Kweli
JF-Expert Member
- Jul 14, 2007
- 1,152
- 302
Miaka nenda,miaka rudi tumekuwa tukisoma KERO zinazoiandama Bandari ya DAR kuhusiana na upotevu, uharibifu na ucheleweshaji wa huduma za makontena yanayoingia ama kupitia bandari hii ya DAR, wengi tunajua kuna ufisadi wa Hali ya juu huko TRA na Mamlaka ya Bandari na Serikali inapoteza mamillioni ya mapato kutokana na ufisadi na uzembe uliokithiri katika Idara hizi. Watanzania wengi wanaosafirisha vitu vyao nyumbani toka Ulaya na sehemu nyengine kwa huduma hii ya Kontena wanapata hasara kubwa, mimi binafsi nilipakia vitu vya nyumbani pamoja na gari mwezi wa December mwaka jana na kampuni ya Maersk na waliniahidi itafika baada ya mwezi,nilichukua likizo na kwenda nyumbani kufuatana na schedule ya meli ya Maersk lakini matokeo yake mpaka naondoka nikiwa nimechelewa kazini, nimeshapoteza nauli na hasara nyengine hakuna hio kontena??? lilipatikana baada ya miezi 5 baada ya kufuatilia sana.
Pengine Serikali ikianza kupata hasara kwa kila mteja kudai fidia kama huyu Mnaijeria Jude O Nwiza ndipo itawawajibisha watendaji wakuu wa THA na TRA.
Link ya habari hii hapa chini:
http://dailynews.habarileo.co.tz/home/index.php?id=6637
Pengine Serikali ikianza kupata hasara kwa kila mteja kudai fidia kama huyu Mnaijeria Jude O Nwiza ndipo itawawajibisha watendaji wakuu wa THA na TRA.
Link ya habari hii hapa chini:
http://dailynews.habarileo.co.tz/home/index.php?id=6637