Tanzania Diaspora in USA inamwakilisha nani?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Diaspora in USA inamwakilisha nani??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Aug 13, 2009.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,108
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mikutano inayoandaliwa ya Diaspora imejaa wazee lakini jumuiya ya USA ni ya vijana. Haina maana tunabagua wazee lakini wazee na serikali hawajasaidia hawa vijana kwa miaka yote iliyopita na sasa wanataka kujifanya wanaweza kuwakilisha hawa vijana.

  1. Wazee na serikali hawajui matatizo ya uhamiaji
  2. Wazee na serikali hawajui watu wanaishi vipi kila siku
  3. Wazee na serikali hawasaidii matatizo yapotokea. Wazee wanakimbia na serikali inasema haina pesa
  4. Wazee na serikali hawana uchungu wa kuishi mbali na familia. Wazee wamehamia huku na familia zao miaka mingi na serikali hawanashida wako Tanzania.
  5. Wazee na serikali hawajui ugumu wa kwenda shule. Wazee wengi wamesomeshwa na serikali na serikali haijui shida.

  Hamuezi kuanzisha diaspora ambayo haina vijana kwani vijana na wazee wa marekani ni vitu viwili tofauti. Diaspora ya kweli ni lazima iwe na vijana wengi kulizo wazee wanaotaka kukutana na kuweka mikakati ya ufisadi. Mikutano hii ilileta Richmond.

  Mkutano unafanyika Houston lakini Watanzania wa Houston hawajaalikwa, kama tatizo ni ukumbi wangesema!! lakini hawataki Serikali ikutane na vijana wanao wakilisha watu wengi waishio marekali kwasababu watazuia muda wa kujadili mikakati na miradi binafsi. Kuna wazee wengi wamesikitika kupoteza nafasi kwani Gire wa Richmond alitumia mikutano kama hii kumzoea Nyanganyi na kuchukua line za ufisadi Tanzania. Diaspora ya USA si ya Watanzania waishio hapa USA ni ya watu wachache wanaotafuta miradi ya kifisadi Tanzania na Raisi usije kwenye hili utaondoka na skendo.
   
 2. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160

  Matatizo ya uhamiaji yanahusiana vipi na mkutano wa Diaspora ? Vitu vingi uliyosema hapo juu havina uhusiano wowote na huo mkutano , tafadhali moderator peleka hii kwenye kunako stahili.
   
 3. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Mabox hayo kaka. Ukichoka kila unachowaza unaandika tu!

  Mwisho atasema NO country for old men kisha aanze kuwamaliza kama kwenye hiyo movie.
   
 4. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,108
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Je nyie ni vijana mnaokaa USA au mnaropoka tu? Kama Diaspora haiwakilishi Wengi je inamwakilisha nani??. Kama hukai USA na si kijana vitu vingi hapa hutavielewa lakini kama Diaspora haiwakilishi watu haina maana kwani ubalozi upo.
   
 5. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,108
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Kuna watu wako bongo wanajidanganya vijana wa huku wanafanya kazi za mabox tu cha kujiuliza ni kwanini hawarudi??. Hutuhitaji visa kwenda bongo kwasababu tunapeta na maneno hayatasaidia familia wala kipato kila mtu anatakiwa kufanya maamuzi yake mwenyewe. Diaspora ilivyo pangwa sasa ni kupoteza muda na ufisadi tu
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Unanivunja mbavu hapa mwanangu....
   
 7. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Ahahaa Bluray, inaboa kamanda. UBAGUZI sio wa rangi tu. Wao wakiitwa manyani na wazungu wanalalamika.

  Ila wao wanawabagua wazee!!
   
 8. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  @Kamundu....pole sana mzee...naona hata baada ya kubeba box kwa miaka kadhaa umeshindwa ku-raise pesa ya kwenda kuona wazazi nyumbani.Katika hali hii lazima huwe na msongo wa mawazo.

  Yaani huamini kinachofanywa na watanzania wenzako kwa nini?...hii si platform ya kulalamika...u need to be objective...sawa?Cha kufanya ni kuhakikisha unapata nafasi ya kushiriki...gharama ya ushiriki ni ndogo ukilinganisha na pesa unayotumia kujaribu kuishi fake...shiriki halafu utoe mawazo yako kwenye tukio...
   
