Tanzania: Disturbing Figures | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Disturbing Figures

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Jan 4, 2009.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Jan 4, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  (1) Tanzania ni kati ya nchi zenye watu wengi sana Afrika
  [​IMG]
  (2) Tanzania ni kati ya nchi zinzopewa sana misaada Afrika
  [​IMG]  (3) Tanzania ni kati ya nchi zenye kuchimba dhahabu sana duniani
  [​IMG]
  (4) Lakini Tanzani ni kati ya nchi maskini sana duniani
  [​IMG]


  (5) Tanzania pia ni kati ya nchi ambazo watoto wake wengi hufa wakati wa kuzaliwa.
  [​IMG]  (6) Vile vile Tanzania ni kati ya nchi zenye maambukizi mengi ya ukimwi duniani
  [​IMG]


  (7) Kinachonishangaza ni takwimu kuonyesha kuwa Tanzania si moja ya nchi ambazo watu wake hawana kazi. Yaani haimo kwenye list ifuatayo
  [​IMG]

  Je namba hizi zinaonyesha kuwa Watanzania tunapunjwa sana kwenye ajira kiasi kuwa pamoja na wengi wetu tuna kazi, lakini bado tu maskini?
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  From the figures, inaonyesha kuwa Tanzania ni nchi ambayo ufisadi ni mkubwa sana.
   
 3. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima yako mkuu; hizi data source yake wapi mkuu naona ina discrepancy sana na current data za Tanzania?

  Kwa mfano;
  - Population ya Tanzania sasa inakaribia au iko 40mil sio 36mil
  - GNI/capita $980 sio $800
  - Watoto wanaokufa kabla ya miaka mitano ni tofauti na infant mortality rate; infant mortality rate hata hivyo iko 74/1000 live births sio 100, ingawa underfive mortality iko 108/1000 live births
  - HIV prevalence rate kwa adults sio 8.8% ni 6.2%
  - Kutokuwepo kwenye highest rates of unemployment inategemeana na definition; wanasema Tanzania 80% ya population wako employed kwenye agriculture, kwa hiyo 20% inayobaki ukiigawanya gawanya kwenye sekta nyingine inawezekana kabisa unemployment rate ikawa ndogo sana.
   
 4. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na kuhusu population, inabidi kuangalia population density, kwani figure tu ya 40mil inaweza ikawa inamislead kama ukicompare na nchi nyingine- ukubwa wa nchi (eneo) ni muhimu kutilia manani.
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jan 4, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Mkuu Outlier ( I guess 3-sigma:))

  (a) Kuhusu idadi ya watu tunaangalia manpower siyo population density. Nchi yetu ina manpower kubwa kuliko nchi nyingi, kwa hiyo watu wetu kwa pamoja wanaweza kufanya mambo makubwa kuliko tufanyavyo unless ungeniambia kuwa tuna idadi kubwa ya watu wasioweza kufanya kazi.

  (b) Kuhusu discrepancies katika namba nyingine si tatizo kubwa sana, kwani inategemea takwimu hizo zilichukuliwa lini; nyingi zinatoka kwenye databank ya CIA ya mwaka 2007-2008. Hata hivyo angalia namba hizo relatively kwani kama GDP yetu imepanda kwa kiasi fulani, it is very likely kuwa GDP ya nchi nyingine pia ilipanda kwa kiasi fulani.
   
 6. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante kunielewesha- kwa hiyo itakuwa ni vizuri kutunyambulishia pia hiyo manpower/country- kwa Tanzania 50% ya watu 40mil wako <18 years of age, na perhaps 3-5% wako >65 years of age nadhani wanaobaki ndio tutawatumia kama population ambayo iko productive- ila sitaki kuleta mabishano, natamani tu tujadiliane tukiwa na indicators na data sahihi!
  Asante tena mkuu.
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Jan 4, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Hapa sijakuelewa vizuri unachotaka kuniambia.Kulingana na hili i swali ulilonilima hapo juu na hayo ya nyuma ninayaelewa kuwa:

  (a) Una hypothesis kuwa Tanzania inafanya vizuri tu, na takwimu hizi zinasema uwongo kabisa. Mimi ninadhani kuwa zina ukweli fulani ambao unasaidia kupima mwelekeo wa nchi kimaendeleo. Kwa ufupi, hali yetu ni mbaya sana pamoja na kuwa tunapata misaada sana, tuna raslimali nyingi, na tunauwezo wa kufanya kazi.

