Date::7/3/2008
Tanzania yatangaza kutotambua urais wa Robert Mugabe Zimbabwe
*Yasema uchaguzi ulikiuka vigezo vyote vya demokrasia
Na Muhibu Said
TANZANIA imesema haimtambui Robert Mugabe kama Rais halali wa Zimbabwe kwa kuwa amechaguliwa katika uchaguzi uliokiuka vigezo vyote vya demokrasia.
Msimamo huo wa Tanzania, ambao ni wa kwanza kutolewa tangu uchaguzi wa rais Zimbabwe urudiwe Juni 27, mwaka huu na kumrejesha Mugabe madarakani, ulitangazwa jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Waziri Membe aliwaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya wizara hiyo, jijini Dar es Salaam kuwa msimamo huo umefikiwa kwa vile ushindi wa sasa wa Mugabe ni sawa na kufunga goli la kuotea katika mpira wa miguu.
''Uchaguzi wa Zimbabwe ni sawa na mchezo wa mpira. Goli la Mugabe limekuwa offside (la kuotea),'' alisema Membe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika (AU).
?Alisema ukiukwaji wa vigezo vya demokrasia katika uchaguzi wa rais wa Zimbabwe, ulibainishwa na ripoti ya waangalizi zaidi ya 413 walioshuhudia uchaguzi huo.
Membe alisema baadhi ya waangalizi, wanatoka Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Bunge la Afrika, wote waliridhika kuwa uchaguzi huo ulipoteza sifa ya kuwa huru na wa haki.
Alisema katika uchaguzi huo baadhi ya vyama (isipokuwa Zanu-PF cha Mugabe) havikuruhusiwa kufanya kampeni na baadhi ya wagombea walinyimwa fursa ya kutumia vyombo vya habari.
Alisema pia vitisho vilikithiri kwa wapiga kura na kwamba, hata vyombo vya habari vilivyojaribu kuwapa fursa baadhi ya wagombea vilifukuzwa Zimbabwe.
Kutokana na hali hiyo, alisema uchaguzi huo hautambuliki na hawaoni sababu ya kuwa na kigugumizi katika kulieleza jambo hilo.
''Hilo halitambuliki, sasa hapo kigugumizi kiko wapi? Kwa sababu ukikubali ripoti ya waangalizi, hutakuwa na haja ya kuuliza kama tunamtambua Mugabe kama Rais halali au la. Uchaguzi hautambuliki,'' alisema Membe alipokuwa akijibu swali la mwandishi mmoja wa habari jana.
Alisema msimamo wa kutotambua uchaguzi wa Zimbabwe, unaungwa mkono pia na AU na Sadc, baada ya kuridhika na ripoti ya waangalizi wa uchaguzi huo.
''Katika mkutano wa wakuu wa nchi za AU nchini Misri, hakuna kiongozi aliyeunga mkono wala kupongeza uchaguzi wa Zimbabwe,'' alisema Membe.
Alisema baada ya mkutano huo uliofanyika katika mji wa Sharm El-Sheikh wiki iliyopita, Mwenyekiti wa AU, Rais Jakaya Kikwete, aliteta na Mugabe na kumtaka ayazingatie yote yaliyozungumzwa katika mkutano huo juu ya hali tete iliyopo nchini mwake.
Hata hivyo, Waziri Membe alisema, AU imeiagiza Sadc ianze juhudi ya kuvikutanisha vyama vya MDC (cha Morgan Tsivangirai) na Zanu-PF, vikutane ili viunde serikali ya mpito, ikiwa ni njia pekee ya kuleta suluhu ya mgogoro wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo hivi sasa.
''Hakuna chama kimoja kinachoweza kutawala peke yake kutokana na hali tete iliyopo Zimbabwe. Sasa hivi Zimbabwe haitawaliki. Zanu-PF haiwezi kutawala,'' alisema Membe na kuonya kuwa:
''Kama mazungumzo yakikwama, vikwazo ndio vitakavyokuwa silaha pekee Zimbabwe,''
alisema.
Source: Mwananchi 03/07/2008 in http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=6448

Last edited by a moderator: