Tanzania fuateni nyayo myakomeshe mafisadi!

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,898
Hebu sikilizeni sasa maoni ya huyu Mtanzania anavyosema na wewe unasemaje ?
Huna haki ya ku-uwawa ila unastahili kushukuriwa kwa
kuufikisha ujumbe huu.

Watanzania hatustahili kuwaiga Wakenya kwa ajili ya
kuiga tu. Ila si vibaya tukaweza kusoma ni jinsi gani
tunaweza kubadili serikali yetu inapohitajika kufanya
hivyo ikiwa ni lazima.

Nimekwisha sema humu ukumbini na hii leo nasema tena.

Tulipopata serikali yetu mara ya kwanza kabisa, ilitulazimu
kwenda Lancaster House, kutengeneza KATIBA upya. Kwa
nini? Tulipotaka kuwa Jamhuri, tuliitengenezea KATIBA.
Kwa nini? Tulipoamua kuwa na serikali ya Chama kimoja
kutoka vyama vingi tulitengeneza KATIBA. Kwa nini? Na
hivi sasa, tumeamua kurudi kwenye mfumo wa vyama vingi
hatutaki, kata kata, kutengeneza KATIBA mpya, tumejiuliza,
KWA NINI?

KATIBA ni SHERIA MAMA inayompa mwananchi aliye HURU
nchini mwake, UHURU na HAKI zake kikamilifu. Hii KATIBA
yetu kama ilivyo inatoa uhuru na haki zaidi kwa Chama cha
Mapinduzi na wanaokiongoza. Madaraka anayopewa Rais
ambaye naye pia ndiye Mwenyekiti wa CCM ni makubwa na
pia ni mengi mno, kiasi cha kuashiria kuonekana kuwa nchi
yetu na serikali yetu ni mali ya CCM badala ya kuwa ni mali
ya wananchi wote bila ya kujali itikadi za za kisiasa. Kwa maoni
yangu, CCM na serikali hii, wanaitumia KATIBA hii kujisimika
katika uongozi wa serikali na nchi kwa jumla, milele na milele.

Kwa hiyo, nafikiri, katika kuwaiga Wakenya, Watanzania
hatuna budi kufikiri na kuweka sawa mikakati. Si suala la kuiga
tu. kwa ajili ya kuiga.

KATIBA ya vyama vingi ni lazima iwape uhuru wa kweli watu
wake. Kwa mfano leo hii nchini mwetu, wananchi wasiokuwa
wanachama wa Chama chochote cha kisiasa, hawana uhuru wa
kugombea uongozi katika ngazi yoyote katika nchi yao wenyewe.
Wananchi hawana uhuru wa kumchagua mtu yeyote katika uongozi
wa nchi yao wenyewe, ila mtu huyo awe amechaguliwa na Chama
kwanza. Mbunge hana ruhusa ya kuwawakilisha waliomchagua bali
ni lazima akiwakilishe Chama. Hana uhuru wa kubadilisha, kusahihisha,
kukosoa na kutengeneza upya kufuatana na mawazo ya waliomchagua.
Executive Branch, Bunge, Judiciary, National Election Commission,
na vyombo vyote vya dola ni rubber stamps za CHAMA TAWALA. Je,
ni kweli Watanzania wanaweza kuwaiga Wakenya, hata kama wanataka?

Vyama vya kisiasa vya ushindani havina uwezo wa kuungana. Kisheria,
naambiwa, wakitaka kufanya hivyo, ni lazima waunde chama kipya. Na
wakitaka wafanye hivyo, ndio kifo chao watakapotaka kukiandikisha
chama hicho kwa Muheshimiwa Tendwa. Wajaribu tuwaone, kama jasho
halitawatoka. Tanzania hakuna kutengeneza NARC wala ORANGE kwa
haraka haraka. Mahakama Kuu imeidhinisha wagombea binafsi, wako wapi?
Imeharamisha TAKRIMA, umeona kilichotokea wakati CCM yenyewe ilivyo-
ndesha chaguzi zake zenyewe ndani ya chama hicho?

Katika KUIGA hapana budi watu wakae chini, kufikiri, kupanga na kutenda.
La sivyo, tukae chonjo tuwashangilie na kuwapongeza wenzetu wa Kenya.

Inahitaji MOYO si BONGO peke yake.
 
Mkuu umenena,
Wananchi wamechoka na kukata tamaa, na hatimaye wakakubali kufuata upepo unapoelekea.

Kila kitu ni majaaliwa. Atakalopanga manani ndilo litakalokuwa!
(Kutokana na imani)
Tuungane na hao waliodhamilia kuliombea taifa ili mwenyezi atunusuru na kutupa ujasiri wa kufikia demokrasia ya kweli na kufanya mabadiliko kila pale panapohitajika.
 
Mkuu umenena,
Wananchi wamechoka na kukata tamaa, na hatimaye wakakubali kufuata upepo unapoelekea.

Kila kitu ni majaaliwa. Atakalopanga manani ndilo litakalokuwa!
(Kutokana na imani)
Tuungane na hao waliodhamilia kuliombea taifa ili mwenyezi atunusuru na kutupa ujasiri wa kufikia demokrasia ya kweli na kufanya mabadiliko kila pale panapohitajika.

Kasana kumbuka imani bila matendo imekufa!
 
Mimi naungana na hawa viongozi wa dini katika kutoa elimu kwa wadau kuhusu haki ya kumiliki mali asili. Watu wengi huwa tunakimbilia kwenye dini ili kupata faraja.
Kitu kinachotia hofu ni pale viongozi wetu hawa wanpokuwa vinyonga na kutoa matamko yanayokinzana kama JK kateuliwa na mungu, na the vice versa.

Kwa njia yoyote ile ni lazima tukazane kuwafikia wananchi wengi ili waweze kuamua mwelekeo wa taifa lao, na si kwa kuiga bali kwa dhamira yenye nia ya dhati.
 
Hatuna cha kuiga huko, ila tumejifunza kuondoa wezi wa kodi kwa kura, wataiba kura zenyewe! wezi wa kodi tuwashughulikie tu bila kujali 60mil za ruzuku au 40bil ya hazina, wote wanyang'anyi.
 
Mkuu umenena,
Wananchi wamechoka na kukata tamaa, na hatimaye wakakubali kufuata upepo unapoelekea.


Huu ndo ujinga wa Watanzania wanapokata tamaa na kufuata upepo wanafanya hivyo kwa faida ya nani???Hivi sasa sisi Watanzania tukikata tamaa tunategemea malaika washuke waje waturekebeshie mambo??
 
Ukiwa Kenya "Nyayo" si mambo ya Moi na KANU? Mfano is more like it unaweza kuingia Nairobberry ukasema Nyayo watu wakakugombania.
 
Back
Top Bottom