Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,107
- 18,323
Kwa matukio yanayotokea na malumbano yanayoendelea ndani ya vyombo vinavyo husika na ulinzi wa mali na raia, huu ni uthibitisho tosha kwamba Tanzania kwa sasa hatuna Waziri wa Mambo ya Ndani.
Wajibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ni upi?
Katika hali kama hii, wananchi tunapata picha gani kama Waziri wenye dhamana anaonekana kwenye kucheza ndombolo lakini mwananchi akipotea hana sauti?
Pia tungekuwa na Waziri wa Mambo ya Ndani angetusaidia kuwauliza vizuri makamanda wa polisi wa mkoa wa Dar es salaam na yule wa Kinondoni kwa kauli zao zinazoonyesha hawajali maisha ya raia.
Tuna amini Mh Rais ni mtu mwema na anayejali maisha ya Watanzania.
Kwa hali tulipofikia tunaomba kauli yako pamoja na kutupatia Waziri wa Mambo ya Ndani maana maisha ya hofu si mazuri.
Mungu turehemu Watanzania.
Sent using Jamii Forums mobile app