  (b) Kuhusu mgawanyo wa umri wa watu, unasema kuwa watanzania wengi ni watoto wasioweza kufanya kazi ukilinganisha na nchi nyingine. Mimi nadhani Tanzania mgawanyo wa umri Tanzania ni karibu sawa na nyingine nyingine za Afrika na sana sana Tanzania ina uwiano wa watu wengi wenye uwezo wa kufanya kazi kuliko nchi nyini za kiafrika. Ukitaka pitia hiyo databank ya CIA, utaona ukweli kuwa age distribution haitofautiani sana katika nchi nyingi za kiafrika. Nitakupa data chache kukusaidia kupima ukweli huu. Pima birth rate na death rate, utapata estimate nzuri ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi. Ukichukua assumption kuwa vifo haviko age-biased hasa kwa vile birth rate huondoa watoto wanaokufa wakati wa kuzaliwa (infant mortality rate), unaweza kutumia tofauti kati ya birth rate na death rate kuangalia ni nchi ipi inaweza kuwa watoto wengi kuliko watu wazima. Tofauti kubwa inaonyeshwa watoto wengi zaidi.


  Tanzania birth rate yetu ni 35.95 births/1,000 na death rate yetu ni 13.36 deaths/1,000 - tofauti ni 22.59/1000.

  Nigeria ambayo ndiyo yenye watu wengi kuliko zote Afrika ina birth rate ya 40.2 births/1,000 na death rate ya 16.68 deaths/1,000 --tofauti ni 23.52/1000

  Malawi ambayo ina watu wachache sana kuliko zote Afrika ina birth rate ya 42.09 births/1,000 na death rate ya 18.25 deaths/1,000 ---tofauti ni 23.84/1000

  Kenya majirani zetu wana birth rate ya 38.94 births/1,000 na death rate ya 10.95 deaths/1,000 - tofauti ni 27.99/1000

  Unaweza kutafuta distribution hiyo kwa Afrika nzima, utagundua kuwa Tanzania ni kati ya nchi zenye watu wengi wenye uwezo wa kufanya kazi kuliko nchi nyingi za Kiafrika.
   
 8. Companero

  Companero Platinum Member

  #8
  Jan 4, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kipembezoni (Outlier) hapo kitu muhimu ni mwelekeo (trend). Huo ndio mwelekeo wenyewe, hakuna mabadiliko makubwa hata ukileta hizo takwimu zako mpya. Uzito wa hoja za Anthill (Kichuguu) uko pale pale. Inakuwaje tunachimba sana dhahabu, tunapewa sana misaada, tupo wengi sana, tunafanya kazi sana lakini bado tu mkukuta/maskini?
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kichuguu, ebu jaribu (na mimi jajaribu) kutafuta corresponding data kutoka National Bureau of Statistics. Huwa ninapata shida sana kuhusiana na hawa watu wa nje wanavyo-compile data kuhusu Tanzania na nchi nyingine ambamo wao hawana operartions zao wazi wazi
   
 10. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Outlier,

  Inaelekea unajua takwimu nyingi sana za TZ. Tafadhali jaribu ku post kwa urefu sio kwa lengo la kubishana bali kufundishana. Pia unaweza kutusaidia kujua wapi tunaweza kupata hizo current data.

  Watu wengi hatuna hizo data na ndio lengo la JF kufundishana.

  Asante mwalimu Kichuguu kwa kuanzisha hii thread.
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Jan 4, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Nitajaribu kutafuta data hizo; hata hivyo tukubali kuwa sehemu kubwa ya data hizi za CIA ni sahihi kwa vile wao pia wanazipata kutoka serikalini kwetu au kwenye taasisi za umoja wa mataifa ambazo zina wawakilishi wao hapa nchini. Inawezekana kukawa na discrepancies ndogo ndogo hapa na pale au data zikawa zinachelewa kuwa-updated kulingana na jinsi wao wanavyozipata, lakini bado zinatufundisha ukweli mmoja kuwa trend yetu ni mbaya kama alivyodokea kifasaha ndugu Companero. Ni vizuri tukubaliane na hii negative report halafu tutafute namna ya kubadili mwelekeo wetu kivitendo kuliko kuikataa halafu tukaendelea kufanya mambo yetu vile vile (status quo.)
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  UKO NBS ukienda data ni za kitambo mno latest ni chache ebu soma iyo attachement.Isitoshe data hutegemea ni za lini.
  To me they are good indicative data and we need to work on our weakness kama twachimba zahabu nyingi,na kupewa misaada kila leo why are we not moving tumelogwa?
  View attachment TAKWIMU ZA AJIRA.pdf
   
 13. Companero

  Companero Platinum Member

  #13
  Jan 4, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Jan 4, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Data za kutoka umoja wa mataifa ziko hapa.