 9. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2009
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Huu ni uvivu tuu wa kufikiri , matatizo ya uhamiaji hayatatuliwa na mkutano huo wa Diaspora. Nakushauri ndugu Kamundu kaa na wenzako uwaulize wanafanyaje . Vile vile sio kazi ya wazee kuangalia watu wanaishi vipi , ni lazima utambue ya kuwa katika nchi za magharibi mtu unatakiwa uwe independent . Tatizo naona huko Marekani lakini mindset yako bado aijabadilika. Kitu kikubwa ninachoweza kuinfer kutoka kwenye email yako ni chuki yako juu wa wazee! However, you are making a colossal mistake by equating your failures with wazee. You hatred will only be good for sometime (temporary solution) ;because, the so called wazee have got nothing to do with your predicament.
   
 10. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,108
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Naona hii topic mnataka kuegeuza iwe kuhusu mimi!

  Mimi sijisifu lakini nimebahatika kupata degree yangu, ninakazi nzuri, nasaidia ndugu na jamaa. Sina shida ya kusafiri na nina passport ya marekani. Mimi mungu kanisaidia nitaishi vizuri tu pamoja na familia yangu hivyo mimi sio story hapa. Unaweza kunipiga madongo sita kutukana wala kukujibu vibaya kwani tabia nyingine ni ngumu kubadilika. Watu wengi hapa ni watu wazuri lakini wameweka tabia za malumbano na madongo ambayo kwa wakati mwingine hajasaidii jamii.

  Tatizo naloliona kwenye jamii yetu ya Watanzania popote tulipo ni ushabiki. Watanzania wengi wamekuwa si watu makini, tumekuwa watu wa kujaribu kupigana madongo, kuwekana chini, kubishana na kutafuta sababu za kushabikia.Mimi ningefurahi kama ningeona kwa wakati mwengine Watanzania badala ya kulumbana tufikirie ni kitu gani tutafanya kusaidia jamii yetu huko nyumbani na huku nje. Watanzania wenzetu wanaishi kwa shida watoto hawana madawati shuleni, familia hazina maji safi na kuwaletea watoto magonjwa yanayotokana na maji machafu hivyo ndugu zangu tupunguze malumbano.

  Kuhusu Diaspora, Balozi alishafanya mkutano wa Diaspora Houston 2007 au 2008 na kuna watu walitoka Tanzania mfano Musiba. Hakuna chochote kilichofanyika ukiacha kupanga tarehe za mikutano ya mbele. Hakuna mtu anayeamini kwamba ubalozi unaweza ku manage diaspora wakati hata kuwatumia watu passport inawasumbua. Huu ni wakati wa vijana kuchukua nafasi za uongozi kwasababu ukweli ni kwamba wazee wamepitwa na wakati hatuwezi kufanya mikutano nenda rudi bila matokeo. Hili jambo na Wazee ni kwa Diaspora pekee bali hata nchi yetu ya Tanzania.

  Sitajibu tena lakini nilifiki ni lazima niweke hili wazi na ndiyo maana napenda mtandao
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Aug 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kamundu,
  Mkuu wangu punguza jazba kidogo pamoja na kwamba umevamiwa...Swala hapa ni fikra zipi ambazo wewe unaweza kuchagia tofauti na hao wazee.. mifano mmoja ungeweza sana kutusaidia lakini ukichukua swala zima na ukawajumuisha wazee wote nadhani ndipo utata ulipotokea.
  Wapo vijana wengi sana ktk serikali ya sasa na hakika naweza sema hakuna wakati mambo yamekwenda hovyo hovyo kama wakati huu na kibaya zaidi ni kwamba vijana wanawaogopa kuwawajibisha wazee hao hao Mafisadi.

  Inawezekana kuwa ni mila au hulka yetu kuogopa wazee tukifikiria kuwa ndio heshima, lakini ndio ukweli wenyewe na wazee hutumia nafasi kama hizi. Pia usisahau kwamba bado tunafikiria au kuheshimu umri wa mtu zaidi ya uwezo wa mtu kufikiria ktk kutoa maamuzi..kwa nini hata sifahamu zaidi ya kukisia kwamba Umri ni moja ya upana wa exposure ya mtu mweusi maanake hatuna cha kutazama zaidi ya maisha yetu wenyewe..

