Tanzania haitakuwa Nchi ya kwanza Duniani kwa Viongozi ku-sacrifice mambo kadhaa kwa ajili ya manufaa ya Taifa na Wananchi wake

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Tanzania Haitakuwa Nchi ya Kwanza Hapa Duniani kwa Viongozi Ku Sacrifice Mambo Kadhaa Kadhaa kwa Ajili ya Manufaa Mapana ya Taifa na Mwananchi Wake.

1. Kambarage alipokubali na kuwashawishi wenzake kukubali kura tatu mwaka 1958 njia ya kuelekea kupata uhuru ilianza kuwa nyepesi.

2. De Clerk alipomtorosha Mandela gerezani kwa siri na kukutana naye Ikulu ndogo kwa siku kadhaa akijadiliana naye juu ya hatima ya nchi, ugumu ulipungua.

3. Maalim Seif na Aman Karume walipokutana "kinyume" na matakwa ya vyama vyao, wakazungumza na kutunza siri na kuaminiana, Zanzibar ilibadilika.

4. Uhuru Kenyata na Raila Odinga waliposhikana mkono na kutazamana usoni, Kenya iliyo imara ilizaliwa.

5. Baba Mtakatifu (sasa Mtakatifu) Papa Yohane wa II alipoamua kwenda gerezani kukutana na aliyempiga risasi, Kanisa Katoliki liliimarisha mafundisho yake juu ya msamaha.

6. Tume ya Ukweli na Maridhiano ya Afrika Kusini ilipowezesha maadui kukutana uso kwa uso na kuombana msamaha, uponyaji wa taifa ulianza.

Uponyaji wa taifa au Mwanzo Mpya huanza pale yafuatayo yanapotokea:

i) Viongozi wa pande zinazovutana wanapoamua kuasi sehemu ya misimamo ya pande zao Ili Marithiano ya Pande zote Wahasimu Ufikiwe (Win Win State of Affair). Kutanguliza Maslahi ya Taifa letu Tukufu Mbele na Kukataa Ubinafsi wa Eitha Mtu au Chama.

ii) Kila upande kukubali kupoteza kitu ili kupata Kingine chenye Maslahi na Manufaa Kwa Wote.

iii) Kila upande kukubali kulitanguliza taifa kuliko vyama au maslahi ya muda ya viongozi.

iv) Dhamira imara (commitment) ya pamoja juu ya ukuu wa katiba na utawala wa sheria.

v) Msimamo wa pamoja wa kukiri kuwa kuna Haki sawa. Hapo ni mwanzo mpya wa Maelewano na Amani ya Kudumu huzaliwa .
Tusikubali Kufuga Chatu Ambaye Baadaye Atataka Damu yetu Wenyewe.

(Mahakama na Bunge Zisimamie Dola kwa Kuzingatia Sheria na Haki) Na Sio Chama Kinachotawala
 
Back
Top Bottom