Tanzania demokrasia yetu hakuna wa kutulinganisha nae Afrika!

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
14,089
15,933
Tanzania ni nchi ambayo kwa Africa bado huwezi kuilinganisha na nchi yeyote kuhusu demokrasia na uhuru wa kujieleza Tanzania bado huwezi kuilinganisha na Rwanda,Burundi,Uganda,Zimbwabwe,Zambia,Misri,Mozambiq na Kenya hii ambayo kwa hapa kwetu tunaiona ni mfano bado haupo huru kama kuweza kuishutumu wazi wazi Serikali na bado ukawa unaangaliwa

Tanzania wanapolalamika demokrasia ,mtu yupo huru kusema serikali ndio imetaka kuua au inafanya mauji,serikali inanitafuta na bado ukawa unaranda mtaani na hata gerezani hujafika zaidi ya kuhojiwa na kuachiwa au kamati ya maadili ya bunge.

Ulizeni uhuru wa kujieleza kwa mtu kama Dhlakhama wa Renamo Mozambiq,Shangirai,mpinzani wa Rwanda na nchi nyingine na hawa kama wangekuwepo Tanzania na wanavyojua siasa ya upinzani basi wangeshakua watawala,hapa wanapolalamika nilichogundua watu wanataka demokrasia ya matusi kuitukana serikali nzima kuanzia Rais mpaka mkuu wa wilaya matusi ya nguoni na familia yake ndio waseme wana uhuru wa kujieleza na demokrasia.

Hii ya kutamba na kusema maneno yote na kuishia na kwenda kulala majumbani familia zao wanaona haitoshi,bado watu wapo huru kuahidi watapambana na jeshi,watu wapo huru kuita media na kueleza ya moyoni na bado mkawa huru ni nchi gani yenye kuvumilia hayo zaidi ya hapa kwetu!

Tufanyeni kazi demokrasia mnayoitaka ya kumtukana rais nchi yeyote hairusiwi!

SIASA MPAKA 2020
 
hamna upinzani wa Tanzania hupo kwenye system ukitoka kwenye system hiyo ukajifanya mpinzani kweli basi utaona utakacho kipata
 
Mkuu unayowaeleza wanayaelewa kabisa.
Wanafahamu fika kwamba kwa aina ya siasa zao wasingekuwa hai isipokuwa Tanzania.

Ila wao wanajitafutia visababu vya kutumia kama Sera/hoja kwa ajili ya kuburuza wazungusha mikono.
 
Na weye acha ujinga. Kwa nini mnashika bunduki? Jibu kwa akili laa sivyo utajuta.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Naona unahalalisha upuuzi kwa kulinganisha na vinchi vichache vinavyotawaliwa kibashite. Yanayoendelea Rwanda na Burundi si kigezo cha haki za watz kuminywa.

Tunatumia katiba yetu si za kwao, na wao wakikiuka katiba zao si kigezo cha sisi kukiuka katiba yetu. Katiba yenyewe mbovu lakini bado mnaona inawabana tu! Kweli BBM...
 
Kilichominywa hapa ni kumshambulia mtu binafsi na matusi mengine sema utakayo!
 
Back
Top Bottom