comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr John Magufuli katika kuweka jiwe la msingi la reli ya kisasa katika hotuba yake alionge maneno fulani hivi muhimu sana kuyatafakari maneno hayo yalikua hivi "amani inaweza kuvurugwa na wachonganishi na mkichonganishwa mnaweza kugombana na mkigombana wale waliwachonganisha wanakaa pembeni kuwaangalia",
Kumekua na habari kadhaa kuhusu neno "utekaji" wa raia nchi, Kwanza tutofautishe hilo neno na kuhitajika kutoa ufafanuzi bila shuruti kwa vyombo vya dola, kwa vyovyote vile vyombo vya dola katika nchi yoyote haviwezi kufanya utekaji kwa raia wake, utekaji hufanywa kwa maadui wa Taifa ili kulinda wananchi wake, kuna minong'ono inayolitia Taifa aibu kuhusu uzushi na kulisakafia kwa sementi kali neno kutekwa kwa raia nchini ni aibu, kuitia doa na udhalilishaji kuitangazia nchi kwamba kuna utekaji wa raia wake, kimsingi mateka ni maadui wa Taifa letu mfano wapiganaji waasi na magaidi hao wanaweza kutekwa ili kulinda maslahi ya nchi yetu lakini mwanachi anaombwa kwaajili ya mahojiano kadhaa kwa jambo lolote lenye utata, katika hatua hiyo sio lazima anaekuhitaji kwa maelezo awe na sare za kazi ila kitambulisho kinatosha, aidha, inategemea utii wa sheria bila shuruti jambo ambalo vyombo vya dola kama jeshi letu la polisi linazidi kuhamasisha utii wa sheria bila shuruti
hivyo hatua hiyo sio utekaji
Maoni yangu-:
Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii tusikuze na kuongeza chumvi habari na maneno yenye ukakasi na tutofautishe maneno utekaji na kuhitajika kutoa maelezo bila shuruti maana inaitia doa Tanzania katika anga za kimataifa.
Comrade igwe