Tanzania: CCM-Ufisadi, CDM-Ubinafsi niende wapi?

Umeongea vizuri mkuu na uchambuzi wako una afya. Lakini nasikitika thread za kuisasambua magwanda huwa nadra sana kupata positive comments. Humu watu huwa wanapenda useme ''CHADEMA ni kibokooo'', ''Mbowe ana akili sana'' nk. Au vinginevyo uwe unaiponda CCM.
 
nadhani uende mahakamani, kaungane na mtikila ili kuwe na mgombea binafsi halafu utoke kivyako vyako.....
 
Majibu mepesi kwenye hoja nzito ni dalili ya kukata tamaa.Hiki hakijawa kirabu cha pombe FILIPO,NDETICHIA kutema pumba japo sishangai kwa LAT kwani ni mgonjwa wa kudumu wa akili nilikuwa na mtibu pale Muhimbili nadhani bado anaendelea na matibabu.

Rudi Magambani
 
nimependa jinsi ulivyo vichambua hivi vyamba Lakini kumbuka kuwa CCM wamejivua GAMBA na NAPE anazunguka ukeeleza WTZ kuwa CCM ya sasa ni mpya hivyo it better you stay in CCM

Pia CHADEMA kimsingi bado ni chama kichanga comparing with CCM hivyo kinahitaji watu wenye constructive ideas kama wewe ili kukiimarisha ZAIDI nakushauri usihame CHADEMA vumilia na apply strategy mbalimbali ili chama chako kiwe bora in the future

MY NOTE " RUNNING FROM THE PROBLEM IS NOT A PROPER STRATEGY OF SOLVING IT "
 
Umeongea vizuri mkuu na uchambuzi wako una afya. Lakini nasikitika thread za kuisasambua magwanda huwa nadra sana kupata positive comments. Humu watu huwa wanapenda useme ''CHADEMA ni kibokooo'', ''Mbowe ana akili sana'' nk. Au vinginevyo uwe unaiponda CCM.
CCM ni nzuri sana,imetuletea maendeleo makubwa sana kama umeme,ufisadi,ubabaishaji,udhurumaji,ukupe, Halafu ina viongozi mahiri sana kwa ubabaishaji,kama Megawati,six,Mzee wa Magogoni,Nipe,Jeuri na washangiliaji wengi kule kenye jengo la ndiyoooooooooo.
 
I hope will be better for these parties to consider the Nation first, otherwise i strickly recommend for private candidate to be taken into constitutional reforms and for the sake of accountability obvious shall remain in the power of voters themselves.Here the discipline will be invigorated and prolonged as the way of restoring our dignity other than being responsible to the part owned machine for an individual or grop interest.The principle of maintaining the community as they say while they keep on feeding their stomacks is ridiculous to hear.
 
Apolyvaripto,Mkuu katika uchambuzi wako nadhani umetumia zaidi mapenzi yako kuliko kuwa mwandishi huru. Nimekusoma vizuri sana na pengine unaelewa unachokiandika lakini makosa mengi ya kiuandishi yamedhihirisha mapenzi yako.
Kwanza Umeonyesha masikitiko makubwa kwa chama CCM ambacho WATU (viongozi) waliokiharibu lakini ukaonyesha kutokuwa na imani na CDM kwa sababu ya WATU wanaokiongoza. Umeweza kuchambua maamuzi ya CDM yanavyofanyika lakini umeshindwa kuonyesha maamuzi ya chama kipenzi chako maanake haiwezekani chama kizima kufikia maamuzi ya Ufisadi pasipo kuwepo shinikizo la mtu au genge fulani..Pengine labda nikufahamishe kinachoendelea CDM zaidi kwa sababu mimi nimetazama matatizo ya chama kwa utafiti tofauti.

