Tanzania External Deficit soaring! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania External Deficit soaring!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rev. Kishoka, Oct 9, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kila siku tunaambiwa mambo powa, kila kitu dole tupu! Uchumi unakuwa!Lakini madeni na matumizi yanaongezeka marudufu.

  Lini tutaacha kuteketea kiuchumi?

   
 2. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Rev. Kishoka,


  Hapa inabidi nicheke kidogo na sisi kumbe tunalima na kusafirisha kabisa agricultural products! najua mazao kama pamba, kahawa, mkonge na karafuu ilikuwa deal miaka ya nyuma sijui siku hizi ni vipi. Kama upungufu wa mvua umekuwa chanzo cha kushuka kwa ukulima tunafanya nini kuhakikisha hali hii hairudii? tunamkakati mzuri wowote wa kuwahamasisha wakulima kuona njia mbadala na sio kutegemea mvua tu, nani hasa anapaswa afanye hili?

  Kwa kujijibu haraka haraka ni jukumu letu wote kusaidiana katika kufanikisha maendeleo ya nchi yetu lakini kitu kinasikitisha figure nyingi kuhusu kukua kwa uchumi zinatengenezwa tu hasa kipindi cha serikali ya tatu.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,563
  Trophy Points: 280
  Bei ya dhahabu kwa ounce moja katika NYSE leo hii ni $907 pamoja na kuwa na rasilimali kubwa ya dhahabu ongezeko la bei ya dhahabu katika soko la dunia halitunufaishi Watanzania. Wanaonufaika na Barrick, rafiki yake Kikwete, Sinclair na mashareholders wa makampuni hayo. Katika mauzo ya dhahabu toka Tanzania yenye thamani ya $2.1 billioni kati ya mwaka 2001 na 2006 Tanzania tuliambulia $78 millioni tu, lakini Kikwete ambaye wakati wa kampeni zake alidai ataingalia upya miakataba hiyo yuko kimyaa na huu ni mwaka wa tatu tangu aingie madarakani hajafanya lolote na sijui kama atafanya lolote kuhusiana na mikataba hiyo isiyo na maslahi kwa Watanzania.

  Tungekuwa tunapata mapato yenye maslahi ya kutosha kutokana na dhahabu yetu tungeweza kupunguza kwa kiasi kikubwa hiyo trade deficit. Watanzania tulimchagua kwa kishindo Kikwete na kumwita mkombozi na wengine kuthubutu kumwita 'chaguo la mungu' kumbe kura za Watanzania zilipotea bure kwani waliyemchagua ni chaguo la mafisadi akina RA, Karamagi na kundi lao la wana mtandao na ahadi zake zote hakuna hata moja aliyoitekeleza anaendeleza usanii tu na uVDG.
   
 4. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  GM,

  Kisingizio cha mvua ni kila mwaka tangu El Nino ije!

  You have asked the right question, lini tutakuwa tunajiaandaa vema ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa?

  Je tumefanya utafiti pale SUA wa kuzalisha mbegu ambazo zinaweza kustahimili mvua kidogo?

  Je tumeboresha uzalishaji wa kilimo kwa kuongeza upandaji na uvunaji ili tuhimili miaka ya kiangaizi kikali?

  Naona hata kwenye Chakula, tumeongeza uagizaji, je tutaachana lini na kuagiza chakula? Je Big Five na Pemba haziwezi kuzalisha chakula cha kututosha Tanzania nzima na akiba ya kutosha miaka hata mitatu?

  Bubu,

  Hilo la dhahabu, tutaambiwa tunasubiri utafiti wa kamati kuchambua mapendekezo ya Tume ya Bomani!
   
 5. K

  Kudi Shauri Senior Member

  #5
  Oct 9, 2008
  Joined: Nov 1, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii ni ishara mbaya kuhusu uchumi wetu! In the past 10 years the in-flow of funds from donors has helped Tanzania to balance its books. With the current financial meltdown in the major donor countries it is likely that in-flow of resources from donor countries will be reduced to a trickle. This should start to be experienced from the first quarter of 2009. We have to start living within our means - especially the Government. Matumizi ya serikali ni lazima yapungue sana.

  Over the past 10 years nimekuwa na bahati ya ku-observe delegations za nchi nyingi za Africa kwenye mikutano ya kimataifa ya UN; AU; World Bank etc. In most cases Delegations from Africa Countries are the largest - at times 5 to 10 times the size of delegations from the more affluent and richer countries [Sweden; Denmark; UK; Singapore; China etc]. Na hata katika nchi za Kiafrika Delegations za Tanzania ni kubwa sana ukilinganisha na uchumi wetu. Mara nyingi unakuta size ya Tanzania Delegation ni mara 3 to 5 times the size of Delegations of much richer countries like Botswana; South Africa; Mauritius etc. I do not know how internally we can justify such trips - lakini kuna haja ya kupunguza drastically. Hata hao donors sidhani watatuelewa tunapopeleka bakuli la kuomba msaada!.

  We are in for hard times and I believe the Government owes it to Tanzanians to be frugal - and this should apply to everybody from the highest level!
   
 6. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2008
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wakati wa hali ngumu ya uchumi, wenzetu nchi zilizoendelea wanakata matumizi ya serikali. Sisi licha ya umasikini wetu, matumizi kila kukicha yanaongezeka, hii ikiwa ni pamoja na safari za kila kukicha, JK alivyoongeza idadi ya wizara, utitiri wa mashangingi n.k.

  Swali la kujiuliza ni moja tu, Hivi tokea JK ameingia madarakani, ni kitu gani alichoanzisha na kuboresha nchini??
   
 7. Mugizi

  Mugizi Member

  #7
  Oct 20, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Thanks Rev. Kishoka and others for sharing these insights.

  Nategemea kwamba with this financial crisis, bei ya dhahabu itaendelea kupanda. Sijui tumejipanga vipi kufaidika na hili?

  Uchambuzi hapo chini unachambua mikataba michache tuliyonayo na wawekezaji wa nje katika sekta ya madini? Vile vile nani anafuatilia na ku-regulate sekta ya wachimbaji wadogo-wadogo. Kuna tathmini yeyote iliyofanyika ili tujue kipato kachopaswa kupatikana kutokana na sekta hii na kama kweli kipato hiki kinapatikana na kama hakipatikani ni kwa nini?
   
 8. Mugizi

  Mugizi Member

  #8
  Oct 20, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nilisahau attachment.
   

  Attached Files:

 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Oct 20, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,009
  Trophy Points: 280
  kudi-shauri,mugizi,mwanakijiji,rev.kishoka,

  ..majuzi Kikwete alikuwa anajisifia sana kuhusu ongezeko la makusanyo ya kodi.

  ..sasa mimi nilidhani ukusanyaji kodi ungeenda sambamba na upunguzaji matumizi yasiyo ya lazima. pendekezo moja ni kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri na serikali.

  ..yaani Raisi anaelezea ongezeko la makusanyo ya kodi, bila kueleza fedha hizo zimekuwa invested wapi na kwa manufaa ya nani.

  NB:

  ..mimi nadhani hiyo mikataba tumeshaula wa chuya. uwezekano wa kuibadilisha without a long and a costly battle ni mdogo sana.

  ..kwanini basi strategically hatuanzishi viwanda vya ku-process hayo madini yetu?

  ..lile azimio la kwamba Tanzania hatutasafirisha un-process tanzanite limeishia wapi?
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Club ya mpira ya Yanga inaongoza ligi ya vodacom.....!!!
   
Loading...