Haya angeyasema kule kule australia alipokuwa nao hao watoa hoja.....kuja kutueleza sisi huku haisaidii hata kidogo , alitakiwa asimame hadharani kupinga hoja hii lakini kule kule, ukute kule alikuwa mdogoo kama piritoni ametua hapa anajitutumua!
mix with yours
Watu wengine bana kwa hiyo wewe ujapenda Membe alivyosema?
Huruma hailei mwana,waache watuchunie ili serikali iweze kutumia akili kufikiri. Nalog offTumezidi kuwa kuomba omba na rasilimali tunazo kibao, ngoja tukomeshwe.
Mh Membe leo amekutana na waandishi wa habari kutujulisha yaliyojiri kwenye mkutano wa Jumuiya ya Madola uliofanyika huko Australia hivi karibuni. Mh Membe ametoa tamko dhidi ya kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Uingereza ya kutishia kusitisha misaada ya kiuchumi kwa nchi za Jumuiya ya Madola zinazopinga suala la mahusiano ya watu wa jinsia moja.
Mh Membe amesema Katiba ya nchi inatambua familia kwa maana ya mahusiano ya kijinsia kati ya mume na mke na si vinginevyo. Amesema pia jadi na utamaduni wa Watanzania unaruhusu uhusiano wa mwanaume na mwanamke tuu na si vinginevyo. Mh Membe amesema Tanzania haikubaliani kwa namna yoyote ile na kauli ya Cameron na kwamba tutakuwa tayari hata kujitoa kwenye Jumuiya ya Madola kama Uingereza itashinikiza Tanzania itambue mahusiano ya watu wa jinsia moja.
Haya angeyasema kule kule australia alipokuwa nao hao watoa hoja.....kuja kutueleza sisi huku haisaidii hata kidogo , alitakiwa asimame hadharani kupinga hoja hii lakini kule kule, ukute kule alikuwa mdogoo kama piritoni ametua hapa anajitutumua!
mix with yours
Nimesoma kwa mshtuko sana kauli za waziri mkuu wa Uingereza kulchanganya basic needs za maskini na kykubali mashoga
nina maswali mawili tu
1. Kwanini ushoga ahead of ufisadi?
2. Vipi wasianze wao na prince Harry aoe dume?
Kwani mtu anapopenda na kuamua kuwa shoga kunatatizo gani?Je kama mnasema Mungu amekataza kitu hicho nadhani mnatumia vitabu kama Quran na Biblia ambavyo ni mwongozo wa dini. Je Tanzania ni taifa la dini au vipi?Kama ni mambo yamakatazo ya dini yasiingilie privacy na haki ya mtu.
USHOGA SIO DHAMBI.
Ushoga Uingereza unaruhusiwa -na kisheria watu wa jinsia moja wanaruhusiwa kuoana. Mfano ni Sir Elton John.
Lakini bado mimi sijaelewa haya makelele yanatoka wapi? David Cameron katoa masharti kwa Matonya kwamba ukipeleka kibakuli basi sharti ukubali 'kuhalalisha' ushoga. Hutaki peleka bakuli lako kwingine. Very simple. After all hela anayowapa inatokana na kodi za watu wa huko wengine wakiwa mashoga.
Mnaacha wajanja wanawaibia madini, voda wanakwepa kodi lakini mnamsumbuwa Cameron kila siku mnaomba chakula. Sasa kawapa masharti- no such thing as free lunch!