CDM ni chama ambacho watu wengi wameingia kama oppoturnist tofauti na CCM ambayo uongozi wake umekuwa wa kurithiana. Watu wengi wanaitazama CDM kwa sababu ya Mbowe kurithishwa na Mzee Mtei, lakini kama utatazama haya CCM utaona kwamba watoto, wakwe, majomba shangazi na kadhalika ndio wameshika mnafasi kubwa za uongozi ktk ngazi tofauti za kiserikali na taasisi zake. Lakini upande wa CDM, Mbowe ndiye amekuwa mazungumzo makubwa ya wanaCCM au wapinzani kwa sababu kila anayejiunga na CDM ni ktk kundi la wale Wonna be!..kuna nafasi kubwa ya kujitengenezea jina CDM kuliko vyama vingine na mgogoro mkubwa wa CDM umetokana na sifa ambazo chama kimejizolea..

Matatizo ya Uhuru wa kushawishi ndani ya CDM umekuwa somo zuri sana la siasa kwa watu wasiojua siasa. Watu wengi waliojiunga CDM wamefikiria hiki ni chama chenye mkusanyiko wa itikadi, nadharia na kila wazo la mtu makini lazima likubalike maadam mtu huyo ana mtazamo tofauti. Mkuu wangu haiendi hivyo, chama kina vision kupitia itikadi yake wameunda mwongozo ambao pamoja na mawazo tofauti ni lazima ujumbe uwe kupitia imani tangulizi. Kwa maana kwamba huwezi kudai unaitangaza dini ya Kikristu hali unapinga kwamba - Yesu sio mtoto wa Mungu ama Yesu sio Njia!..

Tatizo kubwa linalowakuta wafuasi na viongozi wa CDM ambao wamejiunga na chama wameshindwa kuelewa kwanza taratibu na mila za chama hiki isipokuwa wanataka kulazimisha yanayofanyika CCM yafanyike pia CDM hali wanajua fika wameshindwa kujitokeza CCM kwa sababu -They don't belong there..Na wamekuja CDM wakitegemea imani zao ndizo ziwe msingi wa taratibu za kuendesha chama. Ni sawa na Muislaam anayeingia Ukirstu akitegemea kesho atakuwa Padre kwa sababu tu hutangaza jina la Yesu hadi vituo vya mabasi...

Matatizo ndani ya CDM yanaletwa na watu wa kuja ambao wanategemea kuwa wabunge, kuingia makao makuu ama wahusishwe ktk ngazi za juu za uongozi haraka iwezekanavyo kwa sababu ya usomi wao. Na hali hii imejengwa kutokana na kwamba wakitazama mlolongo wa wafuasi wa chama au viongozi wote ni wa Kuja na pengine hawana elimu kuwazidi hivyo njia bora ni kutunisha misuli kuonyesha umahiri wao bila kufahamu kwamba kwa kufanya hivyo unaleta mgogoro ndani ya chama.

Na lipo kundi jingine ambalo wao kazi yao ni Unafiki, kujipendekeza kaa ilivyo kawaida ya Wadanganyika kwa malengo yale yale ya kuonekana wako mstari wambele ili wapate kushika wadhifa ama uwakilishi.Ni rahisi sana kusema Chadema kuna Udini ama Ukabila kama hutapenda kutumia akili zako vizuri.. Kwa sababu tazama Uongozi wa CCM na hasa mkoa wa Kilimanjaro. Hesabu namba ya wabunge wake kisha nambie ni wangapi ni Mawaziri? nadhani wote isipokuwa Mama Anna Kilango na hakuna mkoa mwingine wowote wenye wabunge mawaziri karibu wote.. na ipo mikoa ambayo haina waziri wala Naibu waziri je huu utasema ni Ukabila umetumika au?..Kwa hiyo sisi Watanzania ni watu wa kutafuta mchawi na siku zote tunashindwa kutazama kitulacho kii nguoni mwetu (kunguni) isipokuwa kutazama nje na nafsi zetu ili kuficha uchafu wetu wenyewe.

