Tanzania E-Map

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,842
8,230
Ndugu zangu ninahitaji E-Map ya Tanzania,nijitahidi ku google ramani niliyopata haitoshelezi nahitaji ramani ya Tanzania ambayo inaonyesha mitaa na vijiji vyote vya Tanzania,kwa mfano nikibofya nikitaka kujua mtaa wa Mchamba wima huko Zanzibar niuone kwenye ramani,au nikibofya Nakapanya huko Songea niweze kujua Nakapanya ipo sehemu gani,pia nimetumia ramani kutoka Encarta napo hakuna kitu,hapo zamani niliambiwa nijaribu Takwimu lakini bei ilinikimbiza mwakajuzi walikuwa wanauza CD ya ramani ya Tanzania Tsh 100,000
Naomba aliyenayo tafadhali anidondoshea hapa jamvini
 
Tumia neno kama digital map kuna chuo kimoja marekani kina ramani hii nimesahau kiunganishi chake lakini ipo
 
Level hiyo ya detail sidhani kama utapata, Google ndo walijitahidi zaidi kwa ramani ya bongo.
 
-Takwimu huenda wakawa na na ramani inayokidhi mahitaji yako kufikia mwaka 2012... ukusanyaji wa data za kutengenza ramani ni zoezi lenye gharama kubwa sana(hela, muda vifaa,nguvu kazi)..tambua hilo. lakini ndo wana uwezo kwa kiasi kikubwa wa kukupa kle unachohitaji.

-Google wanajitahidi ila wamekaa kibiashara zaidi. Ni maeneo ya mijini tu ndo wameweka picha zenye resolution nzuri. Na wao wamezuia kusha hizo pcha(kwani ni gharama sana kuzinunua)

Tupeane taarifa zaidi kadri juhudi zako zinavoendelea.
 
Labda usubiri mwaka 2020 au 2030 nadhani hapo Tanzania Map with some street and region zitakuwa digitalized .

Lakini kwa sasa sidhani,Siamini hata wazo hilo lipo kwenye tume ya sayansi na technology.
 
Ndugu zangu ninahitaji E-Map ya Tanzania,nijitahidi ku google ramani niliyopata haitoshelezi nahitaji ramani ya Tanzania ambayo inaonyesha mitaa na vijiji vyote vya Tanzania,kwa mfano nikibofya nikitaka kujua mtaa wa Mchamba wima huko Zanzibar niuone kwenye ramani,au nikibofya Nakapanya huko Songea niweze kujua Nakapanya ipo sehemu gani,pia nimetumia ramani kutoka Encarta napo hakuna kitu,hapo zamani niliambiwa nijaribu Takwimu lakini bei ilinikimbiza mwakajuzi walikuwa wanauza CD ya ramani ya Tanzania Tsh 100,000
Naomba aliyenayo tafadhali anidondoshea hapa jamvini

Wasiliana tena na hao Takwimu, nakumbuka kuwa walikuwa na ramani hadi za kata na hivi sasa walikuwa wanashuka kuelekea ngazi ya vijiji haswa wanapojiandaa kutengeneza ramani ya sensa ijayo pamoja na mahitaji mengine kitaifa. Ni kazi kubwa na pia yakupasa kufahamu kuwa siku hizi nayo iko pia kibibiashara kwa upande mwingine. Kupata ramani yenye vijiji kwa 100,000 ni sawa na bure kabisa ukizingatia ngarama ya kukusanya hizo takwimu. Ukilipia ndio njia pia ya kuisaidia hii idara muhimu na kuifanya iweze kukusanya taarifu muhimu zaidi kwa ajili ya maendeleo yetu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom