Tanzania bila vyama vingine vya siasa, ITAKUWAJE?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,353
38,585
Kuna wakati yanakuwamo mawazo kwamba vyama vingine vya siasa ni kama chanzo cha vurugu na vipo kukwaza maendeleo ya nchi yetu. Hivi ikitokea vile vyama vyenye nguvu kama CUF na CHADEMA viongozi wake wakaamua kusalimu amri kwa CCM, hii nchi itakuwaje baada ya hapo bila ya kuwa na vyama vingine vya siasa zaidi ya CCM?
 
sio mara ya kwanza kuishi kwa mfumo wa single part system. multipartism imekuja 1992. nothing news here.

kama ni upinzani utaibuka humohumo ndani kwa ndani.
 
Vyama Vya Ushindani Ni Vizuri Sana Kama Vina Viongozi Wenye Weledi Ila Kwa Hawa Akina DJ Wa Bilcana Utaona Kama Havifai
 
Mpaka sasa mambo mengi yanafanyika kisirisiri hawataki wananchi wajue lakini wapinzani ndo wametujulisha jinsi waliojuu wanavyo neemeka je bila upinzani tungejua yote hayo
 
Vyama vingi inaongeza ufanisi kwenye utendaji wa kazi wa serekali. Upinzani upo ili kukosoa and kuonyesha altenative jinsi ya kufanya vitu.
Vile vile vinawakilisha itikadi za watu tofauti tofauti uwezi kupata kwenye system ya chama kimoja.

Chama kimoja ni sawa na kusema tuwe na kiwanda kimoja cha MAJI ya kunywa "Kilimanjaro", Imagine tungeweza kununua maji kweli.
 
Vyama vya upinzani visipokuwepo askari wenye mamlaka ya juu watakuwa ni wale wa kikosi cha walinzi wa kijani ndicho kitakachokuwa kinafanya kazi ya kukamata.

Lock up na mahakama zitakuwa ni ofisi za CCM,mahakimu watakuwa ni wenyeviti wa matawi wa CCM na makarani watakuwa ni makatibu wa CCM.
 
Back
Top Bottom