Mbowe, Dr.Slaa, Rostam , Lowassa wote hawa wamechaguliwa na wananchi na ndio wao wanaokisiwa kwa mabaya yote ili hali baina yetu sisi wenyewe ndio tumewachagua na kuwapa nafasi hizo...Again hakuna mtu anayekiendesha CDM mkuu wangu ni chama kilichompa nafasi ya kugombea iwe ubunge au Udiwani. Kama chama kingewaacha nje iwe wangetafuta kuingia vyama vingine ambako sidhani kama wangepokelewa labda huyo Mrema na Mbatia. Unapowataja Lissu, Lema, Mbowe, Slaa, Mnyika, Shibuda na wenigne kuwa na uwezo wa kushinda nadhani unapoteza mantiki nzima ya chama ni Imani na hujengwa na watu.

Sasa kama huyo Lissu, Mbowe, Lema na wengine woote wasingekuwa na imani sidhani kaa wangeweza hata kusimama kugombea, hivyo wasingeweza kushinda. Ni imani yao inayowasukuma kuwepo CDM na wakihamia vyama vingine kwa fikra za wao kuwa sababu sii ajabu nguvu hiyo hawatakuwa nayo tena..Na nakuhakikishia kama sii kampeni za Sangara na maandamano yaliyotangulia hawa wote wasingejulikana. CUF walisema hivyo hivyo uchaguzi wa mwaka 2005 wakiwa na matumaini ya watu wao kuchaguliwa tena kutokana na Umaarufu wao lakini CCM iliwapiga chini vibaya sana kwa sababu walisahau kuelekeza nguvu zao bara kama chama kwa kutegemea watu na CCM kwa kutumia Udini iliwamaliza...
 
Update Maswali na Majibu kutoka gazeti la FAHAMU la leo
1.Unaelezeaje siasa za vyama vya upinzani nchini kwa ujumla, unadhani vinalenga ukombozi wa kweli kwa wananachi ama ni maslahi binafsi?



Kisandu; Siasa ya vyama vya upinzani nchini ni siasa isiyo kuwa na mshikamano, historia inajionesha kuwa kipindi cha Mh.Mrema NCCR-mageuzi ilipokuwa na nguvu vyama vingine havikuwa tayari kukiunga mkono ili chama hicho kishinde, na kipindi chama cha TLP kilipokuwa na nguvu pia vyama vya upinzani havikuwa tayari kusapoti chama hicho ili kishinde, vilevile kipindi chama cha CUF kilipokuwa na nguvu vyama vya upinzani bado havikutaka kuonesha ushirikiano wa kutaka ushindi na kipindi chama cha CHADEMA kilipokuwa na nguvu vyama havikutaka kuisapoti. Nahii yote inasababishwa na maslahi binafsi, moja chama kimoja kikiungwa mkono na kikashinda hicho ndicho kitakuwa chama tawala na jina la chama hicho litakuwa kubwa na vyama vingine vitamezwa kabisa hata kama viongozi wake watakuwa na nafasi katika serikali na hii ndio inayosababisha vyama vya upinzani kushindwa kuungana.Pia kila chama kinajiona kina nguvu kuliko chenzake hasa kutokana na maslahi binafsi, kwa mfano CHADEMA wamekuwa natabia ya kuviambia vyama vingine vinatumika na CCM na kuviita CCM B wakati haohao ndio wanaongoza kwa kutumika na CCM, mfano mzuri mwenyekiti wa kambi ya upinzani alikataa gari la serikali na nyuma ya pazia akalifata. Mh. James Mbatia alipo ibuka na hoja yake ya mitaala ya elimu na kuamua kutoka nje kwa kutorizishwa na Spika, hapo ndipo unafiki wa vyama vya siasa ulipooneka baada ya CHADEMA, CUF,TLP na UDP kuungana na Mbatia kutoka nje wakijiadai wanasapoti wakati haohao wanapenda kuwaita wenzao CCM B na walifanya hivyo si kwa nia njema bali kwa kuogopa kumezwa kisiasa, pamoja na yote CHADEMA walitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa kutakuwa na mkutano wa hadhara na maandamano ya vyama vya upinzani TEMEKE kupokea wabunge wa upinzani lakini kinyume chake chama cha CHADEMA kilitumia mgongo wa vyama vya upinzani hasa hoja ya mbatia ili kupata watu wengi kwenye mkutano tena hata vyama vya upinzani havikupewa taarifa yoyote kuhusu mkutano huo. kwa hali hii vyama vya siasa havina nia ya dhati ya Ukombozi wa watanzania bali vinalenga maslahi binafsi na sio kuiondoa CCM madarakani. Ushauri wangu katika hili kama serikali ikibadilisha mfumo, sheria itakuwa nzuri ili vyama vikiungana vyote vinatumia jina moja na hii ikifanikiwa itakuwa ni rahisi kuiondoa CCM.Na kama hii haitawezekana basi vyama vikubaliane kuachiana majimbo na kusapotiana pamoja na kupendekeza mgombea urais anayekubalika, tukifika hapa tutashinda na ukombozi wa kweli utapatikana.


