TANZANIA HAINA KODI YA UNUNUZI (SALES TAX)
Kodi ya ununuzi hulipwa na mnunuaji wakati anaponunua kitu chochote ukiacha bidhaa chache zikiwemo dawa. Kodi hii hailipiki bila ya risiti. Kwenye hiyo picha ya risiti jamaa amenunua kahawa dola moja akalipa kodi ya ununuzi asilimia 6 ambayo ni senti sita. Muuzaji anakusanya hizo kodi mbili na kuzifikisha mamlaka ya kodi.
Tanzania kodi hii haitozwi kabisa. Kilicho karibu na kodi hiyo ni VAT. Kodi ya asilimia 18 ambayo wanachajiwa wasambazaji bidhaa ili wakipanga bei ya bidhaa zao wajilipe hiyo kodi ya asilimia 18 waliyokwishalipa.
Mfumo huu wa Tanzania una matatizo kadhaa yakiwemo yafuatayo.
Kwanza asilimia kumi na nane ni nyingi mno. Ni lazima wasambazaji bidhaa wataleta janja ya nyani wasilipe hiyo kodi.
Na wakiilipa itabidi waingize hiyo asilimia 18 kwenye bei ya bidhaa wanazouza kwa wateja hivyo kusababisha bei ya bidhaa kuwa juu sana.
Tatizo jingine ni mnunuzi kuwa gizani. Hajui kuwa muuzaji ameilipa hiyo kodi au ametoa rushwa na hakulipa chochote ingawaje anapandisha bei ya bidhaa kwa madai ya kuwa kazilipia kodi.
Vile vile kodi ya VAT hulipwa na wasambazaji wa bidhaa wenye leseni za biashara tu na hawako wengi .
Ushuru au malipo ya kutumia soko yasichanganywe na kodi ya ununuzi.
Long story short, ni kuwa kodi za Tanzania ni kubwa kwa sababu wanaolipishwa kodi ni wachache mno. Na wanabebeshwa mzigo wa kodi ys nchi nzima. Kodi ya kipato wanaolipa ni waajiriwa na waajiri wao. Wafanya biashara hulipa kodi za uingizaji bidhaa nchini na wasambazaji hulipa hii kodi ya VAT.
Consumers (watumiaji) hawalipi kodi yeyote na ndio walio wengi.
Kama kweli Tanzania inataka mabadiliko ifanye mabadiliko kwenye mfumo wake wa uchumi. Kubadilisha viongozi au chama tawala bila ya kubadilisha mfumo wa uchumi ni kutwanga maji ndani ya kinu.