Tanzania: CCM-Ufisadi, CDM-Ubinafsi niende wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: CCM-Ufisadi, CDM-Ubinafsi niende wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by apolycaripto, Jul 23, 2011.

 1. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Nchi imefika njia panda ambayo hatima yake kisiasa si kueleweka bali kutabilika.Chama CCM kilikuwa na mwitikio mzuri na watu walikipenda hasa kwa kubebwa na historia yake.Uzalendo ndani ya chama na NChi ulipotea baada ya Mwinyi kushika hatamu,japo Mwalim alisaidia kutokukua kwa kasi kwa uhasi na kipindi cha Mkapa siri nyingi zilifichika hivyo maovu mengi kutendeka na aliyehoji hakupata nafasi ya kupumua.

  Hali ilikuwa mbaya baada ya Jk kuchukua Nchi,ni kweli alikuwa na makundi yake ambayo yalidumu kwa muda mrefu toka 1995 na kamwe hakuwahi kuyazika zaidi ya kuhisi yatapotea yenyewe pindi akiwa madarakani.Uwazi na kujipambanua kama mtu wa Watu,imesababisha aliyoficha Mkapa sasa yakawa nje pamoja na makundi aliyoyajenga kutanuka zaidi.JK ameweza kunishawishi kuwa ni Rais asiye makini,hana mipango kabla ya maamuzi,vikao vingi hasa vya chama humkuta na kuviendesha pasipo kuviandaa na mengi anayopaswa kuyatolea maamuzi hasa katika chama huwa hana taarifa nayo.

  Hii ni dosari kubwa aliyonayo,kuendesha Nchi bila mipango,uwezo mdogo kwa sababu waliombeba katika mtandao (Lowassa,Membe,Sitta,Makinda,Rostam n.k) kwa kiasi kikubwa ndio wamefanikiwa kuyumbisha Nchi hii.JK hana tafiti pia ni mvivu wa kusoma na pengine si good communicator zaidi ya kupenda kupokea habari za 'majungu' yaani from informal source na hasa zinazowahusu watu binafsi na si kwa maslahi ya Taifa.

  CCM leo imekuwa taabani kwa ajili yake,chama kimetoka katika hali ya 'kizuri cha jiuza' kuelekea kwenye 'kibaya cha jitembeza' inasikitisha sana.Tazama Nape anavyohangaika sasa,huku waliokiaribu wako kimya na kushindwa kuungana naye kujisafisha.Wanachama wameibia Nchi mali nyingi watakazo,Watumishi wa serikali wameiba tena sana na leo wengi wao wanamiliki mali za kutisha na wengi tunawajua kwani hakuna mali iliyo angani zote ziko ardhini tulipo hata kama ni ng'ambo.

  Leo hii chama kinataka kurudisha imani huku ndani kimepasuka ''sijui'' matokeo yake kwani probability is high to loose.

  CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CDM).

  Sio kipya kwa maana ya kuzaliwa kwake,kwani kimezaliwa katika vipindi vya karibu baada ya NCCR,NAREA,CUF,UDP na vinginevyo.Asilimia kubwa ya watendaji wake na waasisi ni wanaCCM na wengine toka vyama vingine.CDM imekua baada ya anguko la vyama vingine hasa NCCR,TLP,CUF na pia uovu wa CCM.

  Viongozi wa CDM wengi kwa kutotaka mabadiliko,wanajalribu kukijenga chama katika sura ya kitaifa huku wakinyima fursa ya mawazo tofauti juu ya muelekeo wa chama.Sauti,ama tamko limekuwa la upande mmoja maarufu kama ''makao makuu'' na si katika ushirikishwaji kupitia ngazi za chini.

  Chama hiki kwa sasa kimekuwa na muelekeo wa udikteta ambao msingi wake ni ''ubinafsi''.Haiwezekani chama kutegemea sana vyombo vya habari,tena mtu mmoja kutoa matamko hata yale ambayo yanahitaji mawasiliano ya ndani kabla ya kuwa aired publically.

  Tukubaliane kuwa umaarufu wa CDM umetokana na watu binafsi na si Chama kwani Lissu,Lema,Mbowe,Slaa,Mnyika,Shibuda nafasi zao za kuwa na wabunge hazikutokana na umaarufu wa chama.Hii na maanisha watu hawa wangepata fursa hata TLP au CCM wangeweza kuwa wabunge pia.