2.Ulikuwa Chadema na kuamua kujiunga NCCR-Mageuzi, ni suala lipi kubwa lililokufanya uondoke Chadema?



Kisandu; kuna mambo mengi tu naomba niyataje:
1.Ubaguzi wa kidemokrasia yaani sisi tunajenga chama kwa nguvu zetu na pesa zetu halafu M4C wanaoshiriki ni ndugu zao na wengi wao wanatoka kaskazini na hawana hata uwezo.
2.Nimekuwa katibu wa BAVICHA mkoa wa Tanga lakini makatibu hatushirikishwi vikao vya kamati tendaji kwa mjibu wa katiba, bali wanavunja katiba na kuwaita wenyeviti ,ukihoji unaambiwa wewe ni nani kwenye chama? tutakufukuza mda si mrefu au tutakuchafua.
3.Madiwani wanapopingana na Dr.Slaa wanafukuzwa kwenye chama na hata viongozi wa chama mikoani wanafukuzana kwa maagizo ya walioko juu na hii ni kutokana na hofu ya kuzidiwa vipaji na viongozi wa zuri wa mikoani.
4.Chama kinapingana na katiba ya nchi ibara ya 18, ambapo kiongozi au mwanachama akionesha nia ya kuwania Urais anaandamwa na kuitwa majina mengi mara Masalia, anatumika na CCM, katumwa kuvuruga chama n.k na kuanza kutafuta njia ya kukufukuza.
5.Chaguzi ndogo za madiwani wanakuja wakurugenzi wa taifa na watu wao na kuwatenga viongozi wa wilaya halafu wakishindwa wanasema viongozi wa wilaya walinunuluwa na CCM.Kitu ambacho ni unafiki na ninjia wnaitumia kula ruzuku.
6.Niliandikiwa barua ya kufukuzwa chuo na hawakujitokeza kunisaidia baada ya Godbless Lema kuja chuoni kufungua tawi ambapo mimi nilikuwa ndiyo mwenyekiti na chuo kukereka na ujio wa Lema na ndipo nikapewa barua lakini wanasheria walinisaidia mpaka nimemaliza chuo.
7. Chama hakithamini mchango wa waliokiinua chama na kuanza kuwafukuza badala ya kuwajenga.
8. Wanajikopesha mamilioni ya ruzuku huku sisi tukitaabika kujenga chama kwa kuharibu magari na pikipiki zetu.
9. Upendeleo katika upangaji wa wabunge wa viti maalum, katika jimbo la Mbowe lina viti maalum wawili wakati mkoa wa Shinyanga wenye wabunge wengi una viti maalum mmoja tu.


3.Unaelezeaji mapokezi yako ndani ya NCCR-Mageuzi? Unadhani huko ndio salama zaidi katika safari yako mpya kisiasa?



