Tanzania, DRC na Burundi zaanzisha utafiti ili kuliokoa Ziwa Tanganyika katika kupoteza maji yake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Katika kupambana na uharibifu wa mazingira katika ziwa Tanganyika, serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Burundi zinafanya tafiti katika bonde la Mto Congo ili kubaini athari zinazojitokeza na kuathiri uendelevu katika Ziwa Tanganyika ambalo linamwaga maji yake katika Mto huo jambo linalochangia kupungua kwa kina chake.

Akizungumzia hilo Katibu Mkuu wizara ya maji Kitila Mkumbo, amesema tafiti zilizofanyika zinaeleza kuwa ziwa Tanganyika linapungua kina chake kwa mita 0.8 ambapo mikakati iliyopo ni kuanzishwa kwa ujenzi wa uzio katika mto Rukuga utakaosaidia kuzuia kupungua kwa kina cha maji Ziwa Tanganyika.

Profesa Preksedis Macro ambaye ni mtafiti kiongozi Tanzania amesema utafiti huo utasaidia kutoa fursa za uwekezaji mkubwa katika miradi ya maendeleo ikiwemo nishati kupitia mto Congo na kuwa na matumizi sahihi ya maji na kuzingatia utunzaji wa mazingira.

Utafiti katika mto Congo unatekelezwa na watafiti wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, kwa kushirikiana na vyuo vikuu vya kimataifa kutoka Uingereza, Kinshasa, Congo DRC na Afrika kusini ambao ulianza tangu mwaka 2016 na unatarajia kukamilika mwaka 2020.
 
Back
Top Bottom