  2007/2008 Human Development Report - Tanzania (United Republic of) HDI Rank - 159


  Hizo ni zimetolewa na UNDP ambao wana ofisi yao Dar es Salaam na wanapata data hizo kutoka serikalini moja kwa moja. Kuna data nyingine ni za zamani kwa vile sisi wenyewe hatuna data mpya; ofisi yetu ya twakwimu iko slow sansa ndiyo maana hatuna sababu ya ku0question sana data za CIA.

  Spread sheet iko hapa chini

  Spread Sheet

  Book zima la HDI kwa dunia nzima liko hapal

  http://hdr.undp.org/en/media/HDR_20072008_EN_Complete.pdf
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Dk Shein anaiita hiyo kuwa ni vicious circle of poverty, ananifurahisha sana kwa terminology hiyo.

  Mkuu Kichuguu, shida yangu si data zenyewe, isipokuwa interpretation yake. nasema hivi kwa sababu source uliyoiquote inaweza kuwa iliamua kuweka data hizo tu kukidhi malengo yake fulani (labda kuna hoja wanaijenga na wanataka kuifanya ionekane kwua ni sahihi kwa kutumia data hizo).
  Generally, matumizi ya data ni vert tricky kwa sababu data za iana moja zinaweza kutumiwa na watu tiofauti kujenga hoja tfauti na zote zikaonekana kuwa zina mashiko kutokana na support kutoka wka data hizo hizo.
  lakini ukweli unabaki pale pale kuwa hali yetu si nzuri (kama data zinzvyoonyesha) lakini hali yetu ni mbaya kiasi hiki tunachokiona kupitia kwenye data hiz?
   
 16. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,721
  Likes Received: 1,212
  Trophy Points: 280
  Outlier umelala mbele? Ebu tuletee hizo takwimu za karibuni kabisa kuhusu Tanzania. Maana nami pia ninatumia hizo data za jamaa wa CIA fact book...
   
 17. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,721
  Likes Received: 1,212
  Trophy Points: 280
  Binafsi nasema hali yetu ni mbaya sana, pengine labda data za CIA zinaweza kutupendelea kwa kiasi fulani (kwa malengo wanaoyajua wao).
   
 18. P

  PanguPakavu Amy Senior Member

  #18
  Jan 4, 2009
  Joined: Jul 7, 2007
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  katika vi-3 vya sera za mwalimu,kuna viwili havipo!!UONGOZI BORA na SIASA SAFI!
  executive yetu ni one of the worst,na judiciary yetu is more like a joke.
  mifano tunayo.  nadhani wote tunajua misaada inakoenda!sio kwa wananchi,au kule inakotakiwa kwenda!
  misaada inaenda kwa viongozi na familia zao(wakiulizwa pesa wametoa wapi wanajiita Investors wa muda mrefu,wamefanya kazi majuu muda mrefu,wamesoma havard and such!!..sighs..,),inaenda kwenye vitu visivyokuwa na umuhimu(poor priorities)!kwa nchi masikini kwa level vitu kama Rada,BOT twin towers costing fortunes,700 new VXs!with thousands more on Gov payroll, nchi kumiliki shirika lake la ndege(huu ni ujima/ukomunisti/prestige),$60m for national Stadium(washabiki wa Mpira mnisamehe..,we just didn't need such an expensive stadium..,but rather that sum of money could fund a national Spots facilities and projects overhaul-from grassroots level!najua wengi tutabisha BUT again we have too much pride,bad trend for a poor person/nation)...etc!!
  kama wangepima misaada/loans/funds given versus actual misaada/loans/funds serving the purpose tungekuwa one of the worst perfomers!
  muhimu kuliko vyote,MISAADA haiendelezi nchi yoyote ile duniani.so we are pretty much on the wrong track

