• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Tanzania , Congo na Burundi waunda Rasmi Muungano wao mpya mara baada ya kutengwa na Rwanda, Kenya

MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,320
Points
2,000
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,320 2,000
Tanzania , Congo na Burundi waunda Rasmi Muungano wao mpya mara baada ya kutengwa na Rwanda, Kenya na Uganda..!!
Wakati Kenya, Rwanda na Uganda zimeunda umoja unaoitwa `Umoja wa Walio Tayari’ , Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) nazo zimeanzisha ushirikiano baina yao.

Katika siku za karibuni kumekuwa na mtikisiko ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Tanzania na Burundi kutengwa na wenzao wa Kenya, Rwanda na Uganda katika baadhi ya masuala muhimu ya ushirikiano hasa wa kiuchumi.Tanzania, Burundi na DRC nazo zimekutana ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliliambia Bunge lililopita kuwa Tanzania inafikiria kushirikiana na nchi hizo.


Mkutano wa ujirani mwema


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa Ujirani Mwema uliofanyika mjini Bujumbura, Burundi jana, Sitta alisema Tanzania, Burundi na Kongo zimekubaliana kuendeleza miundombinu ya barabara, reli, anga na usafiri wa maji katika Ziwa Tanganyika.Alisema mkutano huo ulilenga kuboresha miundombinu ya usafiri katika Ziwa Tanganyika ambalo linaziunganisha Burundi Tanzania, DRC na Zambia.“Pia tumepanga kuendeleza reli ya kati kutoka eneo la Uvinza, Tanzania hadi Msongati, Burundi na pia kuunganisha Barabara ya Manyoni - Tabora - Kigoma kupitia Bujumbura hadi Kivu ya Kusini, DRC,” alisema Sitta.Mkutano huo ulihudhuriwa na Sitta pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Burundi, Leontine Nzeyimana na Waziri wa Uchukuzi wa DRC, Jack Lukeba.


“Pia tulitembelea Bandari ya Kalindo iliyoko katika Ziwa Tanganyika upande wa Burundi kwani tunataka kuboresha bandari za ziwa hilo,” alisema Sitta.Waziri huyo alisema Tanzania na Burundi zitaunganishwa na Barabara ya Manyoni – Tabora - Kigoma na Barabara ya Manyovu - Mgina, Mabanda - Bujumbura itakayounganishwa mpaka Kivu ya Kusini, DRC.Kuhusu usafiri wa anga, Sitta alisema nchi hizo zinaangalia uwezekano wa kuanzisha safari za ndege za Dar es Salaam mpaka Bujumbura.


Muungano wa Walio Tayari------Mwananchi
 
MK254

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Messages
16,841
Points
2,000
MK254

MK254

JF-Expert Member
Joined May 11, 2013
16,841 2,000
Basi mimi naona sawa tu, inafaa kuwe sasa na ushindani wa kiuchumi baina ya miungano hii, nakuhakikishia Afrika Mashariki kwa ujumla itaibuka kuwa jitu la kiuchumi. Sisi Wakenya sasa tupo mbioni tayari.
 
Threesixteen Himself

Threesixteen Himself

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Messages
8,081
Points
2,000
Threesixteen Himself

Threesixteen Himself

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2013
8,081 2,000
!
!
muunganiko na Zanzibar tu majanga,ndio iwe na burundi na kongo. duh
 
Crocodiletooth

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Messages
10,846
Points
2,000
Crocodiletooth

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2012
10,846 2,000
KWA HIYO MAPING BOUNDRY JINSI ILIVYOKAA VEMA INAPENDEZA SANA!!SIO MBAYA JUMUIYA IKAWEPO KAMA KAWAIDA NA MAUSIANO YA KIKANDA YAKAWEPO PIA,"WEST EAST ECONOMIC ZONE" <WEEZ> YETU,AWAKENING OF THE GIANT BRINGS TERRIBLE TO OTHERS....tunatarajiakupata taarifa za namna hii
 
ITEGAMATWI

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Messages
4,694
Points
2,000
ITEGAMATWI

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2012
4,694 2,000
Hili mimi nililipenda liwe hivi tangu mwanzo!Badala ya kulialia tunatengwa ni bora huu yhusiano ungeanza bila kusema chochote wala kulalamika.Yaani dawa ya mnafiki ni kuwa mnafiki pia! Sijui kwanini JK alikuwa nalialia pale dodoma wakati suluhisho lilitakiwa liwe ni hili tangu mwanzo.
 
Crocodiletooth

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Messages
10,846
Points
2,000
Crocodiletooth

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2012
10,846 2,000
MTU YEYOTE MWENYE AKILI TIMAMU AKIANGALIA UKUBWA WA HIZO NCHI TATU KATIKA RAMANI;-tutapata; 1.soko la uhakika
2.
n.b mm sio mchumi,wachumi endelezeni!
 
MwanaCBE

MwanaCBE

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2009
Messages
1,774
Points
2,000
MwanaCBE

MwanaCBE

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2009
1,774 2,000


Kuhusu usafiri wa anga, Sitta alisema nchi hizo zinaangalia uwezekano wa kuanzisha safari za ndege za Dar es Salaam mpaka Bujumbura.


Muungano wa Walio Tayari------Mwananchi
[/FONT][/COLOR]

Hivi shirika la ndege la Tanzania lina ndege ngapi vile....!!!!!!!????
 
K

kenwood

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2013
Messages
757
Points
195
K

kenwood

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2013
757 195
Hivi shirika la ndege la Tanzania lina ndege ngapi vile....!!!!!!!????
Hahahahaha, 'muungano wa wasio tayari'
Usafiri wa anga??
Hiyo reli yenyewe ni propaganda tu, reli hawaitaki watakufa njaa hawa wachumia Tumbo.
 
simplemind

simplemind

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2009
Messages
14,376
Points
2,000
simplemind

simplemind

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2009
14,376 2,000
MTU YEYOTE MWENYE AKILI TIMAMU AKIANGALIA UKUBWA WA HIZO NCHI TATU KATIKA RAMANI;-tutapata; 1.soko la uhakika
2.
n.b mm sio mchumi,wachumi endelezeni!
its not the size of dog that matters. Its the size of the fight in the dog that really matters. Case study nzuri Rwanda versus Tanzania.
 
Utingo

Utingo

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
7,391
Points
1,500
Utingo

Utingo

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2009
7,391 1,500
Basi mimi naona sawa tu, inafaa kuwe sasa na ushindani wa kiuchumi baina ya miungano hii, nakuhakikishia Afrika Mashariki kwa ujumla itaibuka kuwa jitu la kiuchumi. Sisi Wakenya sasa tupo mbioni tayari.
bila ushirikiano thabiti wa Tanzania na Kenya hakuna kitu kinaitwa EAC....lazima tukubali kuwa Uhuru Kenyata and his Co of M7 and kagame wameamua kuua EAC.....haitakufa ghafla lakini itakufa taratibu kwa members kutohudhuria hata mikutano na pengine kutotoa ada za uanachama na hivyo itaanza kuvarnish taratibu na mwishowe itakufa.

The backborne of EAC ni TZ na Kenya, no good relation between the two...NO EAC...period.
 
Suip

Suip

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2010
Messages
1,125
Points
1,500
Suip

Suip

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2010
1,125 1,500
Kinacho ua EAC ni ubinafsi wa Viongozi hususan Uhuru Kenyatta kwa kutaka kumiliki kila njia ya uchumi katika Ukanda huu na anajua mshindani pekee ni Tanzania na ana hofu na Ushindani uliopo kati ya bandari ya Dar- Es-Salaam na Mombasa.Nia ni kugombea mizigo toka nchi za Uganda,Rwanda na DRC.Hivyo Tanzania hakuna haja ya kulalama ni kuchukua hatua mipango iliyopo katika makaratasi kama kimarisha bandari ya DSM,kujenga reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa,kuwa na meli za uhakika katika Ziwa Tanganyika na Kuunganisha nchi hizi (Rwanda,Burundi na DRC) katika reli ya kati.Tusilalame wakuu wa nchi tafuteni fedha kwa ajili miradi hiyo tusiwe watalii na kuvaa suti watendeeni haki watu.Leo Kabila,Kagame,Kikwete, Kenyatta,Museveni lakini kesho hawapo kwani hawawezi ishi milele ila nchi hizi na watu wake watakuwepo milele.Hivyo hiyo safari Samweli Sita isiwe ya kutishia nyau iwe kweli na utekelezaji uanze sio tunatukanwa kuwa sisi Watanzania ni maneno tu hakuna utekelezaji.
 
