raisi Thabo Mbeki ambae ametoa kauli akiwa "chief mediator" wa suala la Zimbabwe, kwamba suala la Zimbabwe liachwe kwa wazimbabwe na katoa kauli hiyo kwa vyombo vyote vya habari ulimwenguni na vimeandika hivyo.

Pia nikiwa nje ya nchi sijapata kauli yoyote ya kusema kwamba Tanzania, ikiwa mwenyekiti wa AU inapinga uchaguzi wa Zimbabwe na kwamba haimtambui raisi wake Robert Mugabe na kwamba uamuzi huo unakuwa unatambulika kimataifa.

Lakini nikiwa pia nje ya nchi nasoma habari kutoka katika gazeti la kitanzania kwamba Bernard Membe akiwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania anatamka(kwa waandishi wa habari wa Tanzania na wengine) kwamba serikali ya Tanzania haimtambui raisi Robert Mugabe!

Pia baada ya kumsikiliza bwana Membe kupitia BBC natambua masuala mawili ambayo anasema yamefikiwa, kwamba suala hilo kuachiwa nchi za SADC ambao watalishughulikia na kuitaarifu AU.

Na pili ni kuwepo kwa kikao cha nchi za SADC.

Sasa baada ya kusema haya naona kwamba hoja kwamba Tanzania haimtambui Robert Mugabe ni ya kizushi na ni "spinning".
 
hapana mzee, mambo ya nje ya kikao ni nje ya kikao. mambo kama haya lazima yafanyike kwenye kikao rasmi vinginevyo msimamo (kama upo) unabakia "informal" na unakuwa hauna mshiko.

Kafara, hata kama tukikubali yanayosemwa nje ya vikao ni formal na yana mshiko -grant them that hypo for a second - mimi nauliza hayo maamuzi ya AU hayo yalifikiwa lini, wapi?

African Union walikutana Ikulu, Magogoni Street wakaamua? Au walikutana mjini kwenye ukumbi wa Maelezo ?
 
Kafara,
Usiharakishe kuhukumu. Nahisi kuna strategy baada ya mkutano wa AU kumtenga kando Mugabe. Sidhani Tanzania imekurupuka tu.

hapana mkuu, sio hukumu ila ni mawazo. kama ningekuwa na uwezo wa kubadili msimamo wa serikali katika hili, hakika ningetoa hukumu.

hiyo strategy ya kumtenga jongwe ndio inakuwaje? sidhani kama ni rahisi kurekebisha hali ya zimbabwe bila kumshirikisha huyo mkuu. hiyo ndio hali halisi. na naamini jongwe atakuwa msikivu zaidi iwapo atakuwa na imani kwamba wasuluhishi hawajachagua upande.
 
Mkuu MJJ,
Nafikiri uelewa wako wa suala la Zimbabwe ni mdogo sana na article yako inaonyesha wazi hilo.
  1. Sababu zipi za kisheria TZ itatoa za kutoutambua utawala wa Mugabe?
  2. Una maana gani ya kuwa TZ itakua imehalalisha kiongozi mbovu, hao wengine Africa wanatofauti gani na Mugabe? Kipimo chako ni kipi?
  3. Unasema kuwa Mugabe kashindwa kuona alama za ukutani, hivi 42% vs 47% votes ndio unasema kashindwa kuona alama? This was a very close contested election.
  4. Umesema matatizo ya Zim yamechangiwa na mambo mengi, ni yapi hayo na kwa kiwango gani? Any solution?
Kwa wewe kulinganisha upinzani Zimbabwe kuwa sawa na TZ nafikiri inaonyesha jinsi usivyoelewa yanayoendelea huko Zim. Jielimishe zaidi na hili suala kabla hujaliingilia maana inaelekea unayoongelea ndio msimamo wa CHADEMA (compare it with Zitto statements). Kwa misimamo yenu butu, mnaweza mkawa mnasaidia kikundi fulani ndani ya CCM ambacho nina uhakika misimamo yao juu ya Zimbabwe ni kwa maslahi yao binafsi na wala sio kwa ajili ya watu wa Zimbabwe, SADC au hat TZ. Zidumu fikra za Mwalimu.

NB: Bernard Membe was neither speaking on behalf of AU nor TZ. He was speaking on behalf of those who sent him to condemn Zim election, even before a vote was cast.

SADC ilipeleka waangalizi wa uchanguzi huko Zimbabwe tangu mwanzo. Wametoa ripoti yao ya jinsi walivyoona kuanzia kampeni mpaka uchaguzi wenyewe. Ni kuwa uchaguzi huo haukutimiza hata moja ya taratibu ili uitwe wa kidemokrasia. Kufiuatia taarifa hiyo Tanzania inaweza kutoa tamko kama ilivyotoa. Ripoti ya waangalizi ni sababu tosha ya kutoutambua utawala wa Mugabe
 
Back
Top Bottom