Tanzania doctor strike escalates on torture claims

JF siku zote umekuwa ni uwanja wa Chadema ukweli lazima tuuseme; sababu kubwa ya mapungufu ya vitendendea kazi kwenye hospitali za serikali ni wizi, wahusika wakubwa ni hawa madaktari na wafamisia; ajabu leo hii wameshika bango wakidai dawa na vitendea hamna; na wajiangaliea miongoni mwao wengi wao sio wakweli; upo ukweli vifaa vingi kwenye mahospitali ya serikali vinaharibiwa kwa makusudi ili wagonjwa waende kwenye hospitali za binafsi;inakuwaje vifaa vinavyoharibika ni vya hospitali za serikali tuu? Hizi ni hujuma za kisiasa dhidi ya serikali; inakuwaje mpaka leo hii hakuna kiongozi wa upinzani anayewasihi madaktari wasirudi kazini; kama wao wanamtetea mtanzania ni mtanzania yupi wanayemtetea? Sasa wananchi tunasema liwalo na liwe kama noma acha iwe noma; mitishamba bado tunayo.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Mkandara;
Nimekupata tatizo la madai ya madaktari halitokani MoU; wanapigania kuboreshwa kwa maslahi na huduma za afya, hotuba ya mh. Raisi Kikwete imeeleza wazi juhudi za serikali katika kufanikisha madai ya madaktari; mengi hatukuyajua mpaka baada ya hotuba Raisi, mimi nadhani viongozi wanaohusika na majadiliano walikuwa wanaonyeshana ubabe kuliko busara, kama Raisi angekuwa mstari wa mbele kupitia ofisi ya Raisi naamini huu mgogoro usingefikia hapa; imedhihirsha wazi mh. Pinda kazi hii ya usuluhishi imemshinda; inaonekana ndani ya mgomo huu kuna mashinikizo ya kisiasa; wapo wanasiasa wana agenda za siri suala linalipiganiwa si mil.3.5; mimi bado naunga mkono hoja zao ila ikiwa serikali inayafanyia kazi madai yao sababu ya kugoma ilikuwa ni nini? Namsubiri Dr. Mkopi aje na maelezo kama yapo; Mkandara sasa hivi nimeanza kuamini wanasisa wa upinzani wapo ndani ya sakata hili, hawa madaktari wanatumika kisiasa vuta subira utasikia mengi.

Chama
Gongo la Mboto DSM
Kuhusu vyama vya Upinzani kuhusika kusema kweli binafsi yangu sidhani kama kuna ukweli wowote maana Chadema kwa kupitia mbunge wetu Mnyika walijaribu kujihusisha na mgomo wa kwanza wakapigwa breki mapema na kusema wasiingilie hayawahusu. Sisi wote hapa tuliwaunga mkono tukaambiwa sii swala letu bali lao wao na wata deal na serikali lakini tuliposoma vipaumbele tukaweka mashaka swala hili linakopelekwa. Jambo la pili madaktari wengi nchini ni wana CCM wenyewe tena wengine tuko nao JF, Tweet na tunawasoma kwa hiyo sidhani kama vyama vya Upinzani vinahusika pengine ndani ya CCM yenyewe ndiko kunakotokea hatya madudu maana kuna power struggle within.

Binafsi yangu, madai ya madaktari ni ya msingi hata iwe kuhusu mshahara bora kulingana na profession yenyewe, sawa lakini kama hukupewa ni maamuzi gani watachukua? hapo ndipo mimi sikubaliani na maamuzi hayo..I mean kama leo wewe ukimfumania mkeo, hakuna mtu hatasema hilo halikuwa jambo baya sana, lakini maamuzi yako yanapofikia kumdhuru mwanamke au mwanamme ulomfumania hapo ndipo watu tunasema hapana maamuzi ya kuua mtu sii mazuri zipo njia za kufanya ikiwa ni pamoja na kumtalakia mkeo au jikate wewe waache wao wajione mabingwa wanawake wapo wengi. Lakini ajabu madaktari wanatupiga huku wakisema wakifukuzwa kazi wataenda nchi zinazolipa vizuri why msianze na kuondoka kwenda huko mnakodai mtalipwa vizuri?

Nimeisoma hiyo hotuba ya Rais na kati ya madai 10 ya madaktari utaona hakuna moja linatuhusu sisi walalahoi isipokuwa wao zaidi na ndio navyojua mimi toka siku ya kwanza... still wanayo haki ya kudai hata iwe swala moja tu. Lakini hapa JF tunapigwa tu changa la macho, ukweli unabakia kwamba madaktari wanajali zaidi maslahi yao kiasi kwamba hata ikibidi watu wafe basi watakufa.. Hapa ndio kuna unyama nisiokubaliana nao wala sii madai yao. Na ndio maana nikasema PR yao mbaya sana sijui ujana au nini, walianza vibaya na wanamalizia vibaya.. Kesi kama iko mahakamani ni kitu gani kiliwafanya wagome hata kabla ya hukumu na wakatae hata amri ya mahakama?.. Wameitwa na rais Ikulu hawakwenda yaani dejavu kama alivyogomewa Pinda mara ya pili.

Kuna utoto fulani fulani ktk jambo hili hasa kukomalia ongezeko la mshahara ambapo wizara ya Afya hutumia karibu asilimia 80 ya fungu lake ktk recurrent expenditure (asilimia 50 ni toka kwa wafadhili) leo tukiongeza mishahara yao hilo fungu la developmant litabakia na kiasi gani? pengine less tha 10% hapa utaboresha vipi mazingira na ununuzi wa vifaa?..Haya wanapodai tuache kununua mashangingi ili kuboresha mazingira ya kazi na vifaa inakuwaje hawa hawa madaktari wabunge wamepitisha bajeti mbovu kisha ktk madai yao wanadai wapewe mashangingi na posho badala ya kutanguliza kuboresha Emergience Medical Serivices kwa kununua ambulance zaidi?... Yaani upuuzi mkubwa unafanyika!
 
Mkandara;
Utakataa sana lakini hili lina mashinikizo ya kisiasa; uzalendo huu wa kumtetea mtanzania madaktari wameutoa wapi? Wao ndio vinara hawakupi huduma ya maana mpaka utoe rushwa? Sijui mara ya mwisho ulifika lini Muhimbili lakini ukweli ni rushwa tupu wahusika ni hao hao wazalendo madaktari wanaojifanya kutetea watanzania; isitoshe hao hao ndio wahusika wakubwa wa wizi wa dawa na vifaa kutoka hospitali za serikali; jiulize inakuwaje vinavyoharibika ni vifaa vya serikali? Hujuma ni nyingi hata CT scan kuharibika kwake ni hujuma ili wagonjwe waende hospitali za binafsi. Umeongelea suala Mnyika zile propaganda za kisiasa; mbona hakujitokeza Dr. Slaa au Mbowe kuwasihi warudi kazini ukitilia umuhimu wa taaluma yao? Wakigoma makuli bandarini meli hazitashusha mzigo ikibidi mzigo utarudishwa ulikotoka; Wanaojiita watetezi wa wanyonge wanahusika sana walinyamza kimya kutaka kujichukulia pointi za kisiasa; Mkandara dini inasema kumfamnia unatakiwa uwe na mashahidi tena uwakute wakiwa ndani ya tendo vinginevyo itakuwa ni dhana tu; kama madaktari wanataka washauri wa bajeti waingie kwenye siasa; tunachoomba wasitumie taaluma zao kuwaadhibu watanzania wa kawaida.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Back
Top Bottom