Kisandu:Mapokezi niliyofanyiwa NCCR-mageuzi ni mazuri sana maana viongozi wananipa sapoti ya kiutendaji na tunazidi kukijenga chama tena kwa mda mfupi tu niliofika NCCR-mageuzi kimepata nguvu kutokana na kazi kubwa ninayoifanya ya kukirejeshea imani kwa wananchi maana ni chama kizuri kwa ukombozi ukifuatilia historia ya uanzishwaji wake.Na mda si mrefu tutakuwa na ziara wilayani Kahama ambako ndio nyumbani kwetu na mapokezi makubwa sasa yanaandaliwa na hapo ndipo tatoa msimamo wangu ama 2015 tagombea Urais au ubunge jimbo la kahama.Kimsingi siasa ni maisha ya kila siku tunayoishi hivyo NCCR-mageuzi ni mahali papya kiasa na sehemu ya kujijenga zaida kisiasa.

4.Umekuwa na tuhuma nyingi ndani ya chadema ambapo ulikuwa ukitajwa kutokuwa mwenzao, unawezaje kuwahakikishia wananchi kwamba uliyokuwa ukiyafanya ndani ya Chadema yalilenga kutaka uhuru wa kweli?



Kisandu: Wale wanaonituhumu ndio wale tunao penda kuwaita wanachama wa helkopita ambao ujinga ukisemwa na kiongozi wajuu wanaamini bila kuhoji.Mimi niligombea ubunge jimbo la Lushoto ambako si mzawa wala mkazi wa wilaya hiyo bali nilikuwa masomoni chuo kikuu, sasa chama kwa kuhofia uwezo wangu na nguvu yangu wakaanza kuwatumia viongozi wa wilaya ya Lushoto na mkoa mzima wa Tanga wafanye kila linalowezekana nifukuzwe chamani, wakati wanapanga huo mkakati tayari taarifa kwa vijana wangu zikanifikia namimi nikawa na jipanga kwa lolote. Mbaya zaidi nilipotangaza kugombea urais mwaka jana 2012 hapo ndipo nilipoongeza chuki kwa chama Taifa na kuwatuma akina John Mrena(mkurugenzi wa halmashauri na bunge) na Bazil Lema(katibu wa mkoa wa kilimanjaro) kuja Lushoto kuniperereza eti nani ananisapoti? hivi kutangaza tu nia mpaka usapotiwe? hapa ndipo changamoto nyingi zilizidi kuibuka mara nimepewa pesa January Makamba mara Kigoda ili mradi tu kunichafua. Mbaya zaidi mimi nina kundi kubwa sana ambalo chama wanaliogopa.


5. Ni mambo gani mpaka sasa mazuri uliyokuwa ukiyaona Chadema lakini ndani ya NCCR hayapo? Unakishauri nini chama kutokana na mambo hayo?



Kisandu:Kwa kweli kila chama kina itikadi zake, itikadi za chadema haziendani na matendo wanayoyafanya lakini ona NCCR-mageuzi ilivyobadilika sasa na mda si mrefu tunaanza kujenga umoja wa watanzania na si kuwagawa watanzania kama Chadema wanavyofanya.


6. Kabla ya matatizo yako na Chadema, uliwahi kuipenda ama kuamini kwamba siku moja utajiunga na NCCR-Mageuzi au ni wazo lililoibuka kutokana na kukosa pa kwenda?



Kisandu: Sikuwahi kuwaza kuwa NCCR-mageuzi ila kwasababu ni kijana kutokana na matatizo ya kufikia mpaka kutishiana maisha kisa Urais na kutafutwa sababu za kunifukuza ilinibidi nisome katiba za vyama vyote ndipo nikaona NCCR-mageuzi panafaa sana maana lengo langu ni ukombozi wa watanzania nakama ningetaka maslahi ningeshaenda CCM mapema sana.


7. Ni kitu gani kilichokuvutia NCCR-Mageuzi ikiwa hulka ya kufukuzana ipo mfano ukiwa ni Davidi Kafulila-Mbunge wa Kigoma Kusini?







