Tanzania , Congo na Burundi waunda Rasmi Muungano wao mpya mara baada ya kutengwa na Rwanda, Kenya

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Tanzania , Congo na Burundi waunda Rasmi Muungano wao mpya mara baada ya kutengwa na Rwanda, Kenya na Uganda..!!

Wakati Kenya, Rwanda na Uganda zimeunda umoja unaoitwa `Umoja wa Walio Tayari’ , Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) nazo zimeanzisha ushirikiano baina yao.

Katika siku za karibuni kumekuwa na mtikisiko ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Tanzania na Burundi kutengwa na wenzao wa Kenya, Rwanda na Uganda katika baadhi ya masuala muhimu ya ushirikiano hasa wa kiuchumi.

Tanzania, Burundi na DRC nazo zimekutana ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliliambia Bunge lililopita kuwa Tanzania inafikiria kushirikiana na nchi hizo.

Mkutano wa ujirani mwema

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa Ujirani Mwema uliofanyika mjini Bujumbura, Burundi jana, Sitta alisema Tanzania, Burundi na Kongo zimekubaliana kuendeleza miundombinu ya barabara, reli, anga na usafiri wa maji katika Ziwa Tanganyika.

Alisema mkutano huo ulilenga kuboresha miundombinu ya usafiri katika Ziwa Tanganyika ambalo linaziunganisha Burundi Tanzania, DRC na Zambia.

“Pia tumepanga kuendeleza reli ya kati kutoka eneo la Uvinza, Tanzania hadi Msongati, Burundi na pia kuunganisha Barabara ya Manyoni - Tabora - Kigoma kupitia Bujumbura hadi Kivu ya Kusini, DRC,” alisema Sitta.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Sitta pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Burundi, Leontine Nzeyimana na Waziri wa Uchukuzi wa DRC, Jack Lukeba.

“Pia tulitembelea Bandari ya Kalindo iliyoko katika Ziwa Tanganyika upande wa Burundi kwani tunataka kuboresha bandari za ziwa hilo,” alisema Sitta.

Waziri huyo alisema Tanzania na Burundi zitaunganishwa na Barabara ya Manyoni – Tabora - Kigoma na Barabara ya Manyovu - Mgina, Mabanda - Bujumbura itakayounganishwa mpaka Kivu ya Kusini, DRC.

Kuhusu usafiri wa anga, Sitta alisema nchi hizo zinaangalia uwezekano wa kuanzisha safari za ndege za Dar es Salaam mpaka Bujumbura.

Muungano wa Walio Tayari

------Mwananchi
 
Basi mimi naona sawa tu, inafaa kuwe sasa na ushindani wa kiuchumi baina ya miungano hii, nakuhakikishia Afrika Mashariki kwa ujumla itaibuka kuwa jitu la kiuchumi. Sisi Wakenya sasa tupo mbioni tayari.
 
KWA HIYO MAPING BOUNDRY JINSI ILIVYOKAA VEMA INAPENDEZA SANA!!SIO MBAYA JUMUIYA IKAWEPO KAMA KAWAIDA NA MAUSIANO YA KIKANDA YAKAWEPO PIA,"WEST EAST ECONOMIC ZONE" <WEEZ> YETU,AWAKENING OF THE GIANT BRINGS TERRIBLE TO OTHERS....tunatarajiakupata taarifa za namna hii
 
Hili mimi nililipenda liwe hivi tangu mwanzo!Badala ya kulialia tunatengwa ni bora huu yhusiano ungeanza bila kusema chochote wala kulalamika.Yaani dawa ya mnafiki ni kuwa mnafiki pia! Sijui kwanini JK alikuwa nalialia pale dodoma wakati suluhisho lilitakiwa liwe ni hili tangu mwanzo.
 
MTU YEYOTE MWENYE AKILI TIMAMU AKIANGALIA UKUBWA WA HIZO NCHI TATU KATIKA RAMANI;-tutapata; 1.soko la uhakika
2.
n.b mm sio mchumi,wachumi endelezeni!
 
Kuhusu usafiri wa anga, Sitta alisema nchi hizo zinaangalia uwezekano wa kuanzisha safari za ndege za Dar es Salaam mpaka Bujumbura.

Muungano wa Walio Tayari

------Mwananchi
[/FONT][/COLOR]

Hivi shirika la ndege la Tanzania lina ndege ngapi vile....!!!!!!!????
 
Hivi shirika la ndege la Tanzania lina ndege ngapi vile....!!!!!!!????

Hahahahaha, 'muungano wa wasio tayari'
Usafiri wa anga??
Hiyo reli yenyewe ni propaganda tu, reli hawaitaki watakufa njaa hawa wachumia Tumbo.
 
MTU YEYOTE MWENYE AKILI TIMAMU AKIANGALIA UKUBWA WA HIZO NCHI TATU KATIKA RAMANI;-tutapata; 1.soko la uhakika
2.
n.b mm sio mchumi,wachumi endelezeni!

its not the size of dog that matters. Its the size of the fight in the dog that really matters. Case study nzuri Rwanda versus Tanzania.
 