  Ukichanganya yote haya bila shaka utaelewa kwamba inabidi vijana mchukue nguvu zaidi ya kulalamika kuweza kupenyeza ktk mfumo wetu. Na nadhani jambo zuri sana ulitakiwa kufanya ni kuwaingilia wazee ktk mkutano huo na ukaeleza wasiwasi yako..Pia ungeweza kuelewa uvivu wao wa kufikiri toka mkutano huo ukatuwekea hapa agenda za kikao hicho.
  Nakuelewa sana unachotaka kuelezea hapa kwani sisi wadanganyika siku zote hugombea TITTLE..Hiyo tittle mkuu wangu huwezi kupewa na mtu mweusi kirahisi kwani wazungu (Waingereza) walisema wakati wa vita vya Mau Mau...Mnyime Mjaluo mshahara lakini mpe tai yake ataridhika, lakini sii MauMau.Hivyo point yako hapa umesimama kama Mkikuyu ukiwatazama Wajaluo wanajisifia kwa tai zao shingoni bila kujua kwamba wanatumiwa na mzungu..Ni ukweli usiopingika lakini kwa Mjaluo hayo ni matusi ya nguoni!
   
 12. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,108
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mkandara labda bongo lakini hapa USA wazee wengi ni loosers! hakuna busara wala chochote kutoka kwa wazee. Misiba inayotokea hapa wazee umewahi kuwasikia hata wakitoa maneno ya busara?? USA siyo bongo kama huonyeshi results huna deal unajua hilo Mkandara.
   
 13. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kamundu;

  Unapowakilisha hoja usiweke ubaguzi. ungesema sio vizuri kushirikisha kundi fulani tu. Lazima makundi yote yashirikishwe!.

  Kwanini haurudi kuona wazee? Nauli? LOL unachekesha kweli!
   
 14. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2009
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Watu wengi wanaomrushia madongo "Kamundu" hawajamuelewa.....lakini pia...sio rahisi kuwaelewesha "kamundu" anamaanisha kwasababu wao tayari wameshajifungia ndani ya wimbi lao la maamuzi.
  Hata nikijaribu kuwaelewesha itakuwa kazi bure.
  Mkuu Kamundu...mimi nimekuelewa .... na ndio maana Tanzania Ufisadi unakomaa na maendeleo yamekuwa "finyu".
   
 15. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Mkuu Rodelite Sidhani kama wote wanaompinga Mh.Kamundu hawajamuelewa,Nafikiri Kamundu amekuja na statement kali na baadaye mwenyewe kashindwa kuitetea,Mimi binafsi kwa sehemu kubwa nakubaliana na Kamundu kuwa kuna Tatizo katika kuuanzisha huu Umoja wa Watanzania - USA.Tatizo ninaloliona Mimi ni muitikio wa hili suala....Kumekuwa na Juhudi kubwa kwa karibu miaka minne sasa,kujaribu kuanzisha Organization itakayowaunganisha Watanzania wote Nchini Marekani....nakumbuka Juhudi hizi zilianzia huko New York kwanza,Lakini kukawa na Migongano kati ya Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania wa New York na kamati ya Watu walioanzisha huo Umoja.Lakini baadaye kulitokea kutokuelewana na hakukuwa tena na muendelezo wa Jumuiya hiyo.

  Alipokuja Balozi Sefue mwaka juzi,kukaanza tena Juhudi za Makusudi za kuanzisha Jumuiya hiyo tena,na safari hii ikaonekana kuna baraka kutoka Ubalozini na MOFA (nyumbani) ambako kuna fununu kuwa kuna Desk Officer anayeshughulikia Jumuiya za Kitanzania Nje.Mwaka jana kulikutana baadhi ya Watanzania na Balozi huko Houston,na Maazimio ya hiyo Kamati ya Mpito ilikuwa kuwasiliana na Jumuiya mbalimbali za Watanzania na mtu mmoja mmoja ili kufanikisha kuundwa kwa Umoja huo,nafikiri zoezi hilo ndio limekuwa gumu,na matokeo yake,kamati inayoshughulikia hili suala imechagua baadhi ya watu wa kuanzisha Umoja huo....Mimi binafsi ninakuwa briefied nini kinachoendelea,lakini sifahamu kwa dhati mawasiliano ya Kamati hii na watanzania wengine yanafanywa kwa Mtindo gani? Kwa sababu kuna Vyama vya watanzania pia hawalifahamu hili.....wanaona Matangazo kama sio kwenye Michuzi Blog basi ni hapa Jamii Forum.

