Tanzania: Chanzo cha kuporomoka kwa Maadili katika Jamii na Hatma ya Taifa!

Ukiona hivyo ujue polisi wadogo wanatafuta vyeo. Wamezoea ukijiripua unazawadiwa cheo. mfano; polisi waliotuhumiwa na Reginald Mengi kuwa walimchomekea binti yake mihadarati walivyopandishwa vyeo.
 
Inaumiza hasa mtu unapopata taarifa kuwa ndugu yako aliuwawa na watu aliokuwa akifanya nao kazi. Nafikiri kwa kweli tunakokwenda ni pabaya kama serikali haitachukua hatua za haraka.
 
Ni mtizamo mzuri saaaana wa mtoa mada.

Kilio changu siku zote bado nasisitiza mfumo wetu wa uendeshaji nchi umevurugika na ukiona taifa lolote police iko shaghalabagala basi ujue maeneo mengine ndo hayafai kabisaaa. Sasa hapa kwetu tayari polisi haifai kwa matendo yake machoni kwa watu wake. Tujiulize wapi? Kunafaaa endapo bungeni tuuuu matendo yao yanachefua. Na endapo wananchi wangepata fursa ya kuona live kwenye tv matendo mbalimbali yanayofanywa ktk ofisi za umma wananchi wangelia machozi.

Jiulize polisi dar imefanya manyanga na wakwepa kodi kwa muda mrefu huku wakihusisha maofisa wa tra jamii wale tra inawaona mashujaaa hawa polisi ni wakosaji mwananchi mkwepa kodi naye huonekana shujaaa. Suala hili pasi kuprpesa macho mfanyabiashara aliyehusika siku hiyo naye alipaswa kukutana na mkono wa dola.

Ninavyosikia( kama ni kweli) kuna video iliwanasa wale askari wakipokea mlu gula jiuli ze kwanini mpiga picha asimpige na mtoaji fedha lkn huyu mtoa fedha anachukuliwa kama shujaaa na jamii yoteeee hata na yule aliamua kuchunguza na kulinasua suala hili mwisho hatuna budi tusonge mbele kiujanja unja kwani hata suala la mkoani mtwara haki ipo wazi watawala na wananchi waliokwenye neeeema wanawaona watu wa mtwara ni wakorofi lkn ukweli na haki za wana mtwara wanazijua pamoja na yote yatakiwayo kufanywa kwa wananchi ili kuwaondolea karaha za maisha lkn wao hufurahia pale wananchi wanapohisi kuonewa na taaasisi moja kiasi cha kuelekeza shutuma watawala huona na kufurahi wakidhani daima dumu itakuwA hivyo ipo siku
 
Kutokana na ugumu wa maisha yanayotokana na serikali ya CCM. Maadili ya jamii yameporomoka kwa kiasi kikubwa
1.Wimbi la watu kujiuza mitaani,kama chanzo cha kipato kukabiliana na ugumu wa maisha.Na matokeo yake ongezeko la watoto wa mitaani,kasi ya maambukizi ya vvu.Na hii inaongeza bajeti kwa serikali ktk kutunza watoto hawa pamoja kuhudumia wagonjwa wa ukimwi kwa kuwapatia madawa nk.
2.Biashara ya madawa ya kulevya hususani biashara ndogo ndogo kuacha zile za kuanzia 10milion-1bilion ambazo mpaka sasa serikali imeshindwa kulitafutia ufumbuzi suala hili.
3.Udokoaji wa vitu kama simu,pesa,nguo nk.Ili tu auze apate pesa kidogo kukabiliana na ugumu wa maisha.
4.Ongezeko la mimba mashuleni.Hii ni kutokana na umaskini wa wazazi ambao chanzo chake ni serikali ya CCM.Hivyo mtoto(binti) anapokutana na wenzio wanaotoka familia bora,hulazimika kufanya ngono ili apate pesa kidogo ya kununua vitu vitakavyomfanya aendane na wenzio wenye maisha bora.
 
Maisha bora kwa kila mtanzania,
Ari Mpya,
Nguvu Mpya Mpya ,
Kasi Mpya,
Subirini maana kipenga cha mwisho ni dakika 90,

Tusubirie Kauli Mbiu ingine 2015 toka CCM!!!!!!!!!!!!!
 
