TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Kuna taarifa kuwa jana tarehe 04 Januari, 2017 Katika ofisi za gazeti la Tanzania Daima kulikuwa na patashika Nguo kuchanika.
Kwa mujibu wa mdakuzi wa taarifa hii, chanzo cha patashika hiyo ilitokana na UKATA unaoukabila uongozi wa gazeti hilo, hali iliyopelekea Watumishi kutolipwa mishahara yao yapata miezi MITANO sasa.
Habari zaidi zinasema mhariri Mkuu wa Tanzania Daima, Ndugu NEVILLE MEENA ametimuliwa kazi kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuingiza wafanyakazi wengi wasiyo kuwa na tija kwa gazeti huku wakilipwa mishahara mikubwa.
Wakati huo huo Mmiliki wa gazeti la Tanzania Daima ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), FREEMAN AIKAELI MBOWE ametoa maagizo ya kuwatimua wafanyakazi wangine na kuwabakiza kumi na nne(14) tu.