Kisandu:mmmmmmmhh, imebidi ni cheke kwanza, ya Kafulila mwachie Kafulila na kamati iliyohusika maana wako kwenye majadiliano ya kusameheana na hii huenda ikawa ni neema pia ya chama kufikia mafanikio ya kuwakomboa vijana. Mimi huwa siangalii nani kafanyiwa nini bali nachoangalia je ukombozi wa watanzania utatimia nikiwa mahali gani.Kikubwa kilichonovutia ni ile itikadi yao ya UTU na kweli huku kuna UTU.


8. Watu husaka uhuru wa kuzungumza na fikra, je unadhani ndani ya NCCR kuna demokrasia ya kweli? Kwa nini?



Kisandu: Demokrasia ipo kaka, tangu nimefika NCCR-mageuzi nimekuwa na uhuru wa kuongea tena nimefululiza kufanya kazi na watu wa media kwa kukijenga chama. Nahuwezi amini chochote nachokifanya Katibu Mkuu wa chama hunipigia simu na kunipongeza na wakati mwingine kunijenga kwa kunikosoa, akina Sungura na wabunge wetu wote wananipa ushirikiano mkubwa sana, vuta subira mikakati endelevu ya PAMOJA TUTASHINDA ikonjiani.

9. Unawezaje kuyaelezea malengo yako ndani ya NCCR-Mageuzi na ushirikiano unaoupata ndani ya chama hicho?



Kisandu: Lengo langu kuu nikuja kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania hapo mbeleni na hasa kama Katiba ya nchi ikishusha umri na uhakika 2015 nitakuwa mgombea wa Urais kijana kuliko wagombea wote na nitashinda, maana vijana ndio tunaotaabika na ndio tuko wengi sana. kwani tunahitaji Rais ambaye hajawahi kuwa Mbunge wala waziri kama Kisandu ili tufikie malengo halisi ya ukombozi wenye vyeo tumeshajua madhaifu yao.Ushirikiano naopata ni mkubwa sana na ndio maana wakanipa cheo cha katibu wa uhusiano na uenezi Taifa, kitengo cha Vijana wa NCCR-mageuzi.Mungu yupo, malengo yangu yatafikiwa tu.


10. Chadema ni chama kikuu cha upinzani, umeshawishikaje kutoka katika tunu hii mliyojenga pamoja kabla ya 2010 na kuwaacha wengine wanufaike nayo peke yao, huoni kama umejidhulumu?



Kisandu: Ni kweli inauma sana, lakini mwanasiasa wa kweli anatakiwa kusimama sehemu yoyote ile na akaonekana tu hata kama chama kiko vipi, na kama nilivyosema awali ningekuwa na shida ya pesa ningeenda CCM, lakini shida yangu ni kuokoa umasikini wa watu wangu(watanzania) na ndio maana nikaja NCCR. Acha wanufaike maana mimi siangalii masilahi bali ukombozi, na kuna siku watanzania watajua ukweli juu ya uongo wa Chadema jinsi wanavyo uhadaa umma wa Tanzania na tena kwa kuwachangisha watanzania mapesa kupitia M4C wakati wanapewa ruzuku na serikali ambazo ni kodi za wananchi.

11. Kukimbia chama kunaashiria kukosa uvumilivu wa kisiasa, hili unalizungumziaje?



Kisandu: Kwa Tanzania bado hatujawa na vyama makini vya upinzani ndio maana Godbless Lema alikuwa TLP tena aligombea ubunge kwa chama hicho na 2010 akahamia Chadema nakina Dkt. Slaa alikimbia CCM na kadi yake akenda CHADEMA, kina Mrema wakatoka NCCR-mageuzi wakaenda TLP, Wassira akatoka NCCR akenda CCM leo waziri na wengine wengi, tatizo hapa wanashindwa kujua kuwa mimi ni kijana na nimeanza siasa ningali mdogo na hivyo mapambano yangu ni makali sana kwasababu ninatafuta demokrasia ya kweli na mwisho wa siku watanzania watakuja kujua nilikuwa na maanisha nini, ukitaka kujua siasa zangu msome sana mwanafalsafa kijana msenegali CHEIK ANTA DIOP ambaye ndiye model wangu mkuu aliyepambana bila kuchoka. vyama vya siasa Tanzania ni vya watu hivyo haina haja ya uvumilivu maana wewe unataka Urais mpaka upate baraka ya mwenyechama ndio maana Zitto atahangaika sana kwa Chadema na malengo yake hayatafikia.

