Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,864
- 155,822
Viongozi wa nchi, na viongozi wa CCM Mara nyingi wamesikika wakisema eti nchi yetu iko kwenye vita vya kiuchumi, ina pambana na mabeberu.
Huuu Ni utopolo daraja la Kwanza, unapambanaje na mbuzi? Kama mabeberu ni nchi hisani unapambanaje na anayekupa msosi?
Hebu fikiria uchumi wetu ulivyo, yaani choka mbaya, balance of trade hamna, tunanunua nje Kila kitu tunachokitumia, isipokuwa maji na chakula tu, halafu tunajinasibu eti tuna Vita.
Taifa hili linaongoza kwa kutokuwa na furaha. Usipokuwa na furaha ni kwamba una majonzi.
Ukikaa kwenye hali ya majonzi kwa muda mrefu, unaanza kuona kila mtu hakupendi, ndio tuonavyo, tunaona Rwanda hawatupendi, Kenya hawatupendi, Wazungu hawatupendi yaaani full wenge.
Hii sii Vita ya uchumi, Ni Vita ya kiroho.
Tunagombana na Yale tuyaonayo kwenye akili zetu.
Ndio maana mkuu kaminya Twitter, bila VPN hutoboi.
Ndio maana anasema anatamani malaika wazime mitandao.
Ndio maana anatamani nchi nzima tuwe CCM
Ndio maana anatamani yeye awe jaji, mwendesha mashitaka, Polisi, mchungaji, daktari, nesi, yaani kila kitu awe yeye. Kwasababu ndani yake hamna kutosheka. Hiyo Ni Vita ya kiroho.
Tanzania hatuna Corona, kaenda kuchukua mahela ya watu, kayatumia, kumbe wanamchora tu, Sasa wanamuuliza, hela zetu za Corona umefanyia Nini wakati kwenu hamna Corona? Hana majibu, hiyo sio Vita vya uchumi, Ni Vita vya kiroho, unasutwa na dhamira yako.
Watu wakipigwa risasi mchana kweupe, hujishughulishi kufanya uchunguzi, unaona is none of your business.
Ben Saanane kapotea, hujali, unaona poa tu
Azory kapotea, Wala huhangaiki
Maiti zinaokotwa kwenye mifuko mitoni na baharini, hujali.
Hii inaonyesha una roho gani, hiyo Ni Vita ya kiroho sio uchumi.
Unasema eti watu wanayatamani madini yetu. Mbona kipindi cha Nyerere hakukuwa na wachimbaji zaidi ya Williamson, hao mabeberu walipungukiwa Nini?
Dunia ikikosa tanzanite kwani itaathirika Nini?
Una Vita vya kiroho ndio maana kila siku unataka kuombewa.
Hamna kiongozi tangu Uhuru ameomba Mara nyingi zaidi aombewe isipokuwa wewe