Tanzania companies owned by foreigners | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania companies owned by foreigners

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee2000, Dec 22, 2009.

 1. M

  Mzee2000 JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 491
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Songas gesi yetu ipo tanzania lakini kwanini wakubwa wote ni wageni?
  Je sisi kweli umeneja hatuwezi?

  -Songas Managing Director, Chris Ford -
  -Songas Ubungo Plant Manager, Ramakrishna
  22nd December 2009


  Songas power plant at Ubungo  Songas Limited has become the first power plant in Tanzania to get the International Standard Organization (ISO) certificate.
  A statement issued in Dar es Salaam yesterday said Songas received the award after the certification body conducted a rigorous audit to ensure successful assimilation of the organization’s existing environmental, health and safety processes in accordance with ISO guidelines.
  “Songas is the only power plant in Tanzania to achieve ISO certificate, this is the result of many months of hard work and dedication by the entire Songas team”, read part of the statement.
  Songas Managing Director, Chris Ford said: "This is a very significant milestone; it shows the company’s determination to grow and develop the power sector in the country by raising the operational bar to international standards”.
  He said through the certificate, Songas would from now on combine both environmental, health and safety into one integrated management system. He said the certification differentiated the company in a competitive market place by clearly demonstrating that it adhered to world-class management standards.
  Songas Ubungo Plant Manager, Ramakrishna, said the certification was a result of team work. He said Songas always ensured that documentation of all environmental, health and safety procedures complied with the relevant standards.
  “We also provide regular trainings to our employees. In order to maintain the world class standards, Songas has implemented reporting measures and will conduct yearly audits by the accredited third party organization”, he said.
  SOURCE: THE GUARDIAN
   
 2. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  hiyo ndiyo bongo...
   
 3. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ndio nchi mliyoitengeneza, God have mercy on us. na bado ngoja afrika mashariki iiingie. itakuwa kwanza mzungu, then muhindi, then mkenya, halafu muosha vyoo ndo mbongo nchi yetu wenyewe.
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Yale ya madini vipi? Umeyasahau?
   
 5. R

  Rubabi Senior Member

  #5
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 30, 2006
  Messages: 174
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii gesi inatoka wapi?Si inatoka kwetu? Hivi viongozi wetu hawaoni hili?
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  bongo yetu ya mazuzu magic
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mbona hamuongelei kilichopo kwenye body ya habari, mnalaumu tu Uongozi?..Sasa mbandikaji nawe, umeweka maelezo mengi ya nini kama ulitaka kujadili uongozi wa weupe?...Hamjui kwamba ile mitambo ni lazima isimamiwe na wanaoijua?..Nyie mna wanataaluma wa masuala ya Gesi waliobobea? ..Kila nchi ina fani zake bana, Hamjui kwamba Tanzania (TBS) ilipata cheti bora kabisa cha upimaji wa condom katika EA, na kwamba nchi nyingi za jirani zinapimia condom zao kwetu? .. Mi nimekuwa interested na suala zima la certification by ISO kwa kampuni hii.
   
 8. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Nchi ya majizi mambo huenda kiholela tu...tunaibiwa kama vile tumelala usingizi wa pono then watu wanatushughuliki kisawa sawa!!!
   
 9. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Ala! Kumbe we ulitakaje? kabla hatujanung'unika tujiulize tumewekeza asilimia ngapi humo!!! Kama hatujawekeza chochote au tumewekeza kiduchu, then ulitarajia mzungu aweke hela yake akupe wewe ubosi mkuu?!THUBUTU!! tutaendelea hivi hivi, miaka yote hadi serikali itakapokuja kuwa serious na large investments!!
   
 10. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Tatizo lenu wabongo ni uwezo wenu mkubwa wa kusoma mabaya, kuona mabovu, na kugundua uhalifu wa wenzenu mkiacha mazuri yao kando na kutojali kujifunza mbinu za kufikia mafanikio bora. Mu-wazuri wa kulalamika na mna mbwembwe nyingi sana na ni hodari katika kuwakilisha malalamiko.

  Katika mwaka 2010 ebu badilikeni. Amasikeni, jumuhikeni na shirikini katika kutafuta maendeleo yeni binafsi na ya jamii zenu.
   
 11. Nicazius

  Nicazius Senior Member

  #11
  Dec 23, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkubwa, hii nchi ni shamba la bibi, Kila mru analima na kuvuna hata ambacho hakupanda, na tutaendelea hivi ikiwa hatutakuwa na nia ya kweli kuhusu mabadiliko, wengi wetu ni wachangia wa mada wazuri kabisa lakini utekelezaji ni sufuri kabisa.

  Tunatakiwa kuwa na mlengo thabiti kuhusu malengo na mataraji yetu, suala siyo nani anaongoza nini bali anafanya nini kwa taifa letu hilo, hapa nchini kuna utitili wa makampuni kutoka nje, wachina, wasausi, wakenya, etc Angalia kwa makini haya makampuni kazi zote wanaoutsource kwa makampuni yapi kama siyo makaumpuni kutoka nchini kwao na nje ya nchi yetu, na hayo makampuni baada ya kupata kazi nayo yanaoutsource kwa makampuni kutoka nchini kwao kwa madai hakuna wataalamu TZ.

  HII IMEKUWA NDIYO HALI HALISI KILA SIKU, kweli hata kuchimba mtoro wa majitaka unahitaji kampuni ktk China au kwingineko lifanye kwa kutumia watanzania kama vibarua, hali kama hii siyo nzuri.

  Kwa kweli tunahaitaji mabadiliko ya kweli in TZ yetu itowe ajira kwa waTZ WENYEWE
   
 12. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Omutwale,
  Ninakubaliana na wewe 100%. Watanzania inabidi wabadilike na waanze kuwa serious na kujitafutia maendeleo yao binafsi na yale ya familia zao. Endapo hilo litafanikiwa kwa watanzania walio wengi basi hata uchumi wa Tanzania utakuwa kweli unamilikiwa na watanzania wenyewe. Wengi wetu tunapenda njia za mkato, ikiwa ni pamoja na kusaka madaraka ya kisiasa ili kuweza kukandamiza rasilimali za nchi.
  Uchumi ndiyo unaoamua kila kitu, gharama za kutafiti na kuichimba ni kubwa ambazo kwa serikali ambayo inategemea kusaidiwa katika bajeti haiwezi kufanya biashara ya kuchimba gesi. Kwa hiyo njia muafaka ni kutafuta wawekezaji ambao watabeba risk ya kuweka mitaji yao. Na endapo hawatapata faida hiyo haitahusu serikali. Lakini hata hivyo, kwa mtu yeyote ambaye anaweka fedha zake ni lazima ahakikishe kuwa udhibiti wa mradi huo unakuwa katika mikono salama anayoiamini yeye na hapa hakuna longolongo. mtanzania yeyote anaweza kuajiriwa kama atakuwa na uwezo na ku-meet vigezo vya mwekezaji. Hata hivyo, katika anga za uwekezaji, watanzania hatuna sifa nzuri katika utendaji hasa katika nafasi za juu. Tabia ya wizi/udokozi, uvivu na uzembe vinameturudisha nyuma. Vilevile, utamaduni wetu wa kufanya kazi ni tofauti na ukweli.
  Kwahiyo tusifikiri kupewa kuongoza makampuni ya wawekezaji ni zawadi, NO!!
   
Loading...