Tanzania Economic Regulation Monitor 2018: The government is damaging the business environment

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Wakuu,

Ripoti hii inasambaa kwenye viwanja vya wanadiplomasia na wawekezaji na inatugonga kweli baadhi ya maeneo, ingawa maeneo mengine inatupa sifa nzuri.

Nashauri mkaisome na tujadiliane kama watafiti hawa walichoandika kina ukweli.

KWA UFUPI:

> Ripoti inaonyesha tangu 2015 hali yetu kiuchumi imeyumba na kutuponda kuwa tuna sera mbovu katika sekta ya biashara
> Ripoti inabainisha kuwa mfumuko wa bei umeshuka tangu 2015 ingawa mauzo ya nje yameporomoka kwa kasi huku manunuzi ya nje yakipanda
> Ripoti inatuchapa kwa kusema kuwa nchi kwa sasa ina mazingira na sera ambazo hazitabiriki kwa mwekezaji kitu ambacho wao wanaonyesha kuwa kinatisha wawekezaji
> Ripoti inadai kuwa viwango vyetu vya kodi viko juu kitu kinachoumiza wafanyabiashara wengi
> Ripoti inaongeza kuwa kuna kubambikiwa kesi na kutishwa endapo hutolipa au kutoa kitu kidogo
> Aidha, ripoti inasema benki nyingi zinapumulia mashine na tangu 2015 zinakiona cha moto
> Ripoti inasema ujenzi wa miundombinu umeshika kasi tangu 2017 dalili ambayo inatia moyo
> Wamegusia pia 'Presidential Orders' zinavyoonekana katika awamu ya tano
> Wanadai hali ya umasikini nchini Tanzania inatisha

Ndani utakutana na maneno kama haya:

‘… bureaucracy and corruption were still at an unacceptably high level in some agencies, thus frustrating investors"
 

Attachments

  • TERM-2018 (190530).pdf
    1.8 MB · Views: 48
... umasikini katika nchi hii unaongezeka kwa kasi ya mwanga! Tafsiri yake nini? Chama kitatawala milele!
 
Tanzania's government faces an enormous economic challenge. Since 2017, Tanzania's economy has experienced a steady decline as a result of rapacious government policies and, possibly well intentioned

The economic problems confronting Tanzania's government were discussed in different reports ,
all we know that the deterioration of our economy is rooted in the predatory policies of past Tanzania's governments and the misguided efforts in this of Magufuli ,

Britanicaa
 
britanicca,

Naona umesoma ripoti pia. Hawa jamaa wametuchambua hadi mtu inakuuma kujua ndivyo tunaonekana mbele za wageni
 
Pamoja na kukubaliana na yaliyomo, lakii mbona report haina details za muandaaji na mchapishaji kwenye hiyo cover page yake? Ni taasisi gani inayotoa report hii?
 
Back
Top Bottom