Tanzania Breweries (TBL) na ubaguzi wa kutoa dili za marketing kwa wasanii wa Arusha pekee

Mtuflani Official

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
1,936
4,347
Matangazo mengi ya beer za TBL wanapewa watu wa Arusha. Hii kitu imekua inaendelea kwa muda sasa. Castle Lite wanawapo deals Weusi (wasanii kutoka Arusha). G-nako alifanya nyimbo kufanya promotion ya beer ya Kilimanjaro na pia alipewa ubalozi wa beer ya Kilimanjaro. Castle Lite Unlocks ya South Africa walipelekwa Weusi na mabalozi wa Castle Lite ni Weusi. Adam Mchomvu (mtangazaji kutoka Arusha) pia ni balozi wa Castle Lite.

Mimi Mars (sio hata maarufu sana) amepewa ubalozi wa Flying Fish (kinywaji cha TBL) kwa sababu tu ni mtu wa Arusha. Kenedy the remedy mtangazaji kutoka Arusha ni mabalozi pia wa Flying Fish. Tatizo TBL ni nini?

Mbona Serengeti Breweries wao deals za matangazo wanawapa Watanzania wote kama tulivoona kwenye Guiness na Serengeti Lite.
 
Hilo nilikuwa naliwaza Sana kitambo

Nilifanya kautafit kangu kadogo pale ilala nukagundua haya

Aliyepo kwenye kitengo Cha marketing n mkaskazini hvyo n ngumu Sana kwa mgogo Kama jobu kupata deals za tbl

Sasa wale wanaongea lugha 1 ile 10% inagawika vizuri bila kwere



Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app

Usiongee kama unaongea na vijiwe vya kahawa, mkuu wa marketing ata sio mtanzania.
 
Kila kampuni ina namna yake ya kufanya kazi sio anachofanya serengeti na tbl afanye.

Ukija swala la deal la flying fish, deal kama deal ilipewa clouds na kipindi cha xxl kilipewa hadhi 1 ya ku push kuhakikisha brand inaingia mtaani. Ndio maana umewaona kennedy.

Swala la adam mchomvu clounds pia walipewa deals kutangaza na kipindi pendwa cha vijana xxl kikala shavu. Adam akaibukia hapo.

Juzi tumeona na Mbona hujauliza kuhusu dj joozey kama brand ambassador wa castle lite na sio mtu wa kaskazini
 
TBL ni wabaguzi so kwenye matangazo tu mpaka ajira, wamejaa wajomba , baba mdogo , uncle, mke , wife , demu wangu . Ukienda pale unakuta vikundi vya kikabila vinaongea lugha moja.
Mkubwa ama mtu wa mauzo na masoko anatokea huko huko. Mana hao wenzetu hawana tofauti na wakenya. Yaani wakenya wametuharibia ndugu zetu. Kama vipi tutawauzia wakenya Mana kule watakuwa wanashindanisha Arusha na kericho ama Moshi na kisumu
 
Back
Top Bottom