  Dhana ya CDM ya kuwa hakuna maarufu kuliko chama in reality doesn't work kwa sababu kwa sasa tunasema bila Slaa umaarufu wa chama usingekuwa hivi sasa kwani kugombea urais kulimpa nguvu ya kusikika,kuzunguka na pengine watu kuanza kusikia CDM zaidi.Leo hii viongozi wa CDM hasa Wabunge wamepata kura si kupitia wanaCDM tu bali wengi ni wasio na vyama ama wafuasi wa CDM.Ushahidi tazama idadi ya kura walizopata wabunge wa CDM Nchi nzima na idadi ya Wanachama wa CDM siku moja kabla ya uchaguzi.

  Migogoro mingi ndani ya CDM inakuzwa kwa sababu ya ubinafsi,huwezi kuongoza chama kama taasisi binafsi kwa maana influence inakuwa ndani na nje ya kamati kuu.Slaa ni mbishi na mpenda hoja yake kupita ata anapokuwa ndani ya kamati kuu,anayeweza kumcontrol ni Mbowe peke yake.Hapa tunapotolewa matamko eti kamati kuu imeamua hivi na vile si kweli bali kuna mtu kaamua na wenzie wamefuata.

  Wabunge na viongozi wengi wa CDM kwa sasa wamejengwa mazingira ya uoga na hofu kwa kudaiwa uwepo wao ni kutokana na chama.Tazama Madiwani Arusha,Shibuda na wengineo aibu tupu,watu wamefikia hatua ya kuwa ''wanafiki'' kwa maani ya funika kombe mwanaharamu apite.Viongozi disign ya Ephata Nanyaro ni wa kuogopwa sana,huyu hafai kupewa madaraka makubwa zaidi ya aliyonayo na pengine ndiye kiini cha chokochoko kwani alikuwa anakula pande tatu (madiwani wenzie,CCM na Makao Makuu CDM).

  Shibuda hawezi leo kugeuka ''bundi'' ndani ya chama huku alipokelewa kwa vifijo,hoihoi na nderemo kipindi anaasi CCM.Shibuda si mgeni kwa WanaCDM,kwani anafahamika kwa tabia,sura na matendo.Ni dhahiri ubunge wake ulikuwa faraja kwa CDM kwani umeongeza idadi na mapato.

  Leo anadaiwa anakiuka ilani na katiba ya chama,eti ni magamba ooooh mamluki hapa kuna tatizo tena kubwa ndani ya chama hiki.Shibuda kama alivyokuwa CCM hajabadilika na hata CDM atagombea nyadhifa kama uenyekiti,ukatibu mkuu kwani hivi kwake ni vidogo kuliko vile alivyokuwa akigombea CCM.Iwapo hofu ni hii ya kukinga kuliko kutibu basi afukuzwe.

  Zitto Kabwe alikuja kuonekana mbaya pale alipotamani kama ilivyotokea kwa Chacha Wangwe (marehemu).Hii si demokrasia bali ubinafsi uliopitiliza wa kutaka waliopo wadumu na kusikika siku zote,waheshimiwe kama wanahisa na wengine wabaki watwana kama waajiriwa.Mallah,leo kumtaja Slaa waziwazi anaonekana tishio ndani ya chama,nasema mfukuzeni pia ili chama kiendelee.

  Kimsingi chama hiki kimekua,kimeoa na sasa kinasubiri kufa.Hakiwezi kukabiliana na mbinu chafu za CCM kwani kama sasa kinalia CCM kuwa inakivuruga kwa kuwapa rushwa baadhi ya madiwani na viongozi wake,ni dhahiri hakitafika mbali kwani CCM itakimaliza tu.

  Tutambue watanzania/wananchi hawana desturi ya kupenda vyama vyenye migogoro isiyokwisha.Issue ya Arusha ikimalizwa vibaya itakiangusha chama na si Arusha tu,sumu hii itaenea Nchi nzima.

  CDM kiko katika hali mbaya zaidi ya hiki cha CCM ambacho kinamihimili mingi ya kukisaidia kuishi lakini CDM sawa na mtoto yatima.Nafikiria niende wapi?
   