12. Ni mwanasisa gani nchini hafai kuwa mfano wa kuigwa? Kwa nini?



Kisandu: Dr. Slaa, ndiye mwanasiasa namba moja anayekula haki ya vija na wijukuu.Huyu mzee bwana hajifunzi kabisa maana ya uongozi, mwenzake Papa Benedikto kaamua kujiudhuru Upapa kwasababu ya Uzee na kasema uongozi(upapa) ni bora sasa wapewe vijana,na hata huko Uganda mzee Besigye kiongozi wa chama kikuu cha upinzani uganda mwaka jana alikataa kugombea uenyekiti wa chama na kusema nawaachia na wengine nao wapambane sasa hawa wazee watanzania hawako tayari kuwaachia vijana kuongoza Taifa kwa mtindo huu hatutapata ukombozi wa kweli kama vijana tunabaniwa.Wazee hawakubali kukosolewa hivyo wanakosa uzalendo wa kweli.


13.Lengo lako ni lipi ndani ya NCCR-Mageuzi?



Kisandu: Lengo langu kuu ni kuwa Kijana mfano wa kuigwa na vijana wote nchi nzima, na hili utaona vijana wengi wanatoka Chadema wanaenda CCM lakini hebu angalia mimi nimpinzani halisi na ndio maana nilizaliwa Chadema sasa ninakulia NCCR-mageuzi kufikia malengo halisi ya ukombozi wa kweli.Na nitagombea Urais na hii ni dhamira yangu mpaka Mungu atakapochukua pumzi yangu.

14. Unadhani kwa sasa ndani ya chama chako, kuna udhaifu gani ambao ukifanyiwa kazi unaweza kukifanya chama kuwa na nguvu na hatimaye kuwa kiongozi wa upinzani kama Chadema?



Kisandu: Hakuna udhaifu ila kulikuwa hakuna watendaji wakusukuma wengine wajitume zaidi ya wabunge, na ndio maana sasa hivi tunajiaandaa na mkakati wa kukamata majimbo mengi zaidi 2015 pamoja na kuingia ikulu kwa kishindo 2015.

15. Ukiachana na wanasiasa kutoka ndani ya chama chako, ni mwanasiasa gani unayemuona kuwa makini zaidi na anakuvutia?



Kisandu: Kwa Tanzani bado sijaona kabisa. Na ndio maana nataka kuwa model wa vijana hapa nchini.




Nakushukru kwa maswali yako mengi sana takribani 15, na nimeyajibu kwakufuata Katiba ya nchi ibara ya 18. Aksante.


DEOGRATIUS KISANDU.
MWANAHARAKATI WA DEMOKRASIA YA KWELI NA HAKI NA USAWA WA KITANZANIA na


14/02/2013
 
Sio lazima wote tuimbe, wengine tubaki mashabiki jamani......nyie kina Kisandu tafadhali msiwachanganye raia, maana wameanza kuelewa
 
Yaani sarakasi zote anazofanya nikuutaka Urais wa JMT. Kweli hii ofisi imedharaurika sana.
 
Hivi huyo Kisandu ni mke wa Zitto? Mbona anamwaga povu hivi mithili ya mke anayebembeleza penzi kwa mumewe?!!!
 
Fahamu ni Gazeti la Chama cha Wananchi CUF linalotumika kuleta chokochoko Chadema.Kila kitu kinafahamika.
 
Kisandu kamwambioe aliyekutuma kachemsha,jungu halina mashiko....mnanunuliwa kwa vijisenti vidogo mnaongea bila mpangilio,asa kweli ulitegemea mtu akuamini kwa usaliti kama huu ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom