Tanzania Garage Directory

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
53,104
53,341
Nadhani ingekuwa vyema tukiwa na directory inayoonesha garage ambazo members wanatumia na ikiwezekana weka namba ya simu ya fundi ambaye unamuona ni reliable.

Hii itawasaidia wengine wanaohitaji msaada wa ufundi au service endapo atakuwa hilo eneo.

Na pia ingekuwa vizuri kama ukisema huyo fundi amebobea upande upi zaidi.

Muongozo utakuwa hivi;
-Jina la Garage/jina la fundi
-Mahali anapopatikana
-Jina la fundi na namba ya simu
-Kitengo alichobobea mf, body works, electrical, paint, general service, diagnosis etc.
-Model ya gari kama itawezekana kama Subaru, European n.k

Hata mikoani ni sawa pia.

Nakumbuka nilishawahi haribikiwa na gari mwanza, nilipata shida sana kupata fundi..
 
Nilishawahi kuharibikiwa na gari Dodoma nikitoka Kigoma. Kuna fundi mzuri sana anaitwa Tall, anapatikana kwenye kituo cha mafuta Total iliyo karibu na njia ya kwenda Iringa, ukitokea barabara ya Mirembe Hospital. Alipiga general service, wheel balance na aligment. Nilikuwa na European car.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom