Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Ndugu wapendwa Watanzania hizi ndio takwimu zinaoonesha namna Taifa letu linavyoenenda katika sekta mbalimbali kwa mujibu wa Utafiti na Taarifa ya WEF(World Economic Forum) ya Mwaka 2017.
- Ubora wa Barabara Sisi Watanzania tunashika nafasi ya 90 kati ya nchi 137 zilizofanyiwa utafiti.
- Ubora wa Viwanja vya Ndege hapa jamani tuko nafasi ya 114.
- Ubora wa huduma za umeme(Usambazaji) hapa wakuu tumeshika nafasi ya 119.
- Ubora wa Sekta Nyeti ya Afya, ndugu zangu tumeshika namba 114.
- Ubora wa Elimu, jamani ukweli mchungu hapa pia tumeshika namba 122.
- Katima masomo ya Hisabati na Sayansi, pia tunaogelea namba 119.
- Katika Uvumbuzi(Innovation) hapa tumeshika nafasi ya 82.
- Katika Umri wa kuishi(Life expectancy) hapa tumeshika namba 108.
- Masuala ya Usalama hapa tumeshika namba 83.
- Aidha, Imani ya kwa wanasiasa hapa sisi tumeambulia namba 48.