Tanzania Daima - Dr. Slaa kinara urais 2015 maoni

Status
Not open for further replies.

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,883
IMG00078-20121128-0854.jpg

images
images

Kulia: Dr. Slaa; Kushoto :Zitto Kabwe
Candidates wa Chadema

images
images

Candidates wa CCM
Edward Lowasa na Bernard Membe
Dk. Slaa kinara urais 2015
• MATOKEO KURA ZA MAONI YAWATAJA LOWASSA, MEMBE NA ZITTO KABWE
WAKATI mjadala wa nani anafaa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Serikali ya Jamhuri ya Mungano unashika kasi kila kona ndani na nje ya nchi, jina la Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa limeng'ara, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Pamoja na uwepo wa vyama 18 vya siasa vyenye usajili wa kudumu, mjadala wa nani anafaa kuwa Rais ajaye, umejikita kwenye vyama vikubwa viwili, kikiwemo Chama tawala cha Mapinduzi (CCM) na Chama Kikuu cha Upinzani cha CHADEMA.
Kwa mujibu wa kura za maoni zilizoendeshwa na mtandao maarufu dunaini wa Jamii Forum kwa kuuliza "Nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA na CCM", majina manne yalipambanishwa, mawili kutoka CCM na mawili CHADEMA.

Waliopambanishwa kutoka CCM ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, ambao wamekuwa wakitajwa kuibua makundi yanayosigana kutaka urais mwaka 2015.
Licha ya kuwapo majina mengine yanayotajwa kufaa kuwania urais ndani ya CCM, wapambe wa Lowassa na Membe, wamekuwa katika mvutano mkali na wa wazi na kuibua mpasuko mkubwa ambao ulionekana wazi hata wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma.

Baadhi ya majina mengine yanayotajwa kuutaka urais CCM ambayo hayakushindanishwa kwenye kura hizi za maoni ni pamoja na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuri, Steven Wassira, Dk. Emmanuel Nchimbi, Frederick Sumaye na Dk. Asha Rose Migiro ambaye hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa mjumbe wa Sekretarieti ya CCM, akiongoza idara ya mambo ya nje.
Nafasi hiyo inampa sifa Dk. Migiro kuingia kwenye vikao muhimu vya chama vya Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC).

Kwa upande wa CHADEMA, kura za maoni zilizoanza Julai, mwaka huu, ziliwakutanisha Katibu Mkuu na mgombea urais mwaka 2010, Dk. Slaa na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Zitto Kabwe.
Katika siku za hivi karibuni, Zitto amekuwa akijinasibu kutaka kuwania urais mwaka 2015 na kupendekeza sifa ya umri wa kugombea kiti hicho upunguzwe kutoka miaka 40 hadi 35.

Hata hivyo majina mengine yanayotajwa kufaa kuwania urais ndani ya CHADEMA na ambayo hayakushirikishwa kwenye kura hizo za maoni ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, ambaye yuko nyuma ya mafanikio yote ya CHADEMA hadi kufikia hatua hii. Katika ordha hiyo, pia yumo Mbunge wa Singida Vijijini, Tundu Lissu.

Matokeo yanaonyesha kuwa

Matokeo ya kura hizo za maoni, yanaonyesha kuwa jumla ya wapiga kura
1188 walishiriki kuwapigia kura wagombea wa CHADEMA, Dk. Slaa na Zitto, wakati wapiga kura 375 walishiriki kuwapigia Lowassa na Membe, wote kutoka CCM.

  1. Dk. Slaa kura 1,007, sawa na asilimia 84.76%
  2. Zitto, Kabwe Kura, aliibuka na kura 181, sawa na asilimia 15.
  3. Edward Lowasa kura164, sawa na asilimia 43.73
  4. Membe Membe kura 67, sawa na asilimia 17.87.

Aidha kwa mujibu wa matokeo hayo, wapiga kura 144 walipiga kura ya kutomuunga mkono mgombea yeyote kati ya Membe na Lowassa.

Matokeo ya jumla yanaonyesha kuwa Dk. Slaa aliibuka na ushindi mkubwa wa kura 1,007 kwa kupigiwa kura nyingi zaidi kuliko majina ya washiriki wengine waliopendekezwa kuingia kwenye mnyukano huo.
Mshindi wa pili ni Zitto mwenye kura 181, watatu ni Lowassa mwenye kura 164 na Waziri Membe anashika nafasi ya nne kwa kura 67.

Licha ya kupata kura chache kwenye mchuano huo, jina la Waziri Membe limekuwa likitajwa zaidi tangu alipoibuka mshindi kwenye nafasi ya ujumbe wa NEC kupitia kundi maalum (Kundi la Kifo), licha ya kupigiwa kampeni chafu na mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), Hussein Bashe, ambaye bila kumung'unya maneno alitamba kumpigia kampeni za kumwangusha asishinde nafasi hiyo.

Hata hivyo matokeo ya kura hizo za maoni sio rasmi kwani kati ya majina yote yaliyoshirikishwa kwenye kura hizo, hakuna hadi sasa aliyekwishatangaza nia ya kuwania urai 2015.
 
Mkuu una quote Tz Daima?
Ni Sawa n ku quote Uhuru tu, inthe extreme opposite.

Hayo magazeti ya vyama, read them with care!
 
Kama uchaguzi ungefanyikia mijini tu, matokeo yangekuwa hivyo. Bahati mbaya wa vijijini walio wengi hawajui kinachoendelea. Elimu ya uraia bado kule. Nirahisi kudanganywa na t-shiet au kanga!!!
 
Mkuu una quote Tz Daima?
Ni Sawa n ku quote Uhuru tu, inthe extreme opposite.

Hayo magazeti ya vyama, read them with care!

JF for Great Thinkers ndo iliyokuwa ''quoted'' acha kulalamika........, we si ulipiga kura, au...kama unaweza appeal fanya
 
JF for Great Thinkers ndo iliyokuwa ''quoted'' acha kulalamika........, we si ulipiga kura, au...kama unaweza appeal fanya
Ni dhahiri kuwa kama Dr angekuwa na constituency au nchi ya JF peke yake, leo angekuwa rais wa JF, thats clear.
We are taliking of Tanzania meeen, wake up!
 
Kuna tatizo kwenye poll ya ZZK na Dr. Slaa...hakuna option ya mtu kumkataa yeyote kati ya hawa...else asipige kura..

So maoni haya yamefinywa uhuru..
 
kama unafiki ukiwekwa pembeni na maslahi ya kuchumia tumbo kwa baadhi ya vijana wenye ushawishi mipango thabit ya kuzibiti wizi mambo na kama hivi hivi
 
Kama ataendelea kuwa imara bila kuyumba dr slaa ananafasi kubwa ya kufanya vizuri kama atagombea 2015 ni mwanasiasa mwenye nyota na hapotezi mvuto wake..ni kama suruali ya jeans kwenye fashion ya nguo au soccer brazil
 
Kama kuna maswali yasio majibu ni kutumia vibaya magazeti kuhadaa umma. Leo hii tanzania daima imeweka matokeo ya kura za maoni ya urais mwaka 2015 na kujinadi eti slaa ni kinara. Wataalamu wa masuala ya siasa na uchumi wa chuo kikuu leo wameponda matokeo kama haya kuwekwa kwenye vyombo vya habari. Lakini walikwenda mbali na kusema vyombo hivyo ni questionable kwa sababu havina objectivity na ni vyombo vinavyo shabikia chadema kupindukia kiasi cha watu kuto vichukulia seriously pale vinapotoa habari kama hizo. Wamehoji sampling method, wakashangaa kuwajumuisha slaa zito na lowasa wakati hat vyama vyao havijawapitisha. Wengine wakabaini ni mbinu ya kusafisha jina kufuatia kuporomoka kwa kasi kwa umaarufu wa mmoja wa hao watu kufuatia kimbunga cha kinana na timu yake. Hapa wana jf nao wachangie kinyoosha hizi globe zisiwe ni vichaka vya kampeni mufilisi.
 