 2. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Kafie mbali....!
   
 3. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nimependa uchambuzi wako umezingatia misingi ya impartiality kwa kiasi fulani na kwa sehemu fulani ninakubaliana nawe but kuna mambo ya msingi ambayo hatuwezi kuwa in agreement (kama hapa unaposema CDM kiko katika hali mbaya zaidi ya hiki cha CCM ambacho kinamihimili mingi ya kukisaidia kuishi lakini CDM sawa na mtoto yatima). Cha msingi ni kubaki hapo ulipo kwanza ili ukabiliane na changamoto zinazokukabili kwani kulikimbia tatizo si kulitatua.
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,766
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  baki ccm mkuu ibadilishe MAGAMBA HAYO, nadhani umesahau ccm wanasifa zoote hizo!
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  go to hell , i can smell gossiping

  this topic is frail
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  nenda polini kapasue mbao...
   
 7. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Majibu mepesi kwenye hoja nzito ni dalili ya kukata tamaa.Hiki hakijawa kirabu cha pombe FILIPO,NDETICHIA kutema pumba japo sishangai kwa LAT kwani ni mgonjwa wa kudumu wa akili nilikuwa na mtibu pale Muhimbili nadhani bado anaendelea na matibabu.
   
 8. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 738
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Hoja yako ni mzuri, hata mimi hicho kitu nimekiona. Mfn.Matamko mengi ya cdm yanatoka kwa mbowe au slaa hata ambayo sio ya lazima. Ukiangalia CUF taharifa nyingi anatoa mtatiro na sio prof. Au maalim. Issue ya Arusha wakienda vibaya madhara yake yatakuwa makubwa.
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kumbe kuna wagonjwa humu!
   
 10. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Rudi CCJ, mkaifufue.
   
 11. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Jaribu kifo!
   
 12. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  good!ni sahihi na ushauri wako una faida sana ktwa cdm.kuhusu mahali pa kwenda nakushauri uende Ppt maendeleo
   
 13. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mawazo yako si mabaya lakini usisahau kuwa cdm na ccm wako vitani kwa hiyo kushambuliwa kwa cdm na kwa mbinu kama za kuwahonga baadhi ya vionozi wake ndo silaha kubwa kabisa ya ccm. Kama cdm wakiweza kuithibiti hii silaha basi ni wazi cdm kitaishi na ccm itakufa.


  Unapowalaumu cdm unakosea unashindwa kuelewa kwamba wako vitani wanapambana na kuna wakati watapoteza wapiganaji baadhi kama tunavyo ona sasa madiwani wa Arusha na huko mbeya.

  Kinachotakiwa ni kwa chadema kutambua kuwa wako kwenye vita na kama wanagundua mapema mbinu za adui ni kufanya maamuzi makini kwa haraka ili kuzuia adui kuendelea kuua.


  Mimi kwa mtazamo wangu cdm inakua na itaishi maana inao viongozi wenye moyo na wana nia njema ya kuelekea mahali fulani.
   
 14. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Mtatiro ni nani Cuf na Dk. Slaa ni nani CHADEMA?
  Nakushauri uende CCJ au UDP.
   
 15. L

  LAT JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Labeled : JF Hate Preacher

  instrumented by infidelity
   
 16. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sidhani ulitegemea wana magwanda wakuunge mkono. Fact is UKO SAHIHI zaidi ya asilimia mia! Nimekuwa nikitafuta watu wenye mawazo kama yako muda mrefu. Nadhani future of TZ iko kwa watu kama nyie.......! CCM IS CORRUPT ............and........... CDM is DIVISIVE!
   
 17. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Kweli haitaji reserach ya miaka hapa unaweza kutoss na kutambua vijana wetu vichwa vyao ni vya namna gani!my comments relied on retionally views on political parties stand lakini mlengo wa kushoto umekuwa na matusi mengi,kejeli up on me.Arafat si kupingi katika wazo lako lakini inanipa mashaka what if CDM wakikupa Uwaziri,will you be different from these lunatic ideas?
   
 18. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani sasa hivi uko wapi? Malawi?
   
 19. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nenda Libya!
   
 20. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mataputapu!
   
Loading...