  kama tunaambulia 3% ya faida,na hiyohiyo kina mramba na wenzie wanataka 1.9%.ka 1.1% kanaenda hazina,kina gray mgonja wanakatafuna weeee,kasehemu kaliko baki tunashare wadanganyika wooooote - 40million.
  oh yeah!!where else could we be??!we deserve that spot!it's like having a 72-10 NBA season!that's got to be a championship team aayt?!
  we are champions of our own poverty!we create it,we share it we preserve it,and we have no plan to get out of it.And if you have a plan,no one lets you execute it.it should be this way for peace(that's what they say).namaanisha what the hell is CCM doing after nearly 50 years since independence?!it's very obvious the fellas have no plan whatsoever,i could imagine the greatest challenge of our president should be planning his calender,for he travels a lot and recite those monthly speeches.
  a nation with characters of ours should be poor.or more than that..,

  kwa sababu,zile Hela kutoka UNDP kwa ajili ya zahanati,zinaliwa..,zinazofika na kujenga zahanati,madaktari hakuna(wengi hawakumaliza MUCHS(migomo etc)-waliomaliza hawataki kufanya kazi njombe,wale wazoefu wako Bungeni!!my god)
  inshort,kutokufa wakati ukizaliwa is more of a fluke..,majaaliwa ya mungu,we say that in swahili.

  You guessed it,fedha chafu,Rushwa,wizi na ufisadi hupelekea kwenye matumizi machafu.nyumba ndogo,umalaya na mengineyo mengi.
  ukosefu wa elimu husababaisha wasichana wadogo kurubuniwa na mizee yenye hela chafu kufanya vitendo viovu.
  kama zile hela za misaada zingefika mashuleni,watotot wakaenda sekondari,vyuoni au kuweza kujiajiri wenyewe kasi ya maambukizi ingepungua.


  Ukweli ni kuwa Nchi yetu haina Data especially online!!if you are interested in Valuable Data from Tanzania you will be suprised!none!!kama zipo zinaozea kwenye mafile!!ndio sababu kubwa ya kuonesha watanzania wengi wanakazi.
  ukweli ni kuwa wengi hawana.hiyo kusema 80% ya working population wanajishughulisha na kilimo si sahihi!!
  as i know familia nyingi vijijini kina mama ndio hufanya kazi za kilimo.mizee hukalia kahawa,na pombe tu!
  still hiyo 80% do not work all the year!it is more of a seasonal occupation thing(sijui hii wanaichukuliaje).
  mbaya ni kuwa wengi wenye kazi hawafanyi kazi ipasavyo!maofisi ya serikali wamekalia soga tu!
  kufika kazini saa 4 kuondoka saa 8!!lunch brake includedhapo kuna kazi kweli?!

  ofcourse wachache wenye kazi wanapunjwa ipasavyo!!na mizigo wanayobeba ni mikubwa!!mishahara midogo,kusomesha watoto,gharama za juu za matibabu,gharama za juu za maisha....,


  tuna matatizo mengi sana.na Hatuna watu wenye wenye nia ya dhati ya kuyapunguza au kuyamaliza!
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Jan 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kichuguu,
  Sahihisho dogo tu, Pale kwenye nchi zinazochimba dhahabu, Tanzania imewekwa nafasi ile kwa sababu mwandishi alifuata alphabetical order..Hivyo, Tanzania ni nchi ya tatu Afrika na kama sikosei nchi ya Tano duniani..
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,596
  Likes Received: 82,153
  Trophy Points: 280
  Hili la kuendelea kuwa maskini pamoja na misaada mingi na kuwa moja ya nchi duniani ambazo zina rasilimali kubwa linachangiwa sana na gharama kubwa za uendeshaji wa serikali yetu ambazo haziongezi chochote katika kuinua kipato cha Watanzania walio wengi na hatimaye maendeleo , ufisadi na kuzigawa bure rasilimali zetu kama Tanzanite, Dhahabu, Almasi na muda si mrefu Uranium ambayo ina bei kubwa katika soko la dunia nayo tutaigawa bure na kutochangia lolote kwenye maendeleo ya Tanzania.

  Hapa wa kulaumiwa kuotokana na kudumaa kwa maendeleo ya nchi yetu ni viongozi.
   
Loading...