Tanzania chini ya chama Cha ukombozi CCM ,imeanza kuvilea viashiria vya kurudisha chiefdoms

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Katika Mambo makubwa ambayo Mwalimu Nyerere aliheshimika na legacy yake itabaki kwenye vichwa vya Watanzania,ni umoja na mshikamano wa Kitaifa.

Tanganyika chini ya dola ya Mwingereza ilitawaliwa katika mfumo wa indirect rule toka kwa wakoloni,kupitia machifu wa makabila mbalimbali na maakida,ambao walimrahisishia mkoloni kulitawala bara hili kwa urahisi kupitia watawala hawa wa kimila.

Machifu hawa walikuwa na nguvu kubwa sana katika jamii zao,Hali iliyopelekea mkoloni kututawala bila vikwazo.

Hata mikataba mikubwa ya ardhi ilifungwa na machifu baina yao na wakoloni. Hali hii ilishindwa kutengeneza umoja wa Kitanganyika kuweza kukabiliana na mkoloni,Hali iliyopelekea kuchelewa kukua kwa miji mbalimbali na kujiletea maendeleo Kama Taifa.

Funzo Hilo Mwalimu alilitumia vizuri wakati wa kupata madaraka kwa kuona ugumu na ubinafsi wa kuendelea kuwa na chiefdoms. Mwaka mmoja baada ya kupata Uhuru,serikali ya Mwalimu ilipitisha rasmi Sheria ya kuondoa mfumo huo.

Leo Tanzania chini ya chama Cha ukombozi CCM ,imeanza kuvilea viashiria vya kurudisha chiefdoms. Tatizo linakuja hapa,kwa nini wasijiridhishe na sababu za kuvunjwa chiefdoms ambazo Mwalimu aliziona Kama kikwazo katika kuunda umoja wa Kitaifa.

Hatuwezi kurudi kwenye dhama za kijima kuegemea kwa kuwa tuna dumisha utamaduni wetu. Lazima tuangalie athari inayoweza kusababisha mgawanyiko na mshikamano wa umoja wetu.

Hii ni mbinu dhaifu sana inayo ratibiwa na viongozi wa CCM kwenye mikoa mbalimbali,ambayo unataka kuturudisha kwenye ukabila.

Ukweli ni kwamba Tanzania ni nchi kubwa kieneo,lakini kama suala ni mgawanyo wa madaraka,kwanini tusitumie mfumo wa serikali ya majimbo,ambao ndiyo unao tumika duniani kote. Mfumo utakao rahisisha huduma za maendeleo kwa nchi.

Dalili hizi zinazo barikiwa na chief of chiefs mh. Hangaya ,zinaibuwa matamko mbalimbali toka kwenye Koo za kichifu kwa kujibatiza wazee wa mkoa fulani,kwa kujenga dhamira ya kurudi kwa mlango wa nyuma bila kuzingatia matakwa ya katiba.

Kama katiba yetu haijaruhusu,hii nguvu ya mama anaipata wapi kama si mbinu chafu za mahafidhina wenye uroho wa madaraka.

Ukichunguza kwa umakini utaona wanao shabikia uchifu ni wazee wastaafu ambao ni makada wa chama,wakitafuta kuendelea kuwepo kwenye madaraka kwa mgongo wa chiefdoms.

Tujitazame na kujitafakari kwa kina,kama kweli Watanzania wanataka kurudisha mfumo huo.

Wapo watakaobeza kwani serikali imetamka kurudisha!! Lakini kama kweli tunaipenda nchi yetu tufuatilie hotuba za rais na kauli zake kuhusu kuwaenzi wazee hao wa kimila,utagundua nini kilicho nyuma ya pazia.

Hizi ni dalili ambazo kwa uzoefu wa utawala wa CCM zimeanza rasmi kupigiwa chapuo.

Watch out brothers and sisters,hiki ni kichomi kipya tunacho tengenezewa.
 
Back
Top Bottom