Kura za maoni ni maoni. Tusidharau hata kidogo maoni ya watu. Kilichoandikwa na TanzaniaDaima ndio maoni ya wana JF wengi. Ni lazima tuheshimu maoni hayo. Ili kupinga kura ya maoni, fanya kura yako ya maoni. As far as I am concerned, kura za JF ni mwakilishi sahihi wa wana JF na lazima tuheshimu
 
Dr. Slaa all the way
 
Mmmmhhh,,,JF ni mtandao wa watu si mbuzi,,watu ndo wanapiga kura si mbuzi,watu ndo wanashika hatamu ya uongozi si mbuzi,na ww ni mtu uliyejiandikisha humu JF si mbuzi na ndoo maana umepata fursa ya kutoa maoni yako kama haya,,,let's people decide what they want about our president,,,naamini upepo ni hewa isiyoonekana ila kwa jinsi Tanzania inapoelekea basi upepo ni hewa inayoelekea kuonekana kwa macho,,,wasup JF! Wasup TZ!
 
Kura za maoni ni maoni. Tusidharau hata kidogo maoni ya watu. Kilichoandikwa na TanzaniaDaima ndio maoni ya wana JF wengi. Ni lazima tuheshimu maoni hayo. Ili kupinga kura ya maoni, fanya kura yako ya maoni. As far as I am concerned, kura za JF ni mwakilishi sahihi wa wana JF na lazima tuheshimu

Ni dhahiri kuwa kama Dr angekuwa na constituency au nchi ya JF peke yake, leo angekuwa rais wa JF, thats clear.
We are taliking of Tanzania meeen, wake up!

Mkuu Mhe. Zitto , I concur with your observation by 100%.
 
Mkuu una quote Tz Daima?
Ni Sawa n ku quote Uhuru tu, inthe extreme opposite.

Hayo magazeti ya vyama, read them with care!

Binafsi sikupiga kura kwa sababu ya utaratibu uliopo mtu anaweza kupiga zaidi ya mara 10 kwa mtu mmoja. JF administration wangejaribu kuweka utaratibu wa kielectronic ambao members wanatambuliwa na ingekuwa kura ya kweli, lakini hii just propaganda.
 
Uchaguzi mkuu utakapofika hoo unajua Slaa Dr. ndo rais bali aliibiwa kula kumbe utalatibu mnaoutumia wala sio sahihi kwani JF haipo mpaka bush huko kwenye population kubwa ya wapiga kula.
 
Uchaguzi mkuu utakapofika hoo unajua Slaa Dr. ndo rais bali aliibiwa kula kumbe utalatibu mnaoutumia wala sio sahihi kwani JF haipo mpaka bush huko kwenye population kubwa ya wapiga kula.
kwani nani kasema haya ni maoni ya watanzania wote? kuna watu wamepaniki bila sababu,haya ni maoni ya wana jf na hayawakilishi watu wote katika nchi hii, na kama alivyosema Zitto, yanapaswa kuheshimiwa.
lakini pia ukweli unabaki kwamba asilimia kubwa ya michango ya wana jf wengi iko positive kwa chadema kama chama cha siasa na kwa dr slaa kama mwanasiasa,,hili lipo wazi tu. lakini kama wewe unaona huko vijijini kuna watu wanakushabikia wewe kuliko slaa au kama kuna mwanasiasa ana nguvu kuliko wengine basi tuwekee utafiti wako na utuambie ulitumia njia gani kupata majibu ya utafiti wako, maana wa jf tunaufahamu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom