Jamani kwa Mambo yanayoendelea bungeni hakuna haja ya kuendelea kuwa na Wabunge. Wanapoteza/wanafuja rasilimali za taifa bila Tija. Ni busara Mabaraza ya madiwani yakaimarishwa.
jamani hili mnaliona aje?
kwa kweli mimi kinachonishangaza pale mbunge anapochangia hoja kwanza kabla ya kuchangia anasema anaunga mkono hoja kwa 100% sasa sijui anachangia nini si bora akae tuu aache wenye hoja wachangie.
naunga mkono hoja bora wabunge 48 wa chadema kuliko 200 wa ccm
Tena hawa wabunge wa viti maalumu ndio wanaharibu kabisa umakini wa bunge, bora viti hivi vifutwe!!
Hilo nalo neno.Jamani kwa Mambo yanayoendelea bungeni hakuna haja ya kuendelea kuwa na Wabunge. Wanapoteza/wanafuja rasilimali za taifa bila Tija. Ni busara Mabaraza ya madiwani yakaimarishwa.
jamani hili mnaliona aje?
Hesabu ni tatizo la kitaifa nchi hii ndugu yangu. Inabidi hawa jamaa waelimishwe maana ya asilimia 100. Yaani kama unaunga mkono kwa asilimia mia moja ina maana hoja haina mawaa na haihitaji kuongezwa wala kupunguzwa.
Pendekezo lako ni zuri lakini halina chanzo...au sababu ya kufikiria hivyo...
Hivi mafanikio kwenye deliverables za mbunge yanaweza kupimwa kwa vigezo vipi?