Tanzania Daima vipi leo?

Mbalinga

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
1,714
1,370
Wapendwa wana jf, nimepita kwenye mitaa kadhaa ya Dar kutafuta gazeti nilipendalo la Tanzania Daima bila mafanikio. Kila ukiuliza wauzaji wanasema leo halijatoka. Kulikoni? walio karibu na Freemedia watujuze kinachoendelea. Ama ndio magamba wameleta fitina zao kwani leo na kesho ndio mwisho wa propaganda.
 
Mtandaoni haitakuwa proof nzuri maana siku zote hawaweki kwa wakati ama kutoweka. Mwenye acces ampigie Kibanda kisha atujuze
 
Kwani vp kuna habari yoyote uliyofuatilia imetoka kwenye hili gazeti..ngoja kwanza.
 
Hata mimi nashangaa sana..sijui wamefeli nini gazeti kubwa kama lile. Nimejisikia vibaya sana kwani ndilo gazeti langu hilo
 
Nimepata habari kutoka Freemedia kuwa tayari liko mitaani, ngoja nitoke nikalitafute lakini mvua mh....
 
Wapendwa wana jf, nimepita kwenye mitaa kadhaa ya Dar kutafuta gazeti nilipendalo la Tanzania Daima bila mafanikio. Kila ukiuliza wauzaji wanasema leo halijatoka. Kulikoni? walio karibu na Freemedia watujuze kinachoendelea. Ama ndio magamba wameleta fitina zao kwani leo na kesho ndio mwisho wa propaganda.

soma online
 
Kwa ujumla Gazeti la Tanzania Daima limekuwa limekuwa likisha mapema sana hapa Mbeya katika wiki hii. Ukichelewa kama saa moja baada ya gazeti kufika huwezi pata nakala ya Tanzania Daima.
 
Magazeti mengi yameenda Dodoma ambako Lowassa aliagiza yapelekwe kwa wingi kwa kuwa Tz Daima lime-carry habari ambayo source ni yeye (Lowassa: Eti Fedha zamwagwa kumng'oa Lowassa! Upuuzi mtupu.
 
gazeti liko mtaani wewe umetafutia magogoni utalipata wapi au ndo bosi wako kakutuma upime upepo
 
...mimi nimelipata Tz-daima la leo exctly saa-1 asubuhi hapa Kimara-Dsm. Wewe ulikuwa unalitafuta mkoa gani ambako ulilikosa?
 
Pesa imemwagwa au siri za Jakaya zimefichuka kiasi cha CCM kuamua kuyamaliza kifisadi. Kimsingi tumenufaika kujua kuwa kumbe Richmond ni wawili yaani Lowassa na Jakaya Kikwete wanaomtumia mwarabu wao wa Igunga. Hata siri ya kutotaka Samuel Sitta aendelee kuwa spika imefichuka. Maana kama siyo hili ngigi lao bunge lingekaa na kujadili mambo yafuatayo
1. Nani alikuwa nyuma ya Richmond?
2. Kwanini Kikwete alimzuia Lowassa kuvunja mkataba wa Richmond?
3. Kwanini rais na waziri wake mkuu walilidanganya bunge na taifa?
4. Kwanini wawili hawa wasichukuliwe hatua haraka?
5. Je baada ya ukweli kubainika Kikwete anatoa utetezi gani unaoingia akilini?
6. Baada ya ukweli kujulikana, katiba na watanzania wanasemaje?
7. Kama rais anaweza kudanganya umma na kupinda sheria kwa maslahi binafsi anafaa kuendelea kuwa rais.
8. Kwanini serikali ya Kikwete imekuwa nyepesi kulipa Dowans ambayo ni Richmond?
9. Je kuna mgongano wa kimaslahi na uvunjaji wa katiba?
10. Je suala la ufisadi na uchafu wa Kikwete na Lowassa ni suala la CCM au taifa?
11. Je ni vizuri kuanza hatua za kumu-impeach Kikwete?
12. Je Kikwete atalimalizaje hivi na abaki salama?
13. Je taifa na mamlaka ya urais viko salama mikononi mwa mtu kama huyu anayetia kila aina ya shaka?
Ongezea hadi mia.
 
Hii habari ni ya saa 13:00 tarehe 30th September 2011.
Nawashangaa mnairukia tu kana kwamba ni freshi newz!!
 
Hili tatizo la kuambiwa kuwa Tanzania Daima leo halijatoka si mara yake ya kwanza! kuna siku nilizunguka Tabata yote nalitafuta sikulipata nikaambiwa eti halijatoka! Nikatuma message kwa mhariri ili nipate kujua tatizo lakutopatikana kwa gazeti hili,sikujibiwa! Ndugu zetu Tanzania Daima,"Kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza" na chonde chonde angalieni isije tokea kuwa,"Mgema ukimsifia,tembo hulitia maji".
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom