Kafara
JF-Expert Member
- Feb 17, 2007
- 1,396
- 411
Kwa Hili Serikali imesimama upande sahihi.....Hongera Mh. Membe
Wakuu inatubidi kuipongeza serikali ya Tz kwa msimamo iliounyesha juu ya sakata hili la Zimbabwe.
H.E J.Kikwete, Hon. Member, You are the new beacons of light to shine where there is darkness in African continent.
Maelfu ya Wazimbabwe wanateseka; wazee, wanawake na watoto kwa kuwa tu Bob. Mugabe/ Jongwe anataka kuendelea kung'ang'ania madaraka na pengine hadi afie hapo. 'This can not be right and it will never be right'.
Nimepata fursa ya kuwa karibu na Wazimbabwe kadhaa, na wanaonyesha masikitiko makubwa kile kinachotokea nchini mwao. Bob Nugabe has turned from 'HERO to ZERO'.
Mkuu Kitila nimekusoma vizuri, ni upofu wa hali ya juu eti ili uonekani Pan-Africanist inabidi umuunge mkono BOB. huu ni upungufu wa fikra na mtazamo sahihi.
Maana ya Pan-Africanism kama ni hiyo inayotaka kupindishwa basi wengi hatumo.
Nnnajua hapa macritics watataka kuchanganya madawa wa kuikoroga hii topic na mambo mengine yasiyokwenda sawia pale nyumbani. i.e Kiwira, EPA n.k. Lakini ikumbukwe pamoja na masakata yote ya hapo nyumbani, 'we 'll be failing our duty as Africans, if we don't speak loud and clear in condemnataion of such sham, unfair and un-democratic election that has put back Bob into power again.
Mungu ibariki Afrika
Mungu wabariki Waafrika.
hapa ndio naona kunaupindishwaji wa hoja za wengine. nimerudia zaidi ya mara mbili kueleza kwamba wengi humu tunaamini anayofanya jongwe kwa wananchi wake si mazuri. hata hivyo tunachotofautiana hapa ni njia ambayo serikali yetu imechukua katika kutatua huu mgogoro.
sasa kama tusioafiki na jinsi serikali inavyoli-handle hili suala kunatafsiriwa ni kumuunga mkono jongwe na upofu wa mawazo hiyo ni utashi wako kuwaza hivyo ila nina hakika mimi si kipofu wa mawazo na wala siungi mkono maovu anayofanya jongwe kwa watu wa nchi yake.