EMT

EMT

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Messages
14,468
Points
2,000
EMT

EMT

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2010
14,468 2,000
Is this a coalition of the willing or a coalition of convenience?
 
Zanzibar-Nyamwezi

Zanzibar-Nyamwezi

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Messages
808
Points
225
Zanzibar-Nyamwezi

Zanzibar-Nyamwezi

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2013
808 225
Tanzania stop trade agreement with the Old EAC but not get out of the membership. But stop Kenyan Companies to robe in Tanzania
 
leme

leme

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2010
Messages
350
Points
225
leme

leme

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2010
350 225
Lakini mkuu vowed to settle dispute diplomatically kwa kuongea nao face to face na akasema amekwishaanza,,, kumbe nyuma ya pazia kuna mengine yanaendelea!...politics!!!
 
murutongore

murutongore

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Messages
2,035
Points
1,250
murutongore

murutongore

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2013
2,035 1,250
Tanzania , Congo na Burundi waunda Rasmi Muungano wao mpya mara baada ya kutengwa na Rwanda, Kenya na Uganda..!!
Wakati Kenya, Rwanda na Uganda zimeunda umoja unaoitwa `Umoja wa Walio Tayari' , Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) nazo zimeanzisha ushirikiano baina yao.

Katika siku za karibuni kumekuwa na mtikisiko ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Tanzania na Burundi kutengwa na wenzao wa Kenya, Rwanda na Uganda katika baadhi ya masuala muhimu ya ushirikiano hasa wa kiuchumi.Tanzania, Burundi na DRC nazo zimekutana ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliliambia Bunge lililopita kuwa Tanzania inafikiria kushirikiana na nchi hizo.


Mkutano wa ujirani mwema


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa Ujirani Mwema uliofanyika mjini Bujumbura, Burundi jana, Sitta alisema Tanzania, Burundi na Kongo zimekubaliana kuendeleza miundombinu ya barabara, reli, anga na usafiri wa maji katika Ziwa Tanganyika.Alisema mkutano huo ulilenga kuboresha miundombinu ya usafiri katika Ziwa Tanganyika ambalo linaziunganisha Burundi Tanzania, DRC na Zambia."Pia tumepanga kuendeleza reli ya kati kutoka eneo la Uvinza, Tanzania hadi Msongati, Burundi na pia kuunganisha Barabara ya Manyoni - Tabora - Kigoma kupitia Bujumbura hadi Kivu ya Kusini, DRC," alisema Sitta.Mkutano huo ulihudhuriwa na Sitta pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Burundi, Leontine Nzeyimana na Waziri wa Uchukuzi wa DRC, Jack Lukeba.


"Pia tulitembelea Bandari ya Kalindo iliyoko katika Ziwa Tanganyika upande wa Burundi kwani tunataka kuboresha bandari za ziwa hilo," alisema Sitta.Waziri huyo alisema Tanzania na Burundi zitaunganishwa na Barabara ya Manyoni &#8211; Tabora - Kigoma na Barabara ya Manyovu - Mgina, Mabanda - Bujumbura itakayounganishwa mpaka Kivu ya Kusini, DRC.Kuhusu usafiri wa anga, Sitta alisema nchi hizo zinaangalia uwezekano wa kuanzisha safari za ndege za Dar es Salaam mpaka Bujumbura.


Muungano wa Walio Tayari------Mwananchi
Old news is no news
 
Lady niece

Lady niece

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2014
Messages
956
Points
225
Lady niece

Lady niece

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2014
956 225
hilo ni jambo la msingi ambalo lilitegemewa na wengi
ukiona ramani utaona kuwa nchi hizi zote kuna upana wa kiuchumi
hivyo tuanze ziara ya kuzitembelea ili tuweekeze kibiashara huko
 

Forum statistics

Threads 1,402,880
Members 531,007
Posts 34,407,971
Top