Tanzania Daima kuweni makini...Jiepusheni na 'Ukanjanja huu' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Daima kuweni makini...Jiepusheni na 'Ukanjanja huu'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Balantanda, Apr 16, 2010.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Katika pitapita yangu kwenye mtandao wa gazeti la Tanzania Daima nimekutana na habari ambazo zimenifanya niamini kwamba hawa jamaa (wa Tanzania Daima) hawapo makini kabisa....Hivi wahariri wanafanya kazi gani???....Soma hbari hizi hapa chini utaona ni kitu gani namaanisha

  Mtangazaji ITV kuwania ubunge Ulanga Magharibi

  na Marietha Mkoka na Benidect Kiwia

  MTANGAZAJI mwandamizi wa kituo cha runinga cha ITV, Reinfred Masako, ametangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Ulanga Magharibi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) linaloshikiliwa na Juma Kapuya ambaye ni Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Masako alisema ameamua kwa dhati kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu mwaka huu kutokana na haki yake ya msingi aliyonayo ya kuchagua na kuchaguliwa katika ngazi yoyote ya uongozi.


  Masako alisema nia hiyo ya kuwania ubunge kwenye jimbo hilo zaidi ni kusambaza elimu kuhusu hifadhi ya jamii, lishe bora kwa makundi maalamu ya kina mama wajawazito na wazee, siasa, uchumi na maendeleo ya jamii pamoja na usalama wa raia na mali zao katika michezo.


  Mkongwe huyo wa habari aliyefanya kazi takriban miaka 32 toka mwaka 1978 hadi hivi sasa na katika vipindi vitatu tofauti visivyopungua miaka 10 alitumia muda huo kutoa elimu ya jamii zaidi kitu ambacho kinampa fursa ya kuwania jimbo hilo.


  “Nimedhamiria kuhamisha uzoefu wangu niliopata katika utendaji wangu kwa miaka yote isiyopungua 32 kwa wananchi wenzangu katika kulenga maeneo makuu matatu ikiwa ni pamoja na shughuli za kilimo, uvuvi na ufugaji,” alisema Masako.


  Aidha, Masako alisema fursa zilizopo katika jimbo ambalo ameweka nia ya kugombea ni pamoja na mito yenye maji yanayotiririka mwaka mzima, miradi ya skimu za maji akielezea kuwa hizo ni rasilimali tosha zinazohitaji maelekezo sahihi ya jinsi ya kutumia na kubadilisha maisha ya wakazi wa jimbo hilo.


  Pia alisema amedhamiria kuutumia uzoefu wake ambao kwa ujumla ni sawa na mgodi unaotembea ili wananchi wa jimbo lake waweze kunufaika nao na utekelezaji wake upo ndani ya matumizi sahihi ya fursa ya mapinduzi ya kijani.  na hii


  CCM wakorogana kampeni za JK

  na Hellen Ngoromera

  KAMATI za kampeni za mgombea urais za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya Rais Jakaya Kikwete zimeanza kukorogana.

  Mkorogano huo umeanza kujitokeza katika Kamati ya Fedha na Vifaa vya Kampeni iliyotangazwa awali kuwa inaongozwa na Mhazini wa CCM, Amos Makala.

  Wakati wa uzinduzi wa uchangishaji fedha kwa njia ya simu za mkononi katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Makala aliwatangazia wanachama kwamba ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo na makamu wake ni Zakhia Meghji.


  Lakini katika mkutano wa chama hicho na waandishi wa habari uliofanyika jana katika ofisi ndogo ya CCM, chama hicho kilitangaza kuwa Meghji ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo.


  Mkurugenzi wa Kitengo cha Propaganda, Ibrahim Msabaha, alisema kuwa Meghji ameteuliwa na NEC iliyomaliza kikao chake hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuongoza kamati hiyo.


  Msabaha aliitaja pia kamati nyingine ya Utekelezaji ambayo itasimamia shughuli zote za kukiletea ushindi chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba.


  Kamati nyingine ni ya Mkakati na Uenezi itakayokuwa chini ya Abdulrahman Kinana.


  Alisema katika maandalizi ya uchaguzi, pamoja na kununua magari 150 ambayo yamesambazwa katika halmashauri zote za wilaya kurahisisha usafiri kwa viongozi, CCM inatarajia kununua magari mengine hivi karibuni kwa ajili ya wagombea urais na wagombea wenza, pia mengine 26 kwa ajili ya mikoa yote.


  Katika hatua nyingine, Msabaha alisema kuwa pamoja na kutenga sh bilioni 40 kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu, bado kiasi hicho hakitoshelezi mahitaji yao.


  Msabaha alisema fedha hizo hazitoshi kutokana na mahitaji mbalimbali wakati wa uchaguzi, hasa ikizingatiwa kuwa chama chao ni kikubwa.


  “Ukinyumbulisha matumuzi ya fedha hiyo hayatoshelezi kabisa. Hapa tulipo tuko vichwa vinatuuma tuko hoi bin taaban kwani ukipiga hesabu kuna suala la kuzunguka huku na huko, kwa hiyo tutahitaji kuweka mafuta na mambo mengine. Sisi ni chama kikubwa,” alisema Msabaha baada ya kuulizwa swali kuhusu malalamiko ya wapinzani kuhusu CCM kutenga kiasi hicho na kwamba haioni kwa kufanya hivyo inakiuka sheria ya gharama za uchaguzi.