Kwa mtazamo wangu wanaosababisha kuporomoka kwa maadili Tanzania ni Chadema ambao ndio chanzo cha vurugu na maandamano na kuchochea matusi na udhalilishaji ktk mitandao ya kijamii hasa hapa jamvin'
 
Kwa mtazamo wangu wanaosababisha kuporomoka kwa maadili Tanzania ni Chadema ambao ndio chanzo cha vurugu na maandamano na kuchochea matusi na udhalilishaji ktk mitandao ya kijamii hasa hapa jamvin'

Lusinde,Nkamia na Serukamba unawaweka position gani? Acha kudanganya umma wewe,umaskini uliopo umetokana na ccm na serikali yake.
 
mkuu kila kitu kina positive na negative effects.suala la simu kuuzwa bei che inatokana na kuzidi kwa supply kuliko demand ya simu!.maendeleo ni kama pencil unaweza kuitumia kutoboa jicho la mtu au kuandikia
 
maendeleo yoyote lazima yawe na faida na hasara ila faida uwa nyingi na tunaangalia faida zaidi. ata vyakula vina faida na hasara.
 
Kumekua na mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa vijana miaka hii ya karibuni ukilinganisha na miaka ya nyuma, vijana wameonekana kukosa maadili mema ikiwa ni pamoja na kukosa heshima kwa wakubwa wao,kuvaa hovyo,utumiaji mkubwa wa vilevi hasa aina ya bangi na pombe,kwenda kwenye viwanja vya starehe usiku(clubs)na mambo mengine mengi tu ambayo siwezi kuyataja yote,chakusikitisha nikwamba vijana wengi hawa ni kuanzia miaka 16 mpaka 24!kwa matazamo wangu naamini wazazi kuhusika kwa namna moja au nyingine kama si kubeba lawama zote.sijui likoje hili wana jamii!
 
Mimi kama kijana huwa najiuliza sana kwanini dunia yetu ya sasa maadili yanaporomoka kila siku
kuona uchi hata wa mama mzima kawaida
kwamba ni utandawazi mbona vijijini hakuna Tv,wala neno mtandao kwao waliowengi simulizi lakini uhuni,umalaya,uvaaji nusu uchi nako umeshamiri

HILI JAMBO KAMA KILA MTU HATASIMAMA KWENYE NAFASI YAKE ..........................................................
 
Richard fahamu maisha yanaenda kasi sana yapo mambo mengi sana yanayochangia maadili kuporomoka,
1.Matumizi mabaya ya utandawazi
2.Umaskini
3.Ulimbukeni
4.Ukosefu wa ajira
5.Vijana kua na malengo yasiotekelezeka
6.Wazazi kukwepa na kukimbia majukumu yao ya malezi.
 
Richard fahamu maisha yanaenda kasi sana yapo mambo mengi sana yanayochangia maadili kuporomoka,
1.Matumizi mabaya ya utandawazi
2.Umaskini
3.Ulimbukeni
4.Ukosefu wa ajira
5.Vijana kua na malengo yasiotekelezeka
6.Wazazi kukwepa na kukimbia majukumu yao ya malezi.

elimu duni isiyomjenga mlengwa kujiajiri. Pamoja na sheria mbovu zinazolinda na kuwabagua wananchi. Siasa mbaya kama hii iliyopo hapa kwetu. Nchi kukosa vipaumbele katika kuujenga uchumi.
 
Suala la mmomonyoko wa maadili kwa vijana wa siku hizi ni wazazi pamoja na walezi, hasa hasa wazazi waliosoma.

Katika hali ya kushagaza sana vijana wenye tabia ambazo hazifai katika jamii kama; uvaaji, matumizi ya madawa ya kulevya, n.k, lawama hizi huwa zinawafuata moja kwa moja vijana wa siku hizi bila kuangalia chanzo kikuu ni nini?

Wazazi wa kileo wamekuwa wajikisifu na kujinadi kwamba wao wakati wa ujana wao walikuwa na tabia zuri sana na wamesahau kabisa kwamba wazazi wao waliwaleaje.

Wazazi wa siku hizi kwa mazingira na tabia ambayo wanawajengea kuazia utotoni, ni lazma mtoto awe na uvaaji wa mlegezo, na uvaaji nusu uchi pindi atakapokua.

Wazazi wa kileo, hasa waliosoma na wanaoishi mjini wanafuata tabia na desturi za nchi za magharibi kwa kile wanachokiita 'wanaenda na wakati'.

Mzazi wa kileo yuko tayari kumnyoa mtoto kama Baloteli, wako tayari kumvalisha mtoto kama Rihanna n.k ili mradi tu, na yeye aonekane anaenda na wakati kwa kuiga uvaaji anauona kwenye TV n.k.
 
Kwa hiyi watoto wa wale ambao hawakubahatika kupata elimu ndii wana maadili mazuri? Hivi wanaojiuza kimboka wanatoka osterbay? Vibaka wanaouwawa kariakoo ni wa Masaki?
 
Back
Top Bottom