  Ninaiamini timu nzima ya Mpito katika suala hili ambayo ina wanachama 16 kutoka sehemu mbalimbali za Marekani na umri tofauti,nakuomba Ndg Kamundu wasiliana na Katibu wa muda Ndg. Nkunga na panapo uwezekano uwakilishe malalamiko yako kwao,na ni vyema ujipe muda ili panapo uwezekano uhudhurie Uzinduzi wa Jumuiya hiyo kama ilivyoelezwa katika matangazo yao.......Dicota haina uhusiano wowote na wazee wa Houston,kama vijana watajitokeza kwa wingi ni wazi watachaguliwa kuongoza Umoja huo.

  Tuendelee kujadiliana kama kuna mengine mengi yanayohusu uanzishwaji wa Jumuiya hiyo.Hayo masuala yanaanzishwa kwa Manufaa ya Watanzania wote na sio miradi ya Kifisadi ya watu...Tukijumuika wengi itakuwa rahisi kukosoana na kurekebishana pale penye kasoro......Kususia na kulalamika bila kutafuta Ufumbuzi sidhani kama kuna nafasi katika Jamii iliyostaarabika!
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Huu mjadala inaelekea una mantiki..lakini labda Kamundu angeweka bayana definition yake ya "WAZEE" maana kama ni masuala ya deals za UFISADI sidhani the so called vijana wamepitiwa mbali.Vijana wengi sasa hivi ndio wanaoonekana hawana tena maadili na ndio wanaofanya mambo ya ajabu hata ya kudidimiza jamii.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,547
  Likes Received: 18,205
  Trophy Points: 280
  View attachment 566354

  [​IMG]
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.
  [​IMG]
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.
  [​IMG]
  Mkurugenzi wa PPR Pascal Mayalla akiuliza suali katika mkutano na waandishi wa habari uliozungumzia Kongamano la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar.
  [​IMG]
  Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi Bi. Adila Hilali Vuai akijibu masuali yaliyoulizwa na wandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano la kitafa litalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. (kushoto) Muandishi wa habari Rahma Suleiman wa Chuchu Fm Redio.
  Picha na Makame Mshenga.
  Wanabodi.

  Declaration of interest. Japo mimi Paskali Mayalla sio mwana Diaspora, bali nimewahi kuishi nje kwa muda mfupi mfupi katika nchi mbalimbali, na nimewahi kufanya kazi tena sio kubeba box, bali kubeba zege ndani ya jiji la London, hivyo nina mwanga kidogo kuhusu diaspora, ila kwenye hili
  Kongamano la Nne la Diaspora, litakalo fanyika Zanzibar, tarehe 23 na 24 Agosti, I have a role to play.

  Hivyo hili ni bandiko la kuomba ushirikiano wenu, kwa ushiriki wako kwenye kongamano hili, physically or by proxy, ili kutoa mawazo yako Tanzania ikusaidiaje ili kukuwezesha wewe kuisaidia nchi yako.

  Tanzania itajengwa na Watanzania wote wakiwemo wana diaspora. Kitu cha kwanza ni kuomba ushiriki wako physically kwa wale wenye nafasi to make it home, wajisajili kupitia
  DIASPORA: Home Page
  or
  4TH Tanzania Diaspora Conference 2017 - Diaspora and SMEs ...

  Kwa wale ambao hawatapata nafasi ya kuwepo physically, wanaweza kushiriki by proxy, kwa vile dunia sasa ni kijiji kimoja, wanaweza kushiriki by proxy.

  Kwanza The Official Opening ya Kongamano lenyewe litatangazwa live za TV za Tanzania. Pili tutatangaza live kupitia video streaming kwenye youtube hivyo wana diaspora wote wenye nafasi wanaweza kufuatilia kupitia youtube, facebook, tweeter na mitandao ya kijamii.

  Hapa naomba ushirikiano wako tujadiliane how to reach you out ili tupate maoni na mawazo yako, Tanzania ikusaidiaje wewe mwana Diaspora ili uweze kuisaidia nchi yako?.

  Uzalendo sio kujiuliza "Tanzania Ikusaidie nini, bali ni wewe kujiuliza jee nimeisaidia nini nchi yangu Tanzania?". Kwa vile wana diaspora wengi wako nchi za nje na wamepata bahati ya kupata exposure kubwa, tunaomba mawazo yenu, Tanzania iwasaidieje ili muweze kuisaidia nchi yako Tanzania.

  Natanguliza Shukrani.

  Pascal Mayalla
  +255 784 270403
  pascomayalla@gmail.com
   
Loading...