Basi mimi naona sawa tu, inafaa kuwe sasa na ushindani wa kiuchumi baina ya miungano hii, nakuhakikishia Afrika Mashariki kwa ujumla itaibuka kuwa jitu la kiuchumi. Sisi Wakenya sasa tupo mbioni tayari.

bila ushirikiano thabiti wa Tanzania na Kenya hakuna kitu kinaitwa EAC....lazima tukubali kuwa Uhuru Kenyata and his Co of M7 and kagame wameamua kuua EAC.....haitakufa ghafla lakini itakufa taratibu kwa members kutohudhuria hata mikutano na pengine kutotoa ada za uanachama na hivyo itaanza kuvarnish taratibu na mwishowe itakufa.

The backborne of EAC ni TZ na Kenya, no good relation between the two...NO EAC...period.
 
Kinacho ua EAC ni ubinafsi wa Viongozi hususan Uhuru Kenyatta kwa kutaka kumiliki kila njia ya uchumi katika Ukanda huu na anajua mshindani pekee ni Tanzania na ana hofu na Ushindani uliopo kati ya bandari ya Dar- Es-Salaam na Mombasa.Nia ni kugombea mizigo toka nchi za Uganda,Rwanda na DRC.Hivyo Tanzania hakuna haja ya kulalama ni kuchukua hatua mipango iliyopo katika makaratasi kama kimarisha bandari ya DSM,kujenga reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa,kuwa na meli za uhakika katika Ziwa Tanganyika na Kuunganisha nchi hizi (Rwanda,Burundi na DRC) katika reli ya kati.Tusilalame wakuu wa nchi tafuteni fedha kwa ajili miradi hiyo tusiwe watalii na kuvaa suti watendeeni haki watu.Leo Kabila,Kagame,Kikwete, Kenyatta,Museveni lakini kesho hawapo kwani hawawezi ishi milele ila nchi hizi na watu wake watakuwepo milele.Hivyo hiyo safari Samweli Sita isiwe ya kutishia nyau iwe kweli na utekelezaji uanze sio tunatukanwa kuwa sisi Watanzania ni maneno tu hakuna utekelezaji.
 
Is this a coalition of the willing or a coalition of convenience?
 
Tanzania stop trade agreement with the Old EAC but not get out of the membership. But stop Kenyan Companies to robe in Tanzania
 
Lakini mkuu vowed to settle dispute diplomatically kwa kuongea nao face to face na akasema amekwishaanza,,, kumbe nyuma ya pazia kuna mengine yanaendelea!...politics!!!
 
Tanzania , Congo na Burundi waunda Rasmi Muungano wao mpya mara baada ya kutengwa na Rwanda, Kenya na Uganda..!!

Wakati Kenya, Rwanda na Uganda zimeunda umoja unaoitwa `Umoja wa Walio Tayari' , Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) nazo zimeanzisha ushirikiano baina yao.

Katika siku za karibuni kumekuwa na mtikisiko ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Tanzania na Burundi kutengwa na wenzao wa Kenya, Rwanda na Uganda katika baadhi ya masuala muhimu ya ushirikiano hasa wa kiuchumi.

Tanzania, Burundi na DRC nazo zimekutana ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliliambia Bunge lililopita kuwa Tanzania inafikiria kushirikiana na nchi hizo.

Mkutano wa ujirani mwema

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa Ujirani Mwema uliofanyika mjini Bujumbura, Burundi jana, Sitta alisema Tanzania, Burundi na Kongo zimekubaliana kuendeleza miundombinu ya barabara, reli, anga na usafiri wa maji katika Ziwa Tanganyika.

Alisema mkutano huo ulilenga kuboresha miundombinu ya usafiri katika Ziwa Tanganyika ambalo linaziunganisha Burundi Tanzania, DRC na Zambia.

"Pia tumepanga kuendeleza reli ya kati kutoka eneo la Uvinza, Tanzania hadi Msongati, Burundi na pia kuunganisha Barabara ya Manyoni - Tabora - Kigoma kupitia Bujumbura hadi Kivu ya Kusini, DRC," alisema Sitta.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Sitta pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Burundi, Leontine Nzeyimana na Waziri wa Uchukuzi wa DRC, Jack Lukeba.

"Pia tulitembelea Bandari ya Kalindo iliyoko katika Ziwa Tanganyika upande wa Burundi kwani tunataka kuboresha bandari za ziwa hilo," alisema Sitta.

Waziri huyo alisema Tanzania na Burundi zitaunganishwa na Barabara ya Manyoni &#8211; Tabora - Kigoma na Barabara ya Manyovu - Mgina, Mabanda - Bujumbura itakayounganishwa mpaka Kivu ya Kusini, DRC.

Kuhusu usafiri wa anga, Sitta alisema nchi hizo zinaangalia uwezekano wa kuanzisha safari za ndege za Dar es Salaam mpaka Bujumbura.

Muungano wa Walio Tayari

------Mwananchi

Old news is no news
 
hilo ni jambo la msingi ambalo lilitegemewa na wengi
ukiona ramani utaona kuwa nchi hizi zote kuna upana wa kiuchumi
hivyo tuanze ziara ya kuzitembelea ili tuweekeze kibiashara huko
 
Back
Top Bottom