  Akizungumzia kuhusu msimamo wa chama hicho kuhusu kura za maoni Zanzibar, kuhusu kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa, Msabaha alisema CCM inakubali kuingia katika ushirikiano kuunda serikali ya pamoja.


  Kwa mujibu wa Msabaha, suluhu ya suala hilo ni kumaliza migogoro Zanzibar ambayo imekuwepo kwa muda mrefu kwa amani na maelewano.
  Ukiisoma habari ya kwanza utaona kwamba ni ya upotoshaji maana Mbunge wa Ulanga Magaharibi si Profesa Juma kapuya,ni Dk. Juma Ngasomgwa....Na habari ya pili nayo jina la Ibrahim Msabaha limeandikwa sivyo...Yule bwana wa Propaganda CCM anaitwa Salum Msabah ....Kuweni makini Tanzania Daima,wahariri fanyeni kazi mnayotakiwa kuifanya...Ni hayo tu
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Msimu wa hela huu bRODA...Wahariri hawana muda wa kupitia habari na kuexamine legitimacy yake, the thing ni kuzipokea tu na kulamba mafao, kufuatilia usahihi ni kazi ya mlaji ...eboo:D:D!
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Teh teh teh No Comment
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Apr 16, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Huu kweli ukanjanja, mhariri sijui anafanya kazi gani!
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,378
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  Kazi tunayo wajomba................
   
 6. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 500
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  I am not suprised. Siku za nyuma niliwahi kumwandikia message Kibanda kumshauri juu ya makosa uandishi kwenye lugha sikupata feedback yeyote, na bado makosa yanaendelea. Watapoteza credibility kwa wasomaji kwa uzembe unaozuilika.
   
 7. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Sasa sijui ni kwa nini tunakuwa na wahariri wa habari....Kibanda na umakni wake wote anayaachia haya yapite!!!...inashangaza kweli....Wabadilike..
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Pesa pesa Pesa nini maana ya mhariri wa habari?
  Ni wazi anashindwa kujua wajibu wake
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama wahariri wa vyombo vyetu huwa wanapitia au kuhakiki habari.
  Na kipindi hiki cha uchaguzi wapo busy kuwapa promo wagombea si mnajua mambo ya njaa.
   
 10. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hayo ni matokeo ya waandishi wa bei poa wasio na taaluma..mhariri usipokuwa makini na kutokana na presha ya kuwahi deadline kitu kinatoka na makosa...sijui kama kwenye postmortem huwa wanakaa na kukemea kasoro hizi. Kazi kweli kweli yaani mhariri wa habari kapitiwa, mhariri mtendaji kapitiwa na proofreader nae ?.
   
 11. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli inashangaza na kusikitisha sana kuona mwandishi wa gazeti 'kubwa' la Tanzania hawezi kuelewa Juma Kapuya ni mbunge wa wapi,anaandika habari na mhariri wake anaipitisha tu......aibu kweli jamani....Kwangu mimi waandishi wa habari hii na wahariri wa gazeti wote ni 'makanjanja' tu(samahani kama nimewakwaza,ukweli daima huuma)......
   
 12. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kibanda anaondoka pale (Free media) huenda ndo maana umakini umepungua.
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Signature yako nimeipenda
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Msisahau kuna watangazaji nao wa bei chee wananunuliwa kwa bei chee ya kutupwa.
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Ukiisoma habari ya kwanza utaona kwamba ni ya upotoshaji maana Mbunge wa Ulanga Magaharibi si Profesa Juma kapuya,ni Dk. Juma Ngasomgwa....Na habari ya pili nayo jina la Ibrahim Msabaha limeandikwa sivyo...Yule bwana wa Propaganda CCM anaitwa Msabaha Salum....Kuweni makini Tanzania Daima,wahariri fanyeni kazi mnayotakiwa kuifanya...Ni hayo tu

  Mkuu,
  Ni Salim Msabah
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Kwani Kapuya jimbo lake lipi?...labda hiyo ndio dosari yenyewe
   
 17. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Ni Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi......Sasa iweje mwandishi aandike kuwa ni Ulanga Magharibi bana...Masako jana katangaza kugombea Ulanga Magharibi kwa Dk. Ngasongwa.........waandishi wetu ni makanjanja..period...Tusitetee uozo kihivi...Pamoja
   
 18. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Umesomeka mkuu....lengo langu lilikuwa kuwakumbusha hawa jamaa wa T/Daima kuwa makini katika uhariri wa habari zao...Maana Ibrahim Msabaha ni mbunge(wa mojawapo ya majimbo ya Kibaha)...na Salum Msabah(kuna kipindi pia huwa anjiita Msabah Salum,hasa kipindi akiwa Mwakilishi wa Mkunazini kwa tiketi ya CUF mara nyingi nilikuwa nikisikia akiitwa Msabah Salum)....Hili la Salim sina uhakika nalo...Anyways,nadhani ujumbe umewafikia Tanzania Daima
   
Loading...