Kutokana na mivutano ninayoiona kwa sasa, naamini serikali ya chama kimoja itatawala kwa shida sana, kutakuwa na hujuma mbalimbali toka vyama vingine kama inavyotokea sasa. Watanzania lengo ni maendeleo na kuboresha hali ya maisha yetu sio malumbano ya kisiasa na kuchafuana. Ikiwa serikali ya Mseto basi tutakuwa na sera aina moja ambazo zitatakiwa kufanikishwa. Wabunge wataweza kuwa na nguvu ya kuhoji mambo mbalimbali kwa uhakika zaidi hakuna kuogopa kufukuzwa uanachama wala nini. Mawaziri watachaguliwa kwa uwezo wao sio uswaiba. Naangalia wabunge wa CDM sioni waziri CCM ndio hao wanaovurunda. Pia mawaziri wachaguliwe na bunge kulingana na uwezo wao na wafanyiwe-open interview. Bunge litakuwa na uwezo wa kuwawajibishi